Riwa
Platinum Member
- Oct 11, 2007
- 2,607
- 3,083
Smile kisheria talaka haitolewi kwa kuomba tu "nipe talaka yangu" kama ilivyo kwa baadhi ya desturi. Inabidi huyo dada aanze divorce proceedings kwa kuchukua hatua za mwanzo kabisa za baraza la upatanishi wa ndoa (Marriage Conciliation Board). Huko mwanaume ataitwa na wanabaraza watawapatanisha, kwa vile mume anasema bado anampenda mkewe watatakiwa kurudiana.
Hapo kwenye baraza la wapatanishi ndio penye tatizo...hivi kweli watu mmetengana miaka miaka miwili, no feelings anymore, pengine mnachukiana...kuna upatanishi hapo!? Na kama hatutaki kupatana, tunataka kuachana kila mmoja ashike hamsini zake bado hao wanabaraza watapoteza time yao kuwapatanisha...ooops, they are paid to waste their time au siyo!
Kwa nini mwanamke anayenyanyasika hasiweze pata talaka na stahiki zake akaishia zake huko kuendelea na maisha yake!