kumbuka mdada namlipa mshahara, kila mwezi, kama ambavyo mimi nalipwa mshahara na bosi wangu na kwenye mshahara wangu sipewi hela ya airtime. ninapopata dharura kupigia ndugu/jamaa na marafiki huwa natumia mshahara wangu. nilitegemea yeye pia akitaka kuwasiliana na ndugu zake atumie mshahara wake. ile ninayompa mimi ni kwa ajili ya kuwasiliana nami
nafikiri hujanielewa,
kwa uzoefu wangu mabinti wa kazi hata umetengee 50000 ya simu itaisha pasikupigiwa tena atakua anazirusha hadi kwa wenzie.
cha msingi kama bint ana simu, basi asimpe yake iwe ya kuwasiliana na wenzie yake inatakiwa iwe ya matumiz ya nyumbn kwake
ha haaaa, ni bora kubaki hivyo hivyo
mkuu mabint adha zao wajua wamama, huyu hata ukimuunga kifurushi cha elfu 10 kwa wiki, itaisha ndani ya siku mbili, kazi hazifanyika, ye anapiga kila atakayembip huko kwao na vijana wa mtaani ndo anawapigia yeye,kifupi hata mtoto hataangaliwa maana anauwezo wa kuongea na simu hata saa 2 na zaidi mfululizo. hapa namsemea msaidizi wangu .cjui ka na huyu yupo hivyo
Rafiki, tunawaachia hawa wasaidizi nyumba zetu, watoto wetu na mali nyingine chungu nzima ndani ya nyumba zetu. Wanatupikia na kufanya kazi nyingine mbali mbali ili kutusaidia katika maisha yetu ya kila siku. Hivyo inabidi tuwathamini na kuwaona kama ni part and parcel ya familia zetu badala ya kuwaona kama ni watu baki na hivyo kuwawekea sheria lukuki, sheria ambazo kama wangekuwa ni ndugu zetu wa damu zisingekuwepo kabisa.
Kama hutaki kubadilisha wasaidizi wako kila baada ya miezi michache basi wasome kwa makini sana akina Miss Kim, Toria na Eiyer na ufuate ushauri wao. Pia badala ya kusubiri mdada akupigie wewe jitahidi katika kila saa kutafuta dakika tano kumpigia ili kujua hali nyumbani ni shwari. Hawa watu ukiwazingua sana kwa sheria lukuki basi wanaweza kabisa kufanya lolote lile ili kukukomoa na kubaki na majuto ni mjukuu.
Good day 🙂🙂🙂
Mwanangu ananifurahisha tukirudi jioni anatoa taarifa ya kila kitu ambacho sio cha kawaida kilichotokea home
Eiyer anaongea points sana...
Kuna watu wanajifanya hawamuelewi...
This man is brave and Bright...
akina mama msikilizeni huyo jamaa...he is having a point to be taken there,kuwa mwanamke sio kujua kila kitu kuhusu hawa beki tatu...!
CC gfsonwin Fixed Point etc..
Mkuu hawa dada/mama zetu wakati mwingine wanatupa kazi sana kuwaelewesha
Lakini taratibu watatuelewa tu
Pamoja saana ..!!
My mdogo, unajua namlipa shilingi ngapi?My dada; one thou a week na ikiisha hutaki akubeep ni mtihani
opt1.. 2500 mon-frdy mwekee jero jero. opt2.. hiyo buku iwe ni ya kukubeep kila kunapotokea tatizo
Hii mishahara ya ma hg ni midogo mnoo jaman ukilinganisha na mahitaji ya mwanamke mnawabana sana ndo mana wanafanyaga makasheshe at the end
You know mabinti wa kazi very well.mkuu mabint adha zao wajua wamama, huyu hata ukimuunga kifurushi cha elfu 10 kwa wiki, itaisha ndani ya siku mbili, kazi hazifanyika, ye anapiga kila atakayembip huko kwao na vijana wa mtaani ndo anawapigia yeye,kifupi hata mtoto hataangaliwa maana anauwezo wa kuongea na simu hata saa 2 na zaidi mfululizo. hapa namsemea msaidizi wangu .cjui ka na huyu yupo hivyo
umeni-judge kwa vitu nisivyovifanya......Fixed Point!
Fixed Point!
Fixed Point!
Back 3 ni binadamu kama binadamu wengine!
Wanainterests and/or mahitaji kama walivyo binadamu wengine!
Na ni wafanyakazi kama wafanyakazi wengine (like you!)
Ivi kwa mujibu wa maelezo yako hapo reds, Unamtofautisha vipi back 3 na Mtumwa?
Ivi unakubali wafanyakazi wote watritiwe kama maelezo yako ya second red?
In treatment, unawatofautisha viki wafanyakazi wa ndani na wafanyakazi wengine?
Plz Fixed Point treat your back 3 like your children in reasonable manner!
Hako karesearch ulikokafanya ndio kanakutia matatani dhidi ya hao/huyo back 3 wako thus why unaquestion vocha ya Buku 1 kwa wiki dhidi ya back 3 wako!
Change your mind! Treat them like a human, im sure utakuja kuleta ushuhuda hapa!
well said rafiki.....well, sijui ni kwasabb ya uzee ama??
binfs napenda sana kuona mtu anaheshimiwa lkn nikionacho kwa waajiri wengi wa beki 3 hushindwa kutofautisha kati ya beki 3, na mtu mwingine hapo nyumban. sababu kubwa ni kwamba huona kama beki 3 anatakiwa kubembelezwa na atritiwe kama yai jambo ambalo pia hawawez kulifikia.
beki 3 anatakiwa apewe majukumu yake na atambue kwamba yupo kazin na alipwe kulingana na mapatano, mpaka uwepo kati yake na mwajiri wake kazi zake zirasimishwe kama wafanyavyo wahindi mbona hua wanakaa muda mrefu na kw nidhamu sii wabongo kwa kujtia umalaika ndo tunakutanaga na haya.
Karibu airtel yatosha package..but Tafuta wataalam simu ifanyiwe settings ipige namba fulani tu...namba zingine haipigi
Mke wangu mwenyewe ana itikadi hizohizo...hii tabia inanikera kuliko zote duniani...!
Wanasahau maisha ya wanafamilia yapo mikononi mwa beki 3,anaweza akawapoteza wote wakati wowote...
Lazima tuishi nao kibinadamu...!
Kabla haujaliona hilo kama tatizo na kuja kuomba muongozo ulipaswa kwanza kujichunguza ili ugundue kikwazo ni kipi.
Pili yakupasa kuelewa kwamba mdada wakazi na yeye pia ana maisha yake anahitaji kuwa huru kufanya baadhi ya mambo yake ambayo hayatavunja misingi ya kazi yake, katika hili swala lako yapo mambo mengi sana ya kuyatazama kiundani zaidi, umedai mara kwa mara huwa unapiga simu sitaki kuuamini kwamba hizo dharura huwa zinategea na kutokea wakati ambao haupigi simu.
Tatizo liko kwenye mitazamo yenu na jinsi mnavyo wachukulia hao wadogo zetu wanapokuja kuwafanyia kazi huko majumbani kwenu, kwanza kabisa kiasi cha pesa mnachowalipa hakiendani kabisa na majuku mnayowatwisha, na pia hauwezi kugharamia mahitaji yake yote, haiitajiki kuchukua maelezo yako mengi ili mtu akusome jinsi unayoishi na binti yako wakazi, kwa maelezo hayo tu inaonesha na wewe ni mmoja kati ya watu wanaoishi na wadada wandani kwa kuwaendesha kama magari mabovu huku mkiwalipa kiasi kidogo cha pesa.
Nafikiri ungekuwa unamlipa kiasi kizuri cha pesa hata usingekuwa unatoa hiyo 1000 kwaajili ya simu, angeweza kulimudu hili kwa vile na yeye mawasiliano kwake ni muhimu kwa ndugu na jamaa zake. kama kweli kiasi cha pesa unachomlipa kinamtosheleza na hiyo 1000 unayotoa, swali la kujiuliza ni kwamba je, ni mzembe kutoa taarifa inapotokea dharura? kama jibu ni hapana, na sababu ni simu haina vocha basi tunarudi kule kule kwenye malipo unayomlipa ni kidogo.
Kweli pesa ni ngumu, na hakuna pesa ndogo, pia ukidharau mia hauwezi kupata 1000, hivyo bajeti ni muhimu swala la msingi ni je kiasi cha bajeti yako kinatosheleza mahitaji ya dada wa nyumabani?...
Swali la kizushi..
Ikitokea huyo mdada wako wa kazi akawa anakupigia simu mara kwa mara hata kama dharura haijatokea na mara nyingine awe anakurushia salio hata 1500, wakati huo wewe huwa unamuachia 1000 kwa wiki, utajifikiria nini juu ya huyo mdada? na utachukua hatua gani?
CC; kiwatengu , The Boss , Mrigariga, ICHANA , Nokia83 , dyuteromaikota , hips.com , Caroline , danzi , Munambefu , Mashaxizo , everlenk , Joseph , Bulldog , Eiyer, Mr mgeni, stroke, byb sac, gfsonwin, Honey Faith, bornagain, thinky, isha, Miss Kim, frank wa moyo, Chauro, Mbu, Escardo-bird, Natanguliza samahani kwa usumbufu kwa kuwakusanya hapa, kilichonifanya niwakusanye hapa naomba muwe watazamaji atakacho nijibu Fixed Point