Naombeni ushauri kwa huyu Msichana

proxy

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
1,194
2,000
Wadau habarini za muda huu, mategemeo yangu mu wazima wa afya na mmeanza kusukuma gurudumu la maendeleo baada ya uchaguzi kupita kwa amani.Nije moja kwa moja kwenye mada nina msichana ambaye namtokea taklibani mwaka sasa ni msichana mzuri sio kisura ila kwa tabia.

Huwa nkutananae mala kazaa na kuongeanae ila shida inakuja ukimgusia mahusiano ndio changamoto inapoanza ,yani anaweza kukata hata simu lakini kama mnaongea mambo mengine tofauti na mahusiano mnaweza ongea hata lisaa . Msichana ni mlokole na hoja yake ya msingi ni kwamba hawezi anzisha mahusiano na mtu mwenye imani tofauti na yake .

Huyu ni binti ambaye sijatembea naye ingawa huwa nakutana na kuongea nae mala kazaa na mala ya mwisho nimekutana nae jmosi hii wakati nampelekea zawadi yake ya kuzaliwa.Kwa kawaida huwa nampigia usiku kuanzia saa 4 hadi 5 na tunaongea bila shida ila ukimgusia kuhusu mahusiano ndio tatizo linapoanza.

Wenye uzoefu na hawa wanawake walokole mje tujadili kidogo hii kitu wakuu.
 
Citizen B

JF-Expert Member
May 13, 2019
4,486
2,000
itakuwa kwasababu unamchanganyia 'z' na 'dh' au 'r' na 'l' basi anaona utakuwa unamchanganyia wanawake hata ukimuoa.

Na kwasababu huwezi kuruka paragraph basi utakuwa huwezi kuruka binti mzuri bila kusimamisha.
Tena ubaya anaona hata akuelekezeje huwezi koma maana hata hauna koma kwenye maandishi yako.
 
SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
132,735
2,000
nkutananae - nakutana naye
mala kazaa - mara kadhaa
taklibani - takriban
kuongeanae - kuongea naye
Mala ya mwisho - mara ya mwisho.

Pia jifunze matumizi sahihi ya koma, vituo na aya

Kama tabia yake ni nzuri na unaona anafaa kuwa mke na wewe okoka tu uwe mlokole umuoe muishi kwa amani katika ndoa takatifu na maisha ya wokovu. Ndoa yenu na maisha yenu yatabarikiwa sana.

Kama nia yako ni kumla tu halafu usepe achana naye na ridhika tu na huo urafiki wa kawaida. Usikubali kujibebesha dhambi ya kutumiwa na shetani ili kumwondoa mtu aliyesimama katika wokovu wake na kumkwaza. Madhara yake ni makubwa sana.

Mungu Akupe busara katika hili kamanda
 
Glenn

JF-Expert Member
May 22, 2018
10,363
2,000
itakuwa kwasababu unamchanganyia 'z' na 'dh' au 'r' na 'l' basi anaona utakuwa unamchanganyia wanawake hata ukimuoa.

Na kwasababu huwezi kuruka paragraph basi utakuwa huwezi kuruka binti mzuri bila kusimamisha.
Tena ubaya anaona hata akuelekezeje huwezi koma maana hata hauna koma kwenye maandishi yako.
Fumbafu wewe

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Modrizzy

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
952
1,000
itakuwa kwasababu unamchanganyia 'z' na 'dh' au 'r' na 'l' basi anaona utakuwa unamchanganyia wanawake hata ukimuoa.

Na kwasababu huwezi kuruka paragraph basi utakuwa huwezi kuruka binti mzuri bila kusimamisha.
Tena ubaya anaona hata akuelekezeje huwezi koma maana hata hauna koma kwenye maandishi yako.
Ila walimwengu
 
Modrizzy

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
952
1,000
Unatwanga maji kwenye kinu nyoosha goti hawanaga jema kweny sual la upendo na hawajawah kuruhusu upendo uwaongoze
 
Dongmei

Member
Oct 10, 2020
43
125
Kama hataki kuzungumzia suala la mahusiano huenda yy hayupo tayar kuwa na mahusiano kw xx au labd anaona hamuwezi kuwa wote kutokana sababu mbalimbali kama dini na kadhalika.. ni ngumu mtu kuacha dini yake kwenda nyingine hasa kwa huyo mlokole.. ni wachache xana...

We kama upo serious kwamba unahitaji kumuoa basi mzungumze ni makubaliano yenu wawili ila kama utahitaji kumchezea tu ni bora umuache maan c vzur uingie ktk mahusiano na mtu wakat huna mpango/malengo naye.
 
  • Thanks
Reactions: Pep

proxy

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
1,194
2,000
Kama hataki kuzungumzia suala la mahusiano huenda yy hayupo tayar kuwa na mahusiano kw xx au labd anaona hamuwezi kuwa wote kutokana sababu mbalimbali kama dini na kadhalika.. ni ngumu mtu kuacha dini yake kwenda nyingine hasa kwa huyo mlokole.. ni wachache xana... We kama upo serious kwamba unahitaji kumuoa basi mzungumze ni makubaliano yenu wawili ila kama utahitaji kumchezea tu ni bora umuache maan c vzur uingie ktk mahusiano na mtu wakat huna mpango/malengo naye.
Nina malengo naye mkuu ila suala la kuokoka kwangu ni mtihani sana. Na kuna siku nilimgusia hivyo what if nikaokoka? ,yeye akaniambia kabla ya yote niende kwa mchungaji nikapate ushauri wa kiroho nisije nikaokoka kwa ajili ya kumfuata yeye niokoke kwa ajili ya Mungu kwanza ,nia ya kuwa nae ije baadae.Binti yupo simple na nimeshakaribishwa mara kadhaa kwake kwa chakula ila inapokuja ishu ya mahusiano ni mtihani mkubwa.
 
CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
7,059
2,000
Huyo ushamkosa, temana naye mapema iwezekanavyo.

Tayari keshakuweka kwenye "friend zone" hata kama asingekuwa mlokole ni ngumu mno kukupa kitumbua maana ulianza kwa gia mbovu.

Sema wanawake wanapenda sana attention ya mwanaume, hasa non sexual attentions.

Huyo manzi anafurahia kuwa na Me anayempa attention kama kumpigia sim na kumtext, kumsindikiza mahali, kumpa vizawadi vya hapa na pale bila ya yeye kutanua miguu yake. Kwahiyo kwake wewe ni dili ingawa ni hasara kwako.

Ukiendelea kumganda utashangaa siku anakutumia kadi ya harusi yake. Kingine koma kumtongoza manzi ambaye hajaonesha dalili za kukupenda.
 
kijana15

JF-Expert Member
Apr 25, 2011
800
250
Huyo nenda naye taratibu haja kolea kwako, na usimgusie kabisa mambo ya uhusiani ila usimpr nafasi yakuwa mbali na wewe, yaani hakikisha unakiwa naye karibu mara kwa mara , akikolea utaona mwenyewe anataka uhusiano
 
  • Thanks
Reactions: Pep

James Comey

JF-Expert Member
May 14, 2017
5,839
2,000
nkutananae - nakutana naye
mala kazaa - mara kadhaa
taklibani - takriban
kuongeanae - kuongea naye
Mala ya mwisho - mara ya mwisho.

Pia jifunze matumizi sahihi ya koma, vituo na aya

Kama tabia yake ni nzuri na unaona anafaa kuwa mke na wewe okoka tu uwe mlokole umuoe muishi kwa amani katika ndoa takatifu na maisha ya wokovu. Ndoa yenu na maisha yenu yatabarikiwa sana.

Kama nia yako ni kumla tu halafu usepe achana naye na ridhika tu na huo urafiki wa kawaida. Usikubali kujibebesha dhambi ya kutumiwa na shetani ili kumwondoa mtu aliyesimama katika wokovu wake na kumkwaza. Madhara yake ni makubwa sana.

Mungu Akupe busara katika hili kamanda
Good one
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom