Naombeni Msaada wa mawazo tafadhali

sweetdada

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
517
169
Wapendwa wana JF nawasalimu wote, natumai mu wazima.

Kuna jambo lanitatiza nahitaji msaada wa mawazo, yawezekana kabisa muamuzi wa mwisho ni mimi mwenyewe ila nikipata mawazo tofauti itasaidia pia.

Nina mchumba wangu ambae tunatarajia kufunga ndoa hivi karibuni. Wiki iJuzi Jumanne niliibiwa simu so yeye akanipa simu yake nitumie.
Hamadi kwenye simu nikakuta texts kwenye inbox ambayo kutokana na flow ya zile texts alikuwa akichat na mwanamke, na ikaonyesha kabisa yule mwanamke waliwahi kuwa na mahusiano na kudo pia, ha hiyo imetokea akiwa na mimi, mana yule dada aliandika kabisa kuwa "bahati ulikuwa nayo wewe tu ya kukupa ....), na nyingine lukuki za kuonyesha mdada ana wivu kuwa amesikia jamaa ana mtu mwingine yani apart from me, na huyo dada anaonyesha kunifahamu mana kuna msg baada ya jamaa kumwambia kuwa hao anaowasema si watu zake hata mchumba wangu (yani mimi) anawajua, mdada akahamaki na kutaja jina langu..

Nilijaribu kuongea na huyo mume mtarajiwa lakini alikana katukatu hajawahi kuwa na uhusiano na mtu huyo ni jokes tu, kama nataka nijaribu kuchukua simu yake nione jinsi gani wanawake wanamchatisha mambo makubwa kuliko hayo. mimi sikubuy story yake kwa kweli hapa kichwa kinaniuma kwa mawazo. Na cha kushangaza yeye kutwa akiongea na simu ni kuita wanawake baby sasa hata akiniita mimi sioni kama kuna uniquness yoyote.

Naombeni msaada wa mawazo tafadhali, nina mawili nimuache au nibaki, na mahali keshatoa. nikimuacha je nitakayempata atakuwa na afadhali au atakuwa worse.nina maswali mwngi kichwani kuliko majibu.

Natanguliza shukrani.

Sweetdada
 
Dada sikushauri kuendelea na mpango wa ndoa huku ukiwa umemtilia mashaka mueleze kuwa haumuamini kwa sababu ya tabia zake hizo na umeamua kusitisha suala la ndoa. niamini nakuambia ni kosa kubwa kuingia kwenye ndoa wakati umeshaona red light utakuja kujuta, nilishafanya hilo kosa kilichonitokea nakijua mwenyewe. Na kwa nini hauamini kuwa wanaume waaminifu wapo?? nakuhakikishia wapo ila inatokana na wewe mwenyewe utakavyokuwa na msimamo na ndivyo wao wanakuwa na msimamo.
 
duh!!! kwnza pole sana na yaloyokukuta dada.
sasa unajua dada yangu ukweli ni kwamba hapa dunianai ni wanaume wachache sana ambao watakuwa na wewe tuu pekee yako. pili huyo jamaa amaeonyesha kutojali hisia zako kabisa maana kama kweli angekuwa anakujali mambo ya kuita wanawake wengi baby sio kitu chakusema kwa majigambo.
with regards to ur options....ukiolewa nae wewe jua ya kwamba huyu ataendelea na tabia hii hivyo mentaly just prepare urself for that. ningekushauri kuwa ukiondoka hapo ujue huko uendapo pia utakutana na haya mambo maana wanaume wengi wetu ndio mambo yetu....sasa chakujiuliza upo tayari kuwa unabadilisha wanaume kila ambapo utakuta jamaa ana kimada nje? mwisho wa siku utakuwa nao wangapi?
ukiachana nae basi ujue ya kwamba unakubali kuwa single for the rest of ur life ama uwe na mshikaji wakukupa raha pale unapohitaji. tafakari haya alafu utachagua lipi lakufanya
 
Sweetdada,

Ndio unaelekea kwenye ndoa , ndoa ni uvumilivu vumilia tu ni kipindi kinapita.
 
point of no return - mpaka kufikia hatua ya huyo jamaa yako kukutolea mahari inaonyesha kwamba ameamua kukuchagua wewe kutoka katika hitlist yake; so jitose tu hivyo hivyo mkapambane hukohuko ndani kwa ndani - afterall utamu wa ngoma ni kuingia na kuicheza...
 
Don't Cry for Someone who Can't Cry for You!!:focus:nilikuwa na mpenzi wangu nilimpenda kwa moyo wangu wooote,nilimuamini saana nilikuwa muaminifu 100% enzi zake izo.yaani kila kitu changu kilikuwa chake.simu yangu nilikuwa naweza kumpa au hata kama nimeisahau kwake naiacha hadi aniletee sio sasa nikisahau mahali nipo radhi kukodi hata ndege niifate maana atazimia kama si kufa. ila simu yake ilikuwa ni marufuku kabisa kuishika kwa sababu ya ujinga na upofu wa mapenzi sikuona ni tatizo.one day hamada nikaipata iyo simu kama ya kwakoooo sms kibao nikapuuzia nikaja kumwagwa shosti lonely lonely nimebakia maweeeeeeeeee
 
mwe shosti pole, kumbe na wewe yalikukuta!!

simu hizi zina mambo, angefuta msg zake kabla hajanipa simu leo nisingekuwa najua mauzauza yake, ila pia nashukuru kuwa nimejua..sasa nipo njia panda looh sijui naanzaje kufanya nini
 
duh!!! kwnza pole sana na yaloyokukuta dada.
sasa unajua dada yangu ukweli ni kwamba hapa dunianai ni wanaume wachache sana ambao watakuwa na wewe tuu pekee yako. pili huyo jamaa amaeonyesha kutojali hisia zako kabisa maana kama kweli angekuwa anakujali mambo ya kuita wanawake wengi baby sio kitu chakusema kwa majigambo.
with regards to ur options....ukiolewa nae wewe jua ya kwamba huyu ataendelea na tabia hii hivyo mentaly just prepare urself for that. ningekushauri kuwa ukiondoka hapo ujue huko uendapo pia utakutana na haya mambo maana wanaume wengi wetu ndio mambo yetu....sasa chakujiuliza upo tayari kuwa unabadilisha wanaume kila ambapo utakuta jamaa ana kimada nje? mwisho wa siku utakuwa nao wangapi?
ukiachana nae basi ujue ya kwamba unakubali kuwa single for the rest of ur life ama uwe na mshikaji wakukupa raha pale unapohitaji. tafakari haya alafu utachagua lipi lakufanya

mmh mbona unanitish!!
 
Hapo hamna cha kushaur maana umeshajua alivyo. Kilichobaki ni wewe kuamua kama utapenda/weza kumvumilia muendelee na kama hutoweza muachane.
 
msg tu sidhani kama kuna shida sana
wapo wanawake wanapenda sana jokes hata mm
huwa nataniwa sana na kina dada kwa smg kama hizo oooh ilikuwa tamu,unajua sana nk
lkn sijawahi kudo nao,nahisi mchumba wako ni mpenda jokes sana na kwa mtu ambae ni mwizi lazima msg kama hizo afute
asingekupa simu yake kama anajua yeye ni mkosaji
ni wangapi wanafanya mambo makubwa lkn ukiwaona machoni utadhani malaika???
wangapi wanachati pamoja wakiitana kaka na dada ili mtu mwingine asijue kumbe wanafanya ufuska mkubwa?
we dada una bahati mahari ushalipiwa na umependwa endelea na mipango ya ndoa
utakayo yakuta ktk ndoa ni ww mwenyewe kuvumilia na kumbadili mwenzio wa ndoa
naamini shetani hupenda kuwatia watu hofu na mashaka ili kutibua mipango yao
mkiachana atabaki anawacheka,,kuwa makini usije ukabaki mtaani daima.its up to u
 
kila kitu hutokea kwa sababu yake mungu amefanya kila kitu kwa kusudi lake usingepoteza simu usingeyajua hayaaa yote? kama unampenda samehe na kusahau kabisa .mpe nafasi nyingine sababu hakuna alliye mkamilifu hata siku moja .usifanye maamuzi kwa pupa mpe mungu nafasi afanye lilo sahihi kwake.pole na ndo ukubwa
 
pole ndo ukubwa,wenzio tushapambana na mazito kuliko hayo.kikubwa give uaself enough time to think before u choose what is best for u.
 
Duh, najitahidi kutumia hekima zangu zote sababu ni sweetlady.
Umeshuhudia kila kitu bila chenga, sasa maamuzi ni yako.
 
Pole sweetdada

Kama unapenda kucheki simu ya mpenzi wako, in fact umeshakuwa na tabia hiyo, basi mkiendelea na uhusiano na mkafunga ndoa atakuwa makini sana kwa kuhakikisha hapigiwi simu wala hawamtumii sms awapo na wewe ili asikuumize lakini ataendelea na tabia hiyo awapo mbali na wewe afetr all wanaume nowdays wanaona ni kama fashio kuwa na wanawake zaidi ya mmoja.

Sweetdada tafakari na uchukue hatua, ila mh, ndoa ni taaaaaaaaamu panapokuwa na uaminifu na mapenzi ya kweli na sio maigizo.
 
Walimweusi, Asante. ila naona hukunisoma vizuri.
mimi sikuchokonoa simu yake, ni kwamba niliibiwa simu yeye akaamua kunipa ya kwake extra
lakini kwa bahari mbaya au nzuri alisahau kufuta msg kwenye hiyo simu aliyonipa,mimi nikaziona,na si mimi kwenda kupekenyua simu yake, huwa sifanyi hivyo kwa kuwa naamini mwanaume hachungwi bali anajichunga mwenyewe.
 
pole sna dadang ila nakshaur uyo c mwaminif cha kufanya km umeamua kumwacha achana nae coz anaeza kukuletea maradhi kwa huruma yako kwmb ni bahat mby.
 
Back
Top Bottom