jmapunda
JF-Expert Member
- Jul 9, 2015
- 731
- 2,923
Wandugu,nilijiapia mwaka huu sitaki tena mambo ya michepuko lakini naona nimewekwa majaribuni.Tena na demu wa jamaa jirani yangu tu.Sina mazoea naye ya ki vilee...lakini siku za karibuni hapa akaanza kunizoea kwa kasi ya kutisha.Akanilazimisha eti tupinge kuhusu nani atafungwa kati ya hizi timu zetu mbili.Ambaye timu yetu itafungwa ampe mwenzake elfu hamsini.Timu yake ndiyo iliyopoteza.Sasa ajabu badala ya mimi ndiye nimsumbue anilipe hiyo hela,yeye ndiye muda wote ananipigia kwamba hana hela ya kunilipa ila yupo tayari kunifanyia chochote kile nachotaka.Eti hata kama jambo la siri yeye ataitunza ili tu roho yake iwe na amani.Jamani nimevurugwa kweli sijui mnasemaje maana kama uzuri tu anao wa kuzaliwa.Naomba ushauri wa kujenga siyo sijui nini inahusika.