Naombeni ushauri ndugu zangu

"Eti kabla mapenzi hayajaota mzizi." unataka mizizi ipi tena wakati tayari mna mtoto. Huyo unaempenda utamtia tena mimba afu utampata tena mrembo zaidi yake. Sijui utakutana na warembo wangapi???
 
Mshkaji utaathiri maisha ya mtoto kama si ya huyo Dada..vuta picha taratibu uzungumze na fikra yako. Urembo wa mwanamke usikuzuzue kwa kuwa utapata sifa kitaa una Mke nzuri,wanaume wa ukweli hawawezi kuacha demu kama huyo wa iringa, akipata MTU anayejua maana utajutia maisha yako ya kimapenzi. Kama huwezi kuwa naye mwambie sasa usichelewe kupoteza muda wake nawe uoe hiyo anayekupendeza muonekano wake ila kichwani hayuko vyemba. Usichezee moyo wa mwanamke jamiimemba.
 
Last edited by a moderator:




mimi kitendo chakuonyesha hanipendi huwa hamu yakuwa naye inaisha gafla kama jinsi hamu yakukaa chooni inavyoisha gafla baada yakujisaidia.
alafu huyo dada kweli hafai kupendwa mwanamme mmezaa hajitambulishi kwenu eti bado unampenda na mkopo wa milioni 7 aisee huyu hamnazo
 
Ninavifahamu ili mapenzi yawe mazuri yadumu, lazima mmoja apende saaana i mean upendwe.

Huko unakotaka kwenda ni ashiki majinuni za wanaume tu.

Mungu atakulaani kumuacha mama na mtoto, havionekani but utajuta siku moja.
 
oa mwanamke anayekupenda kaka.. usije mkumbuka baadaye.!
 

Simlaum sana huyu dada inaonekana kweli anampenda huyu kaka ila ukwel huyu kaka akisema anaishi na huyu dada ndoa haitakuwa ndoa, hamna ndoa hapo sababu kaka anaonyesha hana hata chembe ya mapenzi kwa huyu dada.
 
Post zingine ukisoma unapata hasira sema tu inabidi tuvumulie! Mkuu jamiimemba, acha kujifanya unajua kupenda sana kuliko wenzako! Ni kweli kabisa kwamba busara ya mapenzi inashawishi kwamba fuata kule moyo unakokutuma lakini si mara zote moyo unakuwa upo right... and I hate to say this, more often than not, moyo huwa hauna uwezo wa ku-anticipate for the future coz' unatawaliwa na emotions! Mara zote hakikisha moyo unaupa ushirikiano wa kutosha kutoka kwenye akili zako otherwise, you'll always be a failure! Hata wanyama wa mwituni wanapenda... ajabu hata kuku nao wanapenda na ndio maana si ajabu kuona jogoo linamtoa nduki jogoo mwenzako anayeona anamlia mingo kademu kuku wake! Lakini pamoja na wanyama kupewa uwezo wa kupenda sawa na mimi na wewe, lakini Mungu amewanyima akili zinazotawala utashi na ndio maana wanyama wanawapanda wazazi na binti zao!!

Moyo wako unampenda mtu mwingine... je, umejiridhisha kwamba nae anakupenda kama unavyompenda wewe? Iko hivi! Ni heri kuishi na mpenzi anayekupenda hata kama humpendi kihivyo kuliko kuishi na mpenzi asiyekupenda lakini wewe unam-feel ile mbaya! Case ya pili ni kujitafutia machungu ya kila mara lakini case ya kwanza, itakuwa ni kumtafutia mwenza wako machungu ya mara kwa mara! Lakini kwavile ni wewe mwenyewe utakuwa umeushirikisha ubongo wako kufanya maamuzi, basi kuna uwezekano kwamba hutakuwa chanzo cha maudhi ya mara kwa mara kwa mwenza wako... kinyume chake, huwezi kumfanya yule unayempenda(huku akiwa haja-fall kihivyo kwako) wewe aushirikishe ubongo wake kwa ajili yako wewe...

Mwanamke anakupenda ile mbaya... mbaya zaidi umezaa nae! Si hivyo tu, ni mpenda kujenga badala ya kubomoa! Anaamua kujipiga pini kwa kuchukua mkopo kwa ajili yenu!

Anyway, talk quitely to your heart na kama kweli you feel nothing about her, better you let her go! Usijaribu kuchukua picha zake (kama unazo) ukajaribu kutafuta kitu kitakachokushawishi umpende! Itoshe tu kujiuliza na kuyatafakari kwa kina ni mambo gani ungempenda mke wako awe nayo... haya mambo will never and ever be seen through your heart but your brain, centre of judgement!
 
Last edited by a moderator:
Mpende anaekupenda usimuache kwa ajiri ya huyo uliyemtamani unajua kuwa huyo unayempenda nae anamtu anayempende wewe kakutamani tu.Elewa mapenzi yanatengenezwa tu.
 

We baki na huyo wa O - level huyu wa iringa nipe mm coz nilikuwa natafuta mda mrefu wanawake wanaojitambua kama huyu, usisite kinipm cont zake huyo mwanao tutalea tu usijali.
 
sasa kaka unauhakika unaye mpenda nayeye anakupenda au ndo yaleyale angalia usije ukawa umeokota jiwe ukizani zahabu kila la kheri mapenz siwez kumsemea mtu
 
Mijanaume mingine bhana!Sasa ulipommbimba dada wa watu, kwani hukujua kama kuna kondomu? Umeshamzalisha sasa unamuona hafai! Kama hukua unampenda, ni kwa nini umzalishe? jamiimemba umenikera sana
 
Last edited by a moderator:
Ogoga Kuishi Na Mtu Hauna Upendo Nae Utapata Sheeeedah. Oa Mtu Moyo Wako Umekubali
 
Hakuna kitu muhimu katika maisha kama amani ya moyo. Amini nakwambia.
Tafakari.
 
tunaruhusiwa kutukana katika hii nyuzi


eti founder????
 
Nimegundua kuwa hueshimu hisia zake kama kweli ungekuwa unaheshim hisia zake kwanini utafute mwingine?
Mwingine wa nini sasa wakati unajua wazi kwamba yeye ana hisia nzito kukuelekea?

Na unajua wazi kwamba karibuni atakuzalia mtoto kwanini utafute mwingine? Eti unasema humpendi kwa dhati kwa nini uchezee hisia zake kwa kumdanganya hapo nyuma na kufanya nae ngono?

Anyway tufanye hayo yamepita cha kukushauri ni kuwa ni vizuri usifikirie kumuacha ila uendelee kumtegemeza wakati wote atakapokuwa na ujauzito mpaka kujifungua, halaf mipango mingine ya ndoa na kujenga familia ifuate baada ya hapo.

Nakushauri hivi kwa sababu nimeona hasara zitakazotukia kimbele kwako na kwake pia.
Kwamba utaumiza hisia zake na kudhoofisha utendaji wa kila siku ukizingatia tayari ana uja uzito.
 
Weka Namba Yake,mi Nipo Iringa Nataka Nimshauri Kuhusu Maisha.
 
Mkuu umefanya jambo la mbolea sana kumfafanulia.....kama asipoelewa hapa huyo jamaa atakuwa mtindio wa ubongo na uti wa mgongo..
 
Duh watu mnakosa bahati yani mie nawatafuta wanawake wanajitambuwa na wana akili ya kimaisha siwapati please naomba namba yake mana nipo iringa wacha nijioee fasta wewe endelea na kilaza wako huyohuyo na akuzalie mtoto kilaza iwe familia ya vilaza
 
Ushauri Mkuu ndo Huu juu unataka nn tena. Hakuna Ushauri zaidii ya Huu ktk maisha yako yote.Mpende mwenzio Kama nafsi yako huyu aliekushauri katumwa Na mungu AMINI hivyo ndugu yangu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…