Wapendwa wana JF nawasalimu wote, natumai mu wazima.
Kuna jambo lanitatiza nahitaji msaada wa mawazo, yawezekana kabisa muamuzi wa mwisho ni mimi mwenyewe ila nikipata mawazo tofauti itasaidia pia.
Nina mchumba wangu ambae tunatarajia kufunga ndoa hivi karibuni. Wiki iJuzi Jumanne niliibiwa simu so yeye akanipa simu yake nitumie.
Hamadi kwenye simu nikakuta texts kwenye inbox ambayo kutokana na flow ya zile texts alikuwa akichat na mwanamke, na ikaonyesha kabisa yule mwanamke waliwahi kuwa na mahusiano na kudo pia, ha hiyo imetokea akiwa na mimi, mana yule dada aliandika kabisa kuwa "bahati ulikuwa nayo wewe tu ya kukupa ....), na nyingine lukuki za kuonyesha mdada ana wivu kuwa amesikia jamaa ana mtu mwingine yani apart from me, na huyo dada anaonyesha kunifahamu mana kuna msg baada ya jamaa kumwambia kuwa hao anaowasema si watu zake hata mchumba wangu (yani mimi) anawajua, mdada akahamaki na kutaja jina langu..
Nilijaribu kuongea na huyo mume mtarajiwa lakini alikana katukatu hajawahi kuwa na uhusiano na mtu huyo ni jokes tu, kama nataka nijaribu kuchukua simu yake nione jinsi gani wanawake wanamchatisha mambo makubwa kuliko hayo. mimi sikubuy story yake kwa kweli hapa kichwa kinaniuma kwa mawazo. Na cha kushangaza yeye kutwa akiongea na simu ni kuita wanawake baby sasa hata akiniita mimi sioni kama kuna uniquness yoyote.
Naombeni msaada wa mawazo tafadhali, nina mawili nimuache au nibaki, na mahali keshatoa. nikimuacha je nitakayempata atakuwa na afadhali au atakuwa worse.nina maswali mwngi kichwani kuliko majibu.
Natanguliza shukrani.
Sweetdada
Watu wepesi kweli kushauri umuache,sio mwaminifu....hao waaminifu wako wangapi na probability ya kumpata aliye mwaminifu 100% ni kiasi gani?? Nakushauri, usikilize moyo wako na akili yako, wewe unamjua vizuri,binafsi nachukia cheating,ila ninavyozidi kukua naona kama uwezekano wa kumpata ambaye atakuwa mwaminifu kwangu kwa asilimia 100% ni mdogo, nasikiliza moyo wangu na akili yangu juu ya mwanaume. Kama nimempenda naye kanipenda,ananiheshimu na walio wangu,ananitunza na kunisaidia kuwa bora zaidi,nina furaha.....etc....natulizana hapo hapo....hadi ni-prove ni cheater wa kupitiliza hadi anashindwa majukumu yake ndo nitamuacha,sina muda wa kubadili wanaume kila kukicha,ni wale wale tu.....!
Huu ni aina ya ushauri tunautegemea kutoka kwa dada mkuu!!
Wakati mie niko mdogo, dada yangu alikuwa akija kushitaki nyumbani kila anapokuwa na ugomvi mkubwa na mume wake....Ilikuwa inaniudhi sana hadi namshauri aachane naye!! Leo siwezi kusema kitu kama hicho!
Babu DC!!
Asante Babu DC, mimi ni uzoefu wangu tu mdogo, wengi wa waliokimbia wapenzi wao kwa kosa moja au mawili ya cheating,wamejikuta wakiwa dissapointed zaidi na zaidi na kurudi nyuma inakuwa ngumu. Nimeshuhudia watu wanakuwa na wanaume zaidi ya ishirini na bado wanatafuta that perfect man that doesn't cheat...! Its not realistic and there will never be a guarantee that the next man won't cheat...ukimuacha uliye naye...usiwe na mtu tena,hapo hutakuwa na expectation na hutakuwa dissapointed.
Don't Cry for Someone who Can't Cry for You!!:focus:nilikuwa na mpenzi wangu nilimpenda kwa moyo wangu wooote,nilimuamini saana nilikuwa muaminifu 100% enzi zake izo.yaani kila kitu changu kilikuwa chake.simu yangu nilikuwa naweza kumpa au hata kama nimeisahau kwake naiacha hadi aniletee sio sasa nikisahau mahali nipo radhi kukodi hata ndege niifate maana atazimia kama si kufa. ila simu yake ilikuwa ni marufuku kabisa kuishika kwa sababu ya ujinga na upofu wa mapenzi sikuona ni tatizo.one day hamada nikaipata iyo simu kama ya kwakoooo sms kibao nikapuuzia nikaja kumwagwa shosti lonely lonely nimebakia maweeeeeeeeee
mmh mbona unanitish!!
Mara nyingi walengwa hutuma messages ambazo mpokeaji kwa wakati huo angependa asikie....
mwe shosti pole, kumbe na wewe yalikukuta!!
simu hizi zina mambo, angefuta msg zake kabla hajanipa simu leo nisingekuwa najua mauzauza yake, ila pia nashukuru kuwa nimejua..sasa nipo njia panda looh sijui naanzaje kufanya nini[/QUOT
mtenda kosa mara ya kwanza simkosaji, kosa ni kurudia...so mkalishe chini hubby wako 2b mzungumze siriazly na umfungukie how u feel abt that ishu blah blah...utanote tu if waweza msamehe mkaendeleza mapenzi. usikimbilie kumwacha