Naombeni ushauri katika hili

Naombeni ushauri katika hili

Joined
May 5, 2015
Posts
29
Reaction score
1
Nina miaka 28 kwasasa, ni university graduate na nimeajiriwa serikalini. Nina mwanamke ambaye bado hatujafunga ndoa lakini pia bado hata nyumbani kwao sijajitambulisha. Naye pia ni graduate na yupo kazini pia. Umri wake ni 25yrs, kwa ufupi tulikutana chuoni na tuna miaka kama minne hivi and we have been blessed with a lovely and precious daughter aged 3yrs now. Ok kilichosababisha niandike uzi huu ni kutokana na anayonifanyia huyu mwenzangu, kwa kipindi chote hicho its only 3 months labda ndio nilienjoy mapenzi naye.

1. Haishi kunitukana matusi ambayo yameenda beyond hata kuhusisha wazazi wangu.

2. Alishanitishia nikicheza ataniua kisirisiri au anifanye msukule, nilijipa moyo haiwezekani.

3. Kila ninachonunua anasema ni chetu hata kama hajui nimenunuaje mfano nimenunua uwanja na nishaanza kujenga, sijawahi kumuonesha ila niliwahi kumwambia kuwa nina mipango hiyo surprisingly hajigusi kuhusu hilo lakini kila siku anasema nyumba yetu ikiisha sijui atanya hivi mara vile.

4. Yupo busy na simu yake mara whatsapp sijui FB hata kama ni usiku. Tatizo nikijaribu kuwa busy na simu yangu analeta ugomvi.

5. Pesa zake hataki nijue anafanyia nini wala nisiulize. Kwani nikuliza ni ugomvi.

6. Habari za wazazi wangu hataki kuzisikia kabisa.

7. Kubwa zaidi ilishafika siku akanitemea hadi mate mbele ya wadogo zangu wa kike.

8. Nanii yenyewe napewa kwa masharti mpaka siku apende yeye.

9. Akijua nina pesa anataka mpaka iishe ndio aridhike. Note. Bado sijamuoa rasmi and regardless of all these anasisitiza nimvishe pete ya uchumba na nyumbani kwao niende.

Real nimepata hofu na sina hamu ya kumuoa sababu nahisi she is hunting marriage coz topic kubwa kwake ni ndoa hasa anapoona rafiki zake wamepost may be engaged au wedding pictures.

Kwa haya yote natamani kuachana naye lakini hataki kusikia hilo. Mind u, for the whole time i have been playing role kama baba na mama yake.

Naombeni ushauri wana Jf nifanyeje? Moyo umekufa sina hamu ya mapenzi kwa haya yote na mengine mengi na sioni kama ninaweza kufurahia mapenzi tena.
 
Wanaume siku hizi tumekua watu wa kulia lia kama watoto, hata wanawake wanatushangaa, yaani mtu sio mke wako anakuendesha hivyo na hata kama angekua mke wako ndio akuendeshe hivyo na wewe unachekelea tu.

Mara akutemee mate,akutukane,akunyanyase bado tu umemng'ang'nia, ashagundua huna jinsi au ulimpata kwa bahati sio level yako na wewe hutaki kuganduka acha akuendeshe na mimi nasema akuendeshe tu mara maana sasa hakuna namna nyingine, tumechoka.

Huyo mwanamke ukimuoa si atakuwekea kidole kwa mtindo huo, na wewe mbona umemganda sana kwani huwezi kupata mwanamke mwingine kwa nini ukomae nae hivyo?yaani hadi unatishiwa kifo wewr upo tu, unatishiwa kurogwa ambayo ingekua tiket ya kuachana nae wewe upo tu.

Hataki wazazi wako wewr umemganda tu tena sio mke wako wewe upo tu.
 
Jitahidi tu ulee binti yako, hakuna mke hapo wakati kama huu angetakiwa aonyeshe upendo, heshima na unyenyekevu wa hali ya juu kwako lakini imekuwa ni kinyume sasa ukishamuoa si ndiyo itakuwa balaa ndani ya nyumba. Kila la heri katika maamuzi yako.
 
Kijana acha kulia lia...

Kwa namna ulivyoeleza inaonesha kabisa hakuna mbele baina yenu...

Na tayari inaonekana ushafanywa msukule maana hata maamuzi magumu washindwa yafanya...
 
Ushauri wangu ni mgumu sana bora nikae kimya tu wengine wakushauri.
 
The Unknown wanasema subira yavuta heri, nilikuwa nasubiri heri lakini siioni. And then nadhani nilikuwa so connected to my daughter bt now nadhani i have to decide.
 
Hivi huko shule mnaendaga kusomea ujinga?ni aibu mtu kuomba ushauri kwa jambo kama hli then unajiita graduate.una tofauti gani na deiwaka wa mtaani sasa?
 
Uwe msukule Mara ngapi? washirikishe ndugu zako na hata viongozi wa dini. maaaaasikiiiiin poole
 
Mara nyingi kwenye mahusiano ukiona maudhi ni mengi kuliko raha jua tu huyo mtu sio wako,ukilazimisha ukamuoa baadae utajuta,jali furaha yako kwanza
 
Kijana acha kulia lia...

Kwa namna ulivyoeleza inaonesha kabisa hakuna mbele baina yenu...

Na tayari inaonekana ushafanywa msukule maana hata maamuzi magumu washindwa yafanya...

Huyu wala haitaji maamuzi magumu, alipaswa kufanya maamuzi laini tu, mepesi, ila kwa kuwa kashafanywa msukule basi tena.
 
Tang'ana don't say so coz degree haina impact katika hili. Yeyote anaweza kushauri hili and get it no one knows everything hata kama una masters degree.
 
Jamani hizi habari za kutunga muwe mnazipangilia vizuri na cyo kukurupuka kupost vitu vinavyowadhalilisha.
Kwanza kwa maelezo yako tu inaonesha kuwa wewe kwake ni zezeta na hauna ujanja wa kumkatalia ndoa huyo mwanamke, Inavyoonekana ni kwamba huyo mwanamke hana mpango wa kuishi na wewe au hajaamua kukuhalalisha kama Mume wake.

Wewe huna ujanja wa kuchomoka kwenye makucha ya huyo mwanamke.
 
Ryad siamini kama nimekuwa hivyo unavyosema i believe in one and the only living God naamini sitafika huko.
 
Mkuu pole sana ila pia nikusifu kwa uvumilivu wako mpaka hapo ulipofikia,sijui uhakika pia wa umiliki halali wa huyo mtoto wako maana kwa namna anavyokuchukulie huyo bibie ndipo ninapokuwa na shaka juu ya umiliki wako halali wa huyo mtoto.
Kiukweli sioni ukiwa na amani katika ndoa utakayoiingia na huyo mwana mama,hapo kuna moja kati ya mawili
1:Kuoa uishi kwa shida na ufe mapema
2;Kuachana naye uishi kwa raha maisha marefu pia.
Ila hilo la pili la mhimu zingatia mkuu.
 
Back
Top Bottom