Naombeni ushauri kwa yaliyonikuta leo

Naombeni ushauri kwa yaliyonikuta leo

proxy

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
1,481
Reaction score
1,353
Takribani kama miazi 2 sasa nina-date na demu mmoja; tulikuwa tunachati na kupigiana simu na naweza mpigia mpaka hata saa 3 usiku na hamna shida yeyote na tunachati fresh tu, sasa Leo yamenikuta na mimi kama mwanaume nimeamua kushare na nyinyi wana JF wenzangu.

Ipo hivi, ilipofika kama saa moja na nusu hivi usiku nikaamua kumpigia manzi ili aje twende zetu tukapate msosi kwa sababu tumewahi kufanya hivi mara kadhaa, so leo ilikuwa sio kawaida kabisa, nimempigia toka muda huo mpaka saa tatu hivi ananiambia tu kwamba anakuja, mara oooh kuna kitu namalizia nitakuja.

Basi kidume nikaamua kuachana naye; nikiwa njiani naludi nyumbani nikaona simu inaingia yani yeye ananipigia na kuniuliza nipo wapi ili aje na tayari yupo kwenye pikpiki, basi nikamuelekeza nilipo, basi pikipiki inasogea kuja kucheki yupo na jamaa binafsi nilifikiri dereva boda kumbe ni jamaa yake na inaonekana alimtaiti kwa muda wote huo ambao Mimi nawasiliana naye.

Basi jamaa alipokuja akaanza kupaniki na kuanza kuja juu eti kwanini nimempigia yule simu manzi, mara ooh unajua alikua wapi wakati unampigia?

Wakati anaongea hayo yote namchek tu kama Cavu flani hivi, baadaye nikamjibu bro sikia sisi wote hapa tutaonekana makavu tulianza kuwakiana kwa ajili ya huyu mwanamke na nikamwambia kwanza anza kushangaa huyu manzi anaanzaje kuwasiliana na mimi au na wewe wakati ana mtu mwingine anayeweza kuwasiliana nae kama mpenzi?

Baadaye tukaongea tukayamaliza baadae jamaa akawasha pikipiki ili waondoke na demu, demu akawa anasuasua mimi nikamwambia apande waondoke kwa sababu walikuja wote.

Sasa naombeni ushauri, kuna haja ya kuendelea kufanya mawasiliano na huyu demu au nipotezee?
 
Ww unampenda kwani?! Kama hauna shida nae tena mkaushie tu.

Au mjadiliane kama wanaume nani anamalemgo nae ya muda mrefu ndo abaki naye.

Au aulizwe binti anamtaka nani kati yenu.

Tatizo hili
Binafsi sijapiga nilikuwa naendelea kumchezi ,na nilikuwa nampa mialiko mbalimbali kama ya lunch na kadharika ili niendelee kumcheki
 
Binafsi sijapiga nilikuwa naendelea kumchezi ,na nilikuwa nampa mialiko mbalimbali kama ya lunch na kadharika ili niendelee kumcheki
Basi endelea kumcheki huenda anakuelewa au aje ujue mahusiano yanamambo mengi huenda kule alishaona hapaeleweki labda ndo maana na yeye anatafuta makoloni.
 
Mle kinasihara afu tupa kwenye dustbin...demu kavu sana huyo sio muaminifu
 
Basi endelea kumcheki huenda anakuelewa au aje ujue mahusiano yanamambo mengi huenda kule alishaona hapaeleweki labda ndo maana na yeye anatafuta makoloni
Halafu jamaa alivyokuja akajaribu kunielekeza Mimi kwamba niwe mwelewa kwa nini nampigia huyu demu Mara nyingi? Yani kana kwamba nilikuwa najua kwamba yupo nae ,ila nilichomshukuru hakuja kwa Shari maana pasingetosha.
 
Mle kinasihara afu tupa kwenye dustbin...demu kavu sana huyo sio muaminifu
Hv dada naomba nikuulizie hili japo mm nmelisikia tu kwa watu


Kwamba mwanamke akifikia umri wa kujiona yuko tayari kuolewa hushauriwa kua na wanaume hata 2 au3 kama wanaume wanavyofanya kusudi achague yupi ni yupi anafaaa kua nae forever


Je ww ndo ungekua kwenye age hio ungefanyaje?!


Mwisho wa siku sioni kosa la mdada kucheat kupo na sababu ni nyingi
 
Back
Top Bottom