Saoka
JF-Expert Member
- Oct 23, 2018
- 405
- 565
Habari za muda huu Wakuu. Niende direct to the point.
Mimi ni kijana umri ni miaka 24 nimemaliza chuo kikuu mwaka jana mwezi wa 9 Ila kiukweli bado sijafanikiwa kupata ajira mpaka hivi ninavyoandika hapa bado na fight popote ili niweze kujishikiza na niweze kupata chochote mkono uende kinywani.
Japokuwa bado nipo kwa wazazi na napata mahitaji yote vizuri tokea nimalize ila nikaamua kujiongeza na kutaka kutoka hapa nyumbani niweze kwenda hata mikoani huko kutafuta njia yeyote ya kujikwamua hata kama sitapata ajira ila nipate pa kujishikiza hata kama ni mchongo (kazi yeyote ya kufanya).
Tatizo lina kuja upande wa wazazi hawataki kabisa nitoke hapa nyumbani na nikisema nijishughulishe na vishughuli vidogo vidogo vya kawaida ila naona bado kama sitafanya kama ninavyotaka kutoka nje ya mkoa kwenda huko kusaka life.
Tatizo linakuja hapo upande wa mzazi hataki nikae mbali na nyumbani kwa kuhofia labda kuteseka au huko niendapo.
Wakuu naombeni mnishauri nitatokaje hapa na ukicheki muda unakwenda na sio vizuri kwa mtoto wa kiume kuendelea kukaa hapa nyumbani. Yaani nakosa kabisa njia ya kufanya.