Wanaume siku hizi tumekua watu wa kulia lia kama watoto, hata wanawake wanatushangaa, yaani mtu sio mke wako anakuendesha hivyo na hata kama angekua mke wako ndio akuendeshe hivyo na wewe unachekelea tu.
Mara akutemee mate,akutukane,akunyanyase bado tu umemng'ang'nia, ashagundua huna jinsi au ulimpata kwa bahati sio level yako na wewe hutaki kuganduka acha akuendeshe na mimi nasema akuendeshe tu mara maana sasa hakuna namna nyingine, tumechoka.
Huyo mwanamke ukimuoa si atakuwekea kidole kwa mtindo huo, na wewe mbona umemganda sana kwani huwezi kupata mwanamke mwingine kwa nini ukomae nae hivyo?yaani hadi unatishiwa kifo wewr upo tu, unatishiwa kurogwa ambayo ingekua tiket ya kuachana nae wewe upo tu.
Hataki wazazi wako wewr umemganda tu tena sio mke wako wewe upo tu.