Naombeni ushauri: Mke wangu amejua kuwa nina mtoto kwa mwanamke mwingine

Aah miongozo ni hadi sisi tuchepuke. Mmenichekesha sana na kina junior
Sioni comments za wazee wa kutoa miongozo hapa.....

"Mi mwanamke akicheat nafukuza"
"Mwamba fukuza hiyo malaya inakuchukulia poa"
" Wanaume kucheat ni nature yetu," nk nk

Wakulungwa toeni mwongozo kwa mkulungwa mwenzenu
 
Pole mkuu hilo ni jambo la kawaida muweke sawa mkeo, msameheane muendelee kulea familia yenu
 
Kama ulimpata mtoto kabla ya ndoa, ulichokosea ni kutomweleza mapema.
Ila kama ulimpata mtoto ukiwa ndani ya ndoa ulikosea sana. Na ujinyenyekeshe kwake.
 
Si ameshaambiwa amfukuze tu mke, mke sio ndugu yake; ndugu yake ni mtoto wake.

Siku hizi michepuko imebuni mbwinu, mtoto anapewa jina la nyumbani kabisa la babu yake. Yaani ndugu wakisikia tu jina, wanasema aah huyu wa kwetu kabisa.
Haya mambo ya kujifanya unampa mtoto jina la kwao mwanaume ni kujiingiza chaka, tena bora umpe jina la Bibi sio babu.
Ref mobeto kamuita mtoto Abdul baada ya muda inajulikana kumbe Abdul sio biological father, mdingi ni nyange....๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Haya mambo ya kujifanya unampa mtoto jina la kwao mwanaume ni kujiingiza chaka, tena bora umpe jina la Bibi sio babu.
Ref mobeto kamuita mtoto Abdul baada ya muda inajulikana kumbe Abdul sio biological father, mdingi ni nyange....
Duh! Aisee
 
Kuna jamaa mmoja naye yalimpata hayo. Uzuri alikuwa na pesa akaenda akamletea mke wake Benzi ya uhakika mwanamke akatulia baada ya kuona hiyo mashini na maisha yakaendelea. Ulichofanya si kizuri hata kidogo lakini mwambie akusamehe na uonyeshe upendo wa dhati kwake.
 
Jomba hebu acha upumbafu, katoto kamoja tu kanakutia jakamoyo kiasi hiko!? Au umeshikiwa akili na huyo mwanamke umuitae mkeo? Mwambie amuulize mama yake namna maisha ya ndoa yalivyo.
 
Back
Top Bottom