Naombeni ushauri: Msichana wangu ana mchepuko

Naombeni ushauri: Msichana wangu ana mchepuko

Huyo sio demu wako tena ww ndio umegeuzwa mchepuko

Mh sidhani maana hata akisafiri huwa anaaga anakuja kwangu, na akifika lazma nimpigie bimkubwa wake kumpa taarifa kama kafika
 
Saa nyingine ukisema usikilize moyo tu kuna vitu unakuwa unakubaliana navyo ila madhara yake yanaonekana baadae

Binafsi naona mwanamke anayeweza kutoka kwako akaenda kulala kwa mwanaume mwingine hafai...kama una nia ya kumuoa muoe ila lolote litakalotokea katika ndoa yenu hutatakiwa kumlaumu sana since alishakuonesha true colours zake tangu huku

Kama ningekuwa mimi ningeachana na mtu wa design hiyo...

Asante Kwa ushauri mkuu
 
Habarini wakuu,

Nina msichana wangu mmoja tulianza nae mahusiano toka 2013, katika maisha ya mapenzi baina yetu kuna kipindi cha kati hapo tukagombana, ikabidi kila mmoja akaendelea na ishu zake.

Sasa yeye mwenzangu katika kipindi hicho tulichoachana akatoka na lijamaa huko akapewa kibendi, Mungu akamjaalia akajifungua mtoto wa kiume. Katika kipindi chote toka alipopata ujauzito jamaa aliyempa kibendi alikataa kuhudumia mpaka mtoto alipozaliwa.

Mara baada ya kujifungua huyu msichana akaanzisha tena mahusiano na jamaa aliyemtoa usichana (huyu siye aliyempa kibendi), katika mahusiano yao sijui kilichoendelea lakini niliskia waliachana.

Katika shida shida za utawala huu wa mjomba magu huyu msichana akanitafuta last year and tuka reconcile so akawamsichana wangu tena. Tatizo lilikuja alipotaka nimuoe, mimi sikuwa na tatizo sema kama mtu ninaejielewa ikabidi nifanye uchunguzi (sikutaka kuingia kichwakichwa kwenye ishu za ndoa) kama hana mchepuko huko alipo na ndio hapo nilipojua anatoka na lijamaa lake la zamani.

Ushahidi nilikuwa nao wa kutosha kuanzia messages hadi baadhi ya siku huwa anaenda kulala kwa mchizi, sasa nilipo mconfront kama najua anamchepuko na najua huwa analala kwa mchizi baadhi ya siku msichana alinijia juu kwa maneno mengi akataka tuachane, tatizo sikuwa na nia ya kumuacha ilikuwa tuongee tuyamalize lakini mwenzangu akawa analazimisha tuachane, sasa katika marumbano mimi nikaona isiwe tabu tukapigana chini.

Sasa cha kushangaza jioni yake baada ya kuachana akanitumia message kuniomba msamaha kwa alivyokuwa ananijibu na hataki tuachane kwa hasira, nikamwambia nimemsamehe.

Sasa hapa nipo dilema maana msichana nampenda na yeye ana feelings nasema hivi kwa sababu tunakaa mikoa jirani na kila nikiwa na shida naye nikimpigia aje kesho jua lazima atatia maguu gheto, sijawahi kumwambia aje akazingua au akagoma au akaleta kisingizio cha kutokuja.

Na hata kesho nikimwambia aje huku nilipo atakuja ingawa tumeachana, tatizo hataki kukiri makosa yake na hataki hata kusikia ushahidi niliokuwa nao.

Naombeni ushauri wakuu nimpotezee kimoja au niwe mvumilivu nishee na mchizi?
Ushauri gani sasa kama umeishajua..! Mwache au na wewe tafuta mchepuko mchanganye sample tofauti za vvu..!
 
wewe jamaa ni kilaza sana,yaani wenzako tunavyowasulubu hao wanawake tutakavyo wewe unakuja kututia aibu humu na pumba zako,eti nampenda,unampenda malaya,how does it come?
nilichokigundua jamaa hauna hela,fanya kazi kwa bidii upate pesa hizo shida za moyo wako zitabakia historia!

Kwenye ishu ya kazi na mshiko hapo umekosea maana nafanya kazi kwenye institution ya kigeni na napokea 7 figures
 
mtoa mada sijui ni mtu wa aina gani wewe. Kwa kifupi wewe ndio mchepuko wa huyo demu njia kuu ni huyo mwingine. Halafu demu kazaa na mtu ana jamaa mwingine anakutukana bado tu unataka kumuoa hustuki? au ndio mpaka umwagiwe tindikali usoni ndio ujue hutakiwi?
 
Back
Top Bottom