naombeni msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

naombeni msaada

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by wingman7, Sep 6, 2012.

 1. w

  wingman7 JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  nimefeli 4m4 mwaka jana nimepata divisio 4. Naombeni msaada nijiunge na coz gani ili nipate ajira nzuri.
   
 2. Kisumbo

  Kisumbo Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Hotel management VETA Chang'onbe
   
 3. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  funguka ndugu yangu, umepata division 4 ya point ngapi? hesabu na kiingereza umepata A,B,C,D or F?
  Kwa mfano ukiwa na division 4 point 28 hadi 26, unaweza kupata ualimu, unaweza kusoma cheti cha uhasibu,procurement pale CBE na TIA, na kozi zingine VETA. Ukiwa umefaulu hesabu, English na Biology unaweza kusoma cheti cha nursing ktk vyuo vya nessing kiomboi sgd na vingine vingi(hii ni ajira moja kwa moja)..... changamkia kusoma kama una vigezo tafadhali
   
 4. i

  itagata JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Pole sana dogo, but nakata kukwambia kuwa kupata Division Four sio mwisho wa safari katika elimu, bado una uwezekano mkubwa wa kuendelea katika elimu kama utahitaji kufanya hivyo. kwa mfano kama umepata Division 4 na una pass 3 namaanisha D 3 unaweza kuanza kusoma basic certificate katika chuo cha St. John university kwa kuchukua certificate ya Business administration, chuo cha Utumishi wa Umma TPSC unaweza kusoma koz mbalimbali kama Record Management, Public and Local Administration na nyingine nyingi tembelea hapa www.tpsc.go.tz utapata information zao nyingi tu.

  Pia kama umepata D4 katika matokeo yako, unaweza kujiunga na chuo cha Mipango www.irdp.ac.tz kusoma certificate ya Rural development Planning ambazo zitakusaidia kuendelea na elimu ya juu hadi Diploma. na pia kama kwenye matokeo yako una pass 5 nikimaanisha A,B,C,D 5 unaweza kujiunga kusoma Diploma katika chuo cha St. john www.sjut.ac.tz ambayo itakusaidia kujiunga na degree baada ya kumaliza mafunzo yako.

  Kimsingi kama ulipata pass 2 tu katika matokeo yako, ikimaanisha ulipata division 4 ya point 33 ndo unakuwa katika wakati mgumu na inakulazimu kurudia mtihani wako. But kama ulipata pass 4 au 3 una uhakika wa kusoma mpaka Diploma Level ukianzia Certificate course lakin sina uhakika kama unaweza kujiunga na Bachelor, lakini ukiwa na Pass 5 unaweza kuendelea mpaka bachelor level, tembelea www.nacte.go.tz utapata maelezo zaidi.

  Usipate shida dogo na usikate tamaa, bado una nafasi ya kusonga mbele, watu walio wengi wanashindwa kuelewa kuwa kupata division 4 sio kufeli kiasi cha kukata tamaa, ila ninachojua mie kufeli ni kupata division 4 ya point 33, hivyo unatakiwa kusema kuwa umepata division 4 ya point ngapi ili tuweze kukusaidia.
   
 5. w

  wingman7 JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Nikienda kusomea travel agency ni vibaya
   
 6. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180

  Dogo weka kwanza umepata Division 4 ya points ngapi??kuna watu wapo ready kukusaidia, maana ukisema tu unataka kusoma Travel Agency hatuwezi kukupa jibu wakati hatujui kama una vigezo vya kusoma hiyo course au vipi, ndio maana kuna mdau hapo juu akasema weka umepata Division 4 ya points ngapi??
   
 7. SIR.NOM

  SIR.NOM Member

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Sep 8, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  1 nikutie moyo 1 kwa hyo 4 hujafel km unavodhania,kwn walofeli wana zero.kuwa muwaz una 4 ya ngap,ikbd na masomo uliyoyasomea na GRADE zake itakuwa rahc zaid kukusaidia ukasomee coz gan.nashukuru km umenielewa.
   
 8. w

  wingman7 JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  nimepata ya 28
   
 9. i

  itagata JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Safi! Hiyo sio mbaya Dogo, kwa mtizamo wangu unaweza kusoma vyuo vya afya kama ulipata pass kwenye masomo ya Sayansi, kwa Mfano kama ulipata D kwenye Physics, Biology na Chemistry au Maths itakusaidia sana. Pia unaweza kusoma course zenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii, ambazo huwa hazitegemei sana sehemu moja katika kupata ajira, kwa mfano unaweza kusoma Certificate ya Community Development na baadae ukaingia Diploma, au unaweza kwenda chuo cha St. John na ukasoma Diploma ya Project Planning and Management au ukasoma Diploma ya Laboratory technician, au Diploma ya Agriculture general.

  Hizi kwa mtizamo wangu zinaweza kukusaidia sana kuendelea mbele kwani kuna baadhi ya vyuo bado wanapokea maombi mpaka sasa, hivyo jitahidi uangalie mapema kwani muda unakaribia kwisha. Huu ni ushauri wangu.
   
 10. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mkuu wangu hongera sana kwa kuweza kumsaidia dogo atleast umempa idea nini cha kufanya hata akienda chuo ajue nini cha kuuliza maana umemfungua kidogo, endelea kuwa na moyo wako
   
 11. ankol

  ankol JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 1,185
  Likes Received: 386
  Trophy Points: 180
  Mi sikushauri uanze kuhangaika kusomea masomo kwa level ya Certificate. Ndugu yangu dunia ya leo competition ya ajira ni kubwa mno. kuna watu wana ma degree lakini bado wako nazo mitaani. Badala yake waweza somea ujuzi pale Veta mfano mambo ya Graphic Designing, na vitu kama hivyo ambavyo moja kwa moja vitakuingiza sokoni, kama sio kuajiriwa basi hata kujiajiri. Think twice before making that decision usijekuja jijutia hapo baadae. Ni hayo tu.
   
Loading...