Naombeni mwongozo

mamito usihangaike sana kumjibu Miss Kim, naona bado hajafikia mahala pa kukaa na maid, siku akifikia atakuja hapa na hoja tofauti
Thank you rafiki....
Unajua namwelewa sana Eiyer anaposema haya sababu ni mwanaume......
Mimi pia enzi zangu kabla sijawa na nyumba na kuanza kuishi na hawa watu nilikuwa nawaza kama Miss Kim ninapotembelea kwa ndugu zangu wenye mahg, na sasa nina mwelekeo tofauti kabisa na wa enzi zile
 
Last edited by a moderator:
napenda sana msimamo wako juu ya haki za binadamu na hasa heshima kwa kila mtu.

naomba nikuulize hivi umewah kukaa na maid ww??nikimaanisha kwamba wew ndio bosi wake?

kama ndio wangapi toka uanze kuajiri??

Nashukuru. Ndio nina msichana wa kazi na huyu ni wa pili toka nianze kuajiri (3 yrs ago). I have a boy aged 3yrs old so nilihitaji mtu wa kukaa na mtoto wangu while i am away at work. I usually don't take anyone younger than 18yrs old coz hao under-age wanasumbua sana. Msichana wangu wa kwanza aliondoka after a year and a half na akaenda kuanzisha mji wake. In between i worked as a househelp miaka ya nyuma so nafahamu fika mnayoyazungumzia hapa mpenzi.
 

I am a single parent to a beautiful baby boy so naelewa fika mnachokisema hapa mpenzi. As a single parent hakuna mtu ninaye mdhamini kama msichana wangu wa kazi coz i know without her sitoweza kufanya shughuli zangu za kila siku kwa amani. She's my family and we live like one happy family, mtu akija pale nyumbani huwezi jua kama ni msichana wa kazi ama mdogo wangu. My son loves and respects her like his own and i treat her like my own.
 
mwambie hii hela nnayoweka jtatu marufuku kupiga kwa yeyote zaidi ya kunibip mimi, ikitokea imebaki jpil utapiga kwa nduguzo, jtatu ntaweka tena
 
My dada; one thou a week na ikiisha hutaki akubeep ni mtihani

opt1.. 2500 mon-frdy mwekee jero jero. opt2.. hiyo buku iwe ni ya kukubeep kila kunapotokea tatizo

Hii mishahara ya ma hg ni midogo mnoo jaman ukilinganisha na mahitaji ya mwanamke mnawabana sana ndo mana wanafanyaga makasheshe at the end
 

acha ubahili. Iunganishe hiyoo simu kifurishi cha wiki. Elfu kwa week this z bullshit.
 

mkuu mabint adha zao wajua wamama, huyu hata ukimuunga kifurushi cha elfu 10 kwa wiki, itaisha ndani ya siku mbili, kazi hazifanyika, ye anapiga kila atakayembip huko kwao na vijana wa mtaani ndo anawapigia yeye,kifupi hata mtoto hataangaliwa maana anauwezo wa kuongea na simu hata saa 2 na zaidi mfululizo. hapa namsemea msaidizi wangu .cjui ka na huyu yupo hivyo
 

Fixed Point!
Fixed Point!
Fixed Point!

Back 3 ni binadamu kama binadamu wengine!

Wanainterests and/or mahitaji kama walivyo binadamu wengine!

Na ni wafanyakazi kama wafanyakazi wengine (like you!)

Ivi kwa mujibu wa maelezo yako hapo reds, Unamtofautisha vipi back 3 na Mtumwa?

Ivi unakubali wafanyakazi wote watritiwe kama maelezo yako ya second red?

In treatment, unawatofautisha viki wafanyakazi wa ndani na wafanyakazi wengine?

Plz Fixed Point treat your back 3 like your children in reasonable manner!
Hako karesearch ulikokafanya ndio kanakutia matatani dhidi ya hao/huyo back 3 wako thus why unaquestion vocha ya Buku 1 kwa wiki dhidi ya back 3 wako!

Change your mind! Treat them like a human, im sure utakuja kuleta ushuhuda hapa!
 
kabla hajaanza kazi mnawekeana terms maana hakuna jinsi lazima uwasiliane nae. mwambie nakupa hela ya simu kwa ajili ya kunipigia kama kuna dharura ukiitumia vinginevyo nakata mshahara wako mara tano ya hiyo(1000) halafu ona kama itasaidia maana najua ataogopa
 

well, sijui ni kwasabb ya uzee ama??
binfs napenda sana kuona mtu anaheshimiwa lkn nikionacho kwa waajiri wengi wa beki 3 hushindwa kutofautisha kati ya beki 3, na mtu mwingine hapo nyumban. sababu kubwa ni kwamba huona kama beki 3 anatakiwa kubembelezwa na atritiwe kama yai jambo ambalo pia hawawez kulifikia.

beki 3 anatakiwa apewe majukumu yake na atambue kwamba yupo kazin na alipwe kulingana na mapatano, mpaka uwepo kati yake na mwajiri wake kazi zake zirasimishwe kama wafanyavyo wahindi mbona hua wanakaa muda mrefu na kw nidhamu sii wabongo kwa kujtia umalaika ndo tunakutanaga na haya.
 



".....Most of the things you worry about won't happen!"​
 
Reactions: BAK
Usimpe hela muunganishe kwenye kifurushi cha mwezi mwezi cha messages i hop hata maliza sms zote za kifurushi then mueleweshe kukiwa na emergence home akuandikie msg afu wewe utapiga na kama yeye akitaka kuongea na watu wake atajinunulia mwenyewe airtime.
 

Kabla haujaliona hilo kama tatizo na kuja kuomba muongozo ulipaswa kwanza kujichunguza ili ugundue kikwazo ni kipi.
Pili yakupasa kuelewa kwamba mdada wakazi na yeye pia ana maisha yake anahitaji kuwa huru kufanya baadhi ya mambo yake ambayo hayatavunja misingi ya kazi yake, katika hili swala lako yapo mambo mengi sana ya kuyatazama kiundani zaidi, umedai mara kwa mara huwa unapiga simu sitaki kuuamini kwamba hizo dharura huwa zinategea na kutokea wakati ambao haupigi simu.

Tatizo liko kwenye mitazamo yenu na jinsi mnavyo wachukulia hao wadogo zetu wanapokuja kuwafanyia kazi huko majumbani kwenu, kwanza kabisa kiasi cha pesa mnachowalipa hakiendani kabisa na majuku mnayowatwisha, na pia hauwezi kugharamia mahitaji yake yote, haiitajiki kuchukua maelezo yako mengi ili mtu akusome jinsi unayoishi na binti yako wakazi, kwa maelezo hayo tu inaonesha na wewe ni mmoja kati ya watu wanaoishi na wadada wandani kwa kuwaendesha kama magari mabovu huku mkiwalipa kiasi kidogo cha pesa.

Nafikiri ungekuwa unamlipa kiasi kizuri cha pesa hata usingekuwa unatoa hiyo 1000 kwaajili ya simu, angeweza kulimudu hili kwa vile na yeye mawasiliano kwake ni muhimu kwa ndugu na jamaa zake. kama kweli kiasi cha pesa unachomlipa kinamtosheleza na hiyo 1000 unayotoa, swali la kujiuliza ni kwamba je, ni mzembe kutoa taarifa inapotokea dharura? kama jibu ni hapana, na sababu ni simu haina vocha basi tunarudi kule kule kwenye malipo unayomlipa ni kidogo.

Kweli pesa ni ngumu, na hakuna pesa ndogo, pia ukidharau mia hauwezi kupata 1000, hivyo bajeti ni muhimu swala la msingi ni je kiasi cha bajeti yako kinatosheleza mahitaji ya dada wa nyumabani?...

Swali la kizushi..

Ikitokea huyo mdada wako wa kazi akawa anakupigia simu mara kwa mara hata kama dharura haijatokea na mara nyingine awe anakurushia salio hata 1500, wakati huo wewe huwa unamuachia 1000 kwa wiki, utajifikiria nini juu ya huyo mdada? na utachukua hatua gani?

CC; kiwatengu , The Boss , Mrigariga, ICHANA , Nokia83 , dyuteromaikota , hips.com , Caroline , danzi , Munambefu , Mashaxizo , everlenk , Joseph , Bulldog , Eiyer, Mr mgeni, stroke, byb sac, gfsonwin, Honey Faith, bornagain, thinky, isha, Miss Kim, frank wa moyo, Chauro, Mbu, Escardo-bird, Natanguliza samahani kwa usumbufu kwa kuwakusanya hapa, kilichonifanya niwakusanye hapa naomba muwe watazamaji atakacho nijibu Fixed Point
 
wanawake wengi wapo hivo....unaweza mtumia vocha ya elf 5 akakuandikia msg moja tu ya 'thanx'. baada ya hapo husikii chochote mpaka vocha uliyompa iishe ndo atabeep then anaomba vocha

Mbaya zaidi kwenye whatsapp unaona yuko online lakini msg huoni, Hahahahaaaa:sly: chezeya!!
 
Rafiki, tunawaachia hawa wasaidizi nyumba zetu, watoto wetu na mali nyingine chungu nzima ndani ya nyumba zetu. Wanatupikia na kufanya kazi nyingine mbali mbali ili kutusaidia katika maisha yetu ya kila siku. Hivyo inabidi tuwathamini na kuwaona kama ni part and parcel ya familia zetu badala ya kuwaona kama ni watu baki na hivyo kuwawekea sheria lukuki, sheria ambazo kama wangekuwa ni ndugu zetu wa damu zisingekuwepo kabisa.

Kama hutaki kubadilisha wasaidizi wako kila baada ya miezi michache basi wasome kwa makini sana akina Miss Kim, Toria na Eiyer na ufuate ushauri wao. Pia badala ya kusubiri mdada akupigie wewe jitahidi katika kila saa kutafuta dakika tano kumpigia ili kujua hali nyumbani ni shwari. Hawa watu ukiwazingua sana kwa sheria lukuki basi wanaweza kabisa kufanya lolote lile ili kukukomoa na kubaki na majuto ni mjukuu.

Good day πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚
 
Last edited by a moderator:
Seriously?!!! Kweli some people are soo narrow minded!!! Hivi vitu vidogo vidogo kama sanitary pads, cjui ndala, chakula na soda unavihesabia kama favours unazompa msaidizi wako wa ndani?! Lord have mercy!

Ila naona wewe upo shallow.ila vijisheria vyangu vinanifanya nikae nao muda mrefuπŸ˜€.poleee weee
 

mfundishe huduma ya tafadhali nipigie...mpe mazoezi ya kufanya hivyo angalau mara moja kwa siku....
 

Aisee! kwa binadamu anaefikiri vizuri kabisa hawezi kuwaza kama unavyowaza wewe, labda kama anamatatizo ya kufikiri.

Kama binadamu mwenzako unaweza kumhesabia hivyo kwa vile tu ni dada wa kazi, itakuwaje kwa ndugu wa mume utakao ishi nao hapo nyumba wakiwa hawajishughulishi na chochote? nafikiri lugha tamu ya kuwakilisha kilio chako hapa itakuwa "WANAJAZA CHOO"

Kwa mitazamo hii nawapa pole wadogo zangu wote awanaofanya kazi kwa watu wanao fikiri kama wewe.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…