cleokippo
JF-Expert Member
- Dec 21, 2014
- 2,148
- 1,851
we nenda kamsikilizw kisha muelekeze kama ulivuotuelekeza sisiMimi Ni kijana wa miaka 22, mwanafunzi wa chuo kikuu( Dar es Salaam), mwaka wa Pili Shahada ya sayansi ya jamii.
Ukweli Ni kwamba, nimetoka katika familia masikini, Ila nashukuru Sana juhudi za wazazi wangu kunifikisha hapa japokuwa baba Yangu mzazi ameshafariki.
Sasa Kama mnavyofahamu Elimu ya juu huwa Kuna msaada wa kifedha kwa ajili ya malazi na makazi (Helbs)
Nimekuwa nikitegemea pesa hiyo kuendesha maisha yangu! Japokuwa Kuna asilimia 40 Natakiwa kuongeza Kama ada hivyo Basi napambana ili kuweka sawa masuala ya kielimu.
Na Ni wazi kuwa unavyokuwa kijana ndio majukumu yanavyo ongezeka! Nyumbani Ni masikini hivyo nimekuwa nikitoa msaada wa moja kwa moja (Fedha) nashukuru Mungu kwa Hilo, ili maisha yasonge
Kutokana na majukumu kuwa mengi Ni wazi kabisa pesa ya serikali haiwezi kutosha. Hapo ndio juhudi zangu za kuandika huu Uzi zilianza.
Kutokana na kuwa na maisha magumu kuanzia nyumbani mpaka chuoni, ilinibidi nibadilishe mtindo wa maisha ili kufikia ndoto zangu!
Ndipo Safari yangu ya kutafuta kipato Cha ziada ilianza.
1.Nilianza na biashara ya kuagiza samaki( kamabale) kutoka usinge Tabora.
Biashara hii ilidumu kwa mwezi mmoja. Baada ya hapo mzigo wote ulioza na kutoa wadudu.. kwaiyo mtaji wangu wa Thamani ya laki tatu ulipotea. ( Nilipata experience)
2.Nikaamua kuingia kwenye uvuvi!
Safari yangu ya uvuvi ilianza japo sikuwa na uzoefu wa kuogelea rakini nilianza, Tena kwa ustadi ila Nashukuru Mungu nilianza na kumaliza salama.
Kilichonifanya kuacha Ni HiKi!
Siku moja nilikuwa najiandaa kwa ajili ya kwenda kuvua samaki na wenzangu Bahari ya Hindi.. Sasa mida ya saa kumi nilikuwa napeleka dumu la mafuta kwenye Boti. Aisee mbele ya bot usawa wangu, niliona mtu mwenye macho makali sawa na taa akinitazama kwa mbali! Sikuamini Kama Ni mtu Mana nilihisi ni taaa labda. Baada ya kutuliza akili nikagudua Ni mtu.. Ila ukweli nilibaini lilikuwa Ni jini, maana baada ya kunitazama lilizama na kuelekea kwenye kina kirefu, Nilipatwa na wasiwasi Sana, nikamwambia captain (Nahodha) akasema basi. Leo usiende hiyo Ni ishara mbaya kwako (alionekana kujua ukweli) sikuwa mbishi Sana nikaondoka. Safarii yangu ya uvuvi ikaishia hapo.
3.biashara ya kuuza mitumba(ambayo ndio biashara Yangu mpaka Sasa)
Nashukuru sana MUNGU inaenda vizuri..
Ila changamoto ifuatavyo ndio imenifanya nije kwenu wakuu ili kuomba Ushauri.
Leo nikiwa katika harakati zangu!Cr(Class representative) amenipigia simu na kwa ukali akauliza "ivi kwanini umekuwa Mtoro chuoni? Ntakupeleka kwa dean of students (mlezi wa wanafunzi) ufukuzwe chuo"
Kutokana na hasira za Maisha sikutaka kumjibu muda ule Mana tungefika mbali,
Mana historia ya maisha yangu Ni mthiani mzito Sasa nikiangalia Cr wa darasa anafatilia maisha yangu ety kwann siendi chuo! Naumia Sana Mana, Ada Mimi, Kodi Mimi, kusaidia nyumbani Mimi..
Na ukweli Ni kwamba kutokana na majukumu yangu nimekuwa naudhulia Mara chache sana Chuoni.. Ila Namshukuru Mungu performance Yangu iko poa, Mana nachosomea ndio kitu nakipenda
Sasa Basi huyu Cr amesema ety kesho nimfuate nimwambie kwanini siendi Chuo..
Sasa nashindwa kumuelewa Naombeni ushauri nifanye Nini Ndugu zangu.
Mana nikifanya maamuzi naweza kukosea..
Sasa kutokana na ozoefu wenu mnanishauri kijana wenu niishi kwa ratiba ipi ili nifikishe ndoto zangu..
Lakini pia ushauri wowote au maoni yanapokelewa.
Ahsante.
ila anatakiwa aache unoko