Naombeni msaada wenu tafadhali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni msaada wenu tafadhali

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by quimby_joey, Jan 27, 2011.

 1. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  habari zenu wana JF,

  naomba mawazo yenu ndugu zangu hasa kwa kuamini kuwa hapa ni jukwaa sahihi kwa shida kama hii. kuna jamaa yangu mmoja amekuja kwangu kuniomba ushauri wa kisheria kutokana na tatizo lililoko kwenye familia yao kwasasa.

  Stori yenyewe iko hivi, huyu jamaa wamezaliwa wanne kwa mama yao na kwa baba yao wako saba. baba na mama yao walikutana mwaka 1980 na kuanza kuishi pamoja bila ndoa. wakazaa watoto wanne (3 +ke, 1 +me), wa kwanza alizaliwa 1981, wa pili 1982, na yeye 1985 na wa mwisho 1986. Wakati baba na mama yao wanakutana tayari baba alikuwa ameshazaa watoto 3 nje kila mtoto na mama yake (wote waliishi kwa mama zao). Ilipofika mwaka 1988 wawili hao wakaachana baada ya baba kumfukuza hapo nyumbani, na watoto wote kuchukuliwa na baba. Mama huyu akafariki mwaka 1990. Wakati wanaachana baba huyu alikuwa tayari na mahusiano na mwanamke mwingine ambapo walianza kuishi pamoja mwaka 1989. Mama huyu alikuwa na mtoto mmoja aliyezaa nje, hivyo wakaamua kuishi pamoja na watoto wote (wanne wa baba na mmoja wa mama). Walikuja kufunga ndoa kanisani mwaka 1994, ndoa hii haikubarikiwa mtoto. Huyu mama alifariki mwaka 1997. wakati wa ndoa yao walijenga nyumba moja, moja ya serikali na kununua gari moja.

  Baada ya kufariki kwa huyu mama, baba huyu alianza kuishi na mwanamke mwingine mwaka 1998 ambapo walifunga ndoa mwaka 2000 na kuzaa mtoto mmoja (wakati akiolewa huyu mama alikuwa pia na mtoto aliyezaa nje) Wakati wote wa maisha yake huyu baba amekuwa akiishi na hawa watoto wake wanne. Mwaka 2005 mke aliamua kuondoka na kurudi kwao baada ya kugundua kuwa baba huyu alikuwa na mahusiano na mwanamke mwingine nje (tuhuma za kweli), mtoto waliyezaa alibaki na baba. baada ya kutengana, baba huyu alibaki na watoto wake wanne pamoja na yule aliyezaa na mkewe aliyeondoka.

  Mwaka 2008, baba huyu aliamua kumleta nyumbani yule mwanamke aliyesababisha mkewe kuondoka kurudi kwao, na hadi sasa wanaishi pamoja kama mke na mume. Huyu mama ana watoto watatu aliozaa nje, na amekuja nao hapo nyumbani. Jumla ya familia ni kwamba baba + watoto wake 5 na huyu mama + watoto wake 3 jumla ni familia ya watu 10.

  Kilichompelekea huyu jamaa yangu kutafuta ushauri ni kwamba, huyu mama tayari ameshika ujauzito wa huyu baba na karibu atajifungua, huyu baba anawafukuza watoto wake wanne akisema waondoke pale nyumbani wakatafute maisha yao familia imeshakuwa kubwa, watoto wamegoma wamesema labda yeye mzazi ndo aondoke na huyo mkewe waende wanakokujua, baba katishia kuiuza nyumba ambayo ni ya NHC. Sasa watoto hawa wanne akiwemo huyu jamaa wanataka kujua kama wana haki kwenye hiyo nyumba na mali ya baba yao kwa ujumla, na je waondoke kwenye hiyo nyumba?

  Naomba ushauri wenu wana JF....
   
 2. L

  Leornado JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Dah swala tata kidogo ila logically hiyo nyumba mmiliki ni huyo baba na ana haki ya kuamua nani aishi naye au akifa nani amrithishe. Ila watoto wanaweza enda kuweka pingamizi mahakamani kama dingi atataka kuuza nyumba ya familia na kuacha watoto bararani...
  Watu wa family law na right to property mwageni mamboz...
   
Loading...