Naombeni msaada wenu juu ya mkasa huu ulionikuta mtanzanua mwenzenu

Habari zenu wakuu!!! mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 25.
Kuna kampuni ya printers nilikua nafanya kazi nikiwa kama msaidizi wa kiongozi mkuu. Hapo ofisini pakatokea wizi wa kuibiwa pesa usiku wa saa10.
Basi hiyo kesi ikanidondokea mimi. Nikawekwa lock up na baadae mahakamani, nilipokua naenda mahakamani walionishitaki hawakuwa wakija hapo mahakamani.
siku tatu zote hawakutokea basi hakimu akanambia case imekufa kuanzia siku hiyo nipo huru.

Hii case imechukua miezi miwili na nusu hadi kuisha kwake.

Kwenu wana JF nilikua naombeni msaada wenu juu ya swala la madai kwa upande wangu linaweza kuleta tija maana wamenidhalilisha sana kwa kitendo cha kuwekwa lock up nikiwa na mtoto mchanga wa miezi miwili ninae mlea mm kama baba ake.
Je naweza kufungua madai? na kama nikifungua madai haitoweza kuni cost kwa jambo lolote?

Kwenu wana JF, naombeni msaada wenu plz.
Maadam uko huru achana na ishue za kufungua kesi... Matatizo ni sehemu ya maisha. Sasa pambana upate shughuli nyingine ya kukuingizia kipato. Yaliyopita si ndwele, ganga yajayo...
 
Back
Top Bottom