NAOMBENI MSAADA WA KISHERIA

flank

Member
Jan 14, 2017
89
125
Habari za saa hizi wanajamvi!
Mwishoni mwa mwaka jana (2016) tulisainiana mkataba na bodaboda ambapo nilimkabidhi pikipiki ili arejeshe kiwango cha hela kwa kila wiki. Hazikupita wiki tano jamaa akawa harejeshi hela kama tulivyokubaliana na wala hakunipa taarifa yoyote. Nilipokuwa napiga simu yake ya kiganjani ikawa haipokelewi. Nilihamua kumfuata nyumbani kwake na bahati nzuri nilimkuta akanieleza kuwa amepata ajali na pikipiki iko kwa fundi, kila nilipomuomba anipeleke ili nijiridhishe kuwa ni kweli pikipiki imeharibika alifanya kila jitihada kunikwepa. Sikuona sababu ya kuendelea kuumiza kuchwa changu ndipo nilihamua kumfungulia kesi ya jinai kwa kujimilikisha mali kwa njia za udanganyifu.
Hiyo kesi nikawa nimeshinda akahukumiwa kifungo cha nje miezi sita na kunilipa sh. milioni mbili abayo ni gharama ya pikipiki, ila alitakiwa kurejesha hela hiyo mara baada ya miezi mitatu ya awali akiwa anatumikia kifungo hicho. Cha ajabu huu ni mwezi wa tano tangu hukumu hiyo itolewe jamaa hajarejesha chochote, jana nilienda mahakamani kujua nifanyeje zaidi na bahati mbaya hakimu sikumkuta nikaonana na karani wake akanieleza kuwa inabidi niandike barua ya KUKAZIA HUKUMU kwa ajili ya utendaji zaidi.
Kiukweli hii barua ya kukazia hukumu imekuwa mtihani kwangu kwani nijuavyo mimi ni kuwa, barua ya kukazia hukumu inahusika kwenye kesi za madai ila sina uhakika kama inahusika kwenye kesi za jinai au la. Sasa naombeni msaada, ni kweli inabidi niandike barua ya kukazia hukumu? au nikiiandika itanipelekea kukosa haki yangu maana naogopa kuandika barua hiyo nikajikuta kesi inakuwa ya madai. Na je, kama sitakiwi kuandika barua hiyo nifanyeje ili nipate haki yangu?
Nina imani humu kuna wataalam wengi Wa sheria hivyo mtanisaidia. Kumbuka sijasomea sheria kama nimekosea nikosoeni.
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,744
2,000
Mimi sio mtaalamu wa sheria lakini nashauri ufuate maelekezo yao, ingekuwa kesi ya makinikia ningekushauri vizuri
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom