Naombeni msaada wa ushauri nasaha

Naombeni msaada wa ushauri nasaha

Kwanza naomba mod usitoe uzi huu hapa
kuna dada alikuwa ameolewa amekaa na mume wake 12 years ndoa ya kikristo
hawakuwa na mtoto
mwaka 2010 mwanaume alimshutumu wife kutokuwa mwaminifu akamfukuza bila hata nguo,na kagoma kumrudisha hadi leo
walikuwa na vitu vingi nyumba maduka magari
mwanaume hataki kutoa talaka maybe anaona watagawana vitu ilasijui
sasa huyu dada anaomba ushauri afanyeje apate haki yake? ,maana nanateseka
mwanaume akiulizwa vipi anadai hana shida na mkewe bado anampenda ila sio kweli,hawaongei wala hajawai kumpa hata mia toka iyo jan 2010. Na huyo mwanaume hajaoa tena
Aende ustawi wa Jamii,hili sio swala la kisheria take into consideration that a woman still loves the man,watawasuluhisha and things might get better to the way it was before.Hawa jamaa wanasaidia sana ingawa to be honest ni vi-ofisi vya serikali vilivyochoka sana mpaka unaweza ukakata tamaa.
 
umeshamshauri vema sana hatua za awali
yaelekea umekula shule ya prof kabudi family law vizuri.[
Smile ushauri huu umekamilika.
wakisha file petition mahakamani wakili ana kazi ya kuthibitisha ndoa hiyo haiwezekaniki tena
(broken down irreperabily) awe na supporting evidences,
mahakama lazima itatoa talaka, mgawanyo wa mali na maintance kipindi chote alichomtimua mke wake.

UOTE=mwaJ;5673466].
[/QUOTE]shukrani mkuu lokisa
 
Aende ustawi wa Jamii,hili sio swala la kisheria take into consideration that a woman still loves the man,watawasuluhisha and things might get better to the way it was before.Hawa jamaa wanasaidia sana ingawa to be honest ni vi-ofisi vya serikali vilivyochoka sana mpaka unaweza ukakata tamaa.
mambo ya upendo temana nayo
 
Duh! Wamekaa kama mme na mke katika kipindi cha muongo mmoja na miaka miwili! Na hawajabahatika kupata mtoto! Na ukizingatia ni ndoa ya Kikrsto! Na katika maneno ya mwisho kabisa mbele ya kadamnasi yote ya kanisa waliambia hivi Ndoa iliyofungwa na MUNGU mwanadamu asitenganishe! ama kweli hapa sasa ni wale magwigi wa sheria ndiyo tunawahitaji hapa tumnusuru huyu rafiki yake Ndugu yetu Smile;

Copy;

PakaJimmy;
Mr Rocky;
Rutashubanyuma;
Mtumishi Wetu;
Dark City


Hawa member tajwa wanaweza wakampatia mwanga Ndg yetu Smile;
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Lokissa sorry sana mkuu nishaipanga maana na mimi niliona imekaa vibaya sana
 
Last edited by a moderator:
Duh! Wamekaa kama mme na mke katika kipindi cha muongo mmoja na miaka miwili! Na hawajabahatika kupata mtoto! Na ukizingatia ni ndoa ya Kikrsto! Na katika maneno ya mwisho kabisa mbele ya kadamnasi yote ya kanisa waliambia hivi Ndoa iliyofungwa na MUNGU mwanadamu asitenganishe! ama kweli hapa sasa ni wale magwigi wa sheria ndiyo tunawahitaji hapa tumnusuru huyu rafiki yake Ndugu yetu Smile;

Copy;

PakaJimmy;
Mr Rocky;
Rutashubanyuma;
Mtumishi Wetu;
Dark City


Hawa member tajwa wanaweza wakampatia mwanga Ndg yetu Smile;
huyu jamaa ana hela sana hataki mgawanyo,ila kurudiana nayo haiwezekaniki tena, na mali wamechuma wote kwa kweli
 
2. KUKATAA KWA MAKUSUDI KUITIMILIZA NDOA:
Kama baada ya kufunga ndoa mmoja wa wafunga ndoa atakataa kuitimiliza ndoa anayekataliwa ana haki ya kuiomba mahakama kuvunja ndoa hiyo. Maingiliano yanayotambulika kisheria ni yale yanayofanyika siku ya ndoa na kuendelea na siyo kabla ya ndoa. Kukataa kuitimiliza ndoa kunakuwa sababu ya kubatilisha ndoa ikiwa mwenye kukataa hana sababu yoyote ya msingi na mwenye kukataliwa ametumia kila mbinu kumshawishi aliyekataa lakini ikashindikana kufanya tendo la ndoa.

SABABU YA KUTOA TALAKA MAHAKAMANI
Kabla ya kupeleka shauri au maombi mahakamani ya talaka, mwanandoa husika hana budi kufuata au kuzingatia hatua zifuatazo;
a) kufungua au kupeleka malalamiko kwenye
Baraza la Usuluhishi la Ndoa kwa mfano
Bakwata, kanisani,Utawi wa Jamii au
Baraza la Kata.
b) Baraza litasikiliza, na endapo litashindwa
mapatano au muafaka kati ya wanandoa hao,
21
basi baraza litatoa cheti ambacho kitaeleza kuwa limeshindwa kusuluhisha mgogoro wa ndoa na kuomba
mahakama kuendelea kutoa talaka.
c) Baada ya mwanadoa mmoja kupata cheti hicho basi atatakiwa atayarishe madai ya talaka akionyesha kuwa kulikuwa na ;-
ndoa halali,
kuna mgogoro kati yao,
watoto,
mali walizochuma wakati wa ndoa yao,.
Muombaji huyo ataiomba mahakama hiyo itoe amri ya
talaka,
mgawanyo wa mali zilizochumwa kwa nguvu za pamoja,mamlaka ya kukaa na watoto na matunzo yao,
gharama za madai / shauri.
Ili mahakama itoe talaka sababu kadha huangaliwa na mahakama. Sababu hizo ni mambo ambayo yatakayofanya ndoa ionekane kuwa imevunjika kiasi kwamba haiwezi kurekebishika tena, mambo hayo ni kama ifuatavyo;
a) Ugoni; hii ni zinaa ambayo hufanywa na mwanaume na mwanamke ambao hawajaoana.
Hii hutokea ambapo mwanaume ana mke wake au mwanamke ana mume wake, hivyo mmoja wapo anamwacha mke/mume na kufanya zinaa na mtu mwingine.
b) Ukatili; ukatili ni kuumiza nafsi nyingine, kuharibu mwili au kuwa na hofu ya kuumizwa.
c) Kulawiti; kulawiti ni kumwingilia mtu kinyume na maumbile,
d) Kichaa; ni kutokuwa na akili timamu, na hali hii lazima iwe imethibitishwa na madaktari bingwa wa akili.
e) Kuzembea wajibu kwa makusudi; haya ni majukumu ya mume, majukumu hayo ni kama haya; kumtunza mke kwa kumpa chakula, malazi na mavazi.
f) Uasi Ni hali ya mke au mume kuhama nyumba ya ndoa na kwenda kuishi mahala pengine bila sababu yoyote ya msingi,
g) Kutengana; kukaa mbalimbali kwa mume na mke kwa muda wa miaka isiyo pungua mitatu, kutengana kwao ni sababu tosha ya talaka.

HAKI NA WAJIBU KATIKA NDOA
Baada ya kufunga ndoa na ikaonekana haina kasoro yoyote, mke ana haki mbalimbali kisheria anazostahili kuzipata kisheria. Haki hizi ni kama;
- Matunzo; mke au wake wana haki ya kutunzwa na mume wao kwa kuwapatia mahitaji muhimu kama chakula, malazi, mavazi, matibabu, n.k kulingana na uwezo alionao mume.
- Kumiliki mali; mke ana haki ya kumiliki mali aliyoipata kabla na baada ya ndoa kama aliipata kwa
24
fedha yake mwenyewe. Mke ana haki ya kuingia mikataba, kushitaki na kushitakiwa. Makubaliano yaweza kufanywa na wanandoa hiyo jinsi ya kumiliki mali iliyopatikana kabla ya ndoa yao jinsi gani waimiliki. Kwa mali iliyopatikana wakati wa ndoa, mali hiyo ni mali ya wanandoa wote, kwa sababu imepatikana kwa mchango wa nguvu za pamoja. Hii haijalishi kuwa mmoja wa wanandoa (mke) hachangii pesa tasilimu au anakaa nyumbani na kufanya shughuli za nyumbani tu. Kufanya shughuli za nyumbani ni mchango mkubwa na ameokoa fedha nyingi. Umiliki wa mali kwa wanandoa haujalishi kuwa mmoja wapo amemiliki mali hiyo kwa jina lake au la. Sheria ya Ardhi inatamka wazi kuwa kama mwanandoa mmoja anamiliki mali kwa jina lake, na mwanandoa mwingine akachangia nguvu zake katika kuendeleza, kuboresha au kuzalisha mali hiyo basi anapata haki ya kumiliki mali hiyo.
- Haki ya kukopa kwa dhamana ya mume; jukumu la kutunza mke na watoto ni jukumu la mume au baba. Kwa msingi huo, endapo baba amesafiri, au ametoroka na baadaye matatizo yakajitokeza yanayohitaji fedha, basi mke ana haki ya kukopa fedha kwa jina la mume au kuweka rehani mali ya
25
mumewe.
- Haki ya kuishi katika nyumba ya Ndoa;
Nyumba ya ndoa ni nyumba ambayo mke na mume wanaishi wakati wa ndoa. Hata kama wanandoa wana nyumba nyingi, basi wanayoishi au kutumia kama makazi ndiyo nyumba ya wanandoa. Nyumba hii haiwezi kuuzwa, kuweka rehani au kuchukuliwa na mtu mwingine kama zawadi bila ya makubaliano ya wanandoa wote.(bila ridhaa ya wanandoa). Mwanandoa ana haki ya kuishi kwenye nyumba hiyo mpaka amri ya mahakama ya kuvunja ndoa, au kutengana itakapotolewa.

Hapa nimejaribu kuchukua baadhi ya vifungu kwenye sheria ya ndoa ya mwaka 1971, na vingi nilivyochukua ni vile vinavyoweza kumsaidia huyu mdada
 
Je ni kweli alifumaniwa au hapana? Kama alifumaniwa sijui wanasheria watasemaje ila kidini kama mkristo ndoa inavunjika on the sport, though sijui kama kuna kugawana mali mliyochuma pamoja. Ila sheria ndio yenye haki ila ajiandae kukumbana na misukosuko kwani kama mme ana uwezo ni wazi haki kibao zitapindishwa na mapene.
 
sasa kama bwanake kaachana naye miaka 3 iliyopita unategemea nini? Hata huyo baba ni binadam sio malaika anaweza kushawishika>
 
je ni kweli alifumaniwa au hapana? Kama alifumaniwa sijui wanasheria watasemaje ila kidini kama mkristo ndoa inavunjika on the sport, though sijui kama kuna kugawana mali mliyochuma pamoja. Ila sheria ndio yenye haki ila ajiandae kukumbana na misukosuko kwani kama mme ana uwezo ni wazi haki kibao zitapindishwa na mapene.
wala hakumfumania ni fununu tu kwamba anachipuka nje
 
Shukrani sana kwa ushauri wenu ngoja nimprintie jamani
nitaleta feedback
 
wala hakumfumania ni fununu tu kwamba anachipuka nje

Kidini haina mshiko kwani ili ndoa ife lazima umfumanie akiwa tendoni tena na mashahidi au shahidi. Afuate hatua za kisheria kwani pamoja na kuwa nipo kabila la mmewe ila kwa baadhi yao swala la ukandamizaji wa wanawake hasa la kipato na kama hakuhusika moja kwa moja kuzalisha ni jadi yao. Yaani wapo tayari kuuza mali zote kuendesha kesi na sio kukubali defeat. Ikishindikana kabisa wanarudi ktk ndoa kuliko kugawa mali. Hope unawajua vizuri
 
Kama unataka ushauri wa kisheria ipeleke Jukwaa la sheria.
 
kidini haina mshiko kwani ili ndoa ife lazima umfumanie akiwa tendoni tena na mashahidi au shahidi. Afuate hatua za kisheria kwani pamoja na kuwa nipo kabila la mmewe ila kwa baadhi yao swala la ukandamizaji wa wanawake hasa la kipato na kama hakuhusika moja kwa moja kuzalisha ni jadi yao. Yaani wapo tayari kuuza mali zote kuendesha kesi na sio kukubali defeat. Ikishindikana kabisa wanarudi ktk ndoa kuliko kugawa mali. Hope unawajua vizuri
acha tu wanadhani watazikwa na mali
 
59764_10200563042147350_379695010_n.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom