Nadhani vyuo tulivyosoma viko tofauti na material wanayofundisha yanatofautiana na inawezekana hata kazini tukatofautiana kwa sababu tulivyofundishwa kwenye IT ni tofauti.
Wewe ni IT,unadesign network,naamini hata subnet mask kuipata utafanya logic "ANDing" mambo ya logic,samahani siongelei default subnet mask mlizozizoea bila kujua zilipatikana je(255.255.255.0).1+1 siyo 2,ni 0 na unaenda na 1 kichwani(mambo ya primary).Sasa mtu kama hesabu ni tatizo leo umwambie 1+1 siyo 2 wakati yeye hiyo ndiyo hesabu nyepesi kwake.Ukipewa Ip addreeses kujua kama ziko kwenye network moja unahitaji kufanya some logic ANDing,hapo watanielewi wanaojua "subnetting na supersubnetting".Kama ninachozungumza ni level za juu mseme niache kupoteza muda wangu.Huo ni mfano mdogo tu upande wa Network,au ndiyo mambo ya "paper ilikuwa nyepesi,majibu yakija "round about".
Tukija programming,kama hujui hesabu na unatengeneza program inayotambua kwamba a certain number is divisible by 5,mimi ninayejua maths nafahamu kwamba number itagawanyika kwa tano ikiwe "last digit ni 5 au zero" so programme yangu itakuwa inaangalia 'last digit ya input data".Kwa mfano 20 inagawanyika kwa 5 kwa sababu last digit ni zero,75 inagawanyika kwa tano kwa sababu last digit ni 5.
Namba itagawanyika kwa tatu ikiwaje?namba itagawanyika kwa tatu ikiwa jumla ya namba zinazoitengeza jibu lake litagawanyika kwa tatu,mfano 21 inagawanika kwa tau (2+1=3),81 inagawanyika kwa tatu(8+1=9),249 inagawanyika kwa tatu(2+4+9=15).Sasa ukiwa kilaza wa Maths utaweza kuandika hiyo program?Tuwe makini tusije tukaonekana watu wa IT wote,tiatia maji.
Computer inatumia binary numbers,herufi zote na alama za kwenye computer zina code,sasa ukiambiwa uandike program ya kubadilisha small leters to capital letter utatumia geography?
Namba shufa zote zina pattern fulani ukiziandika kama binary,.....
IT umepewa kazi utengeneze system kwa ajiri ya shule fulani,ichukue matokeo yao,itoe matokeo yao nani wa kwanza na wa mwisho wastani wao,wanafunzi wangapi wamefail,passmark iwe ipi ili waliofaulu wawe 126 tu?.Je unaweza kufanya hii project kama statistics hujui?formula za average?standard deviation?
Kwa kifupi hesabu inahusika kuimprove reasoning capacity ya mtu hasa kwenye haya masomo ya technology.
Si lazima wote tuone kitu kimoja, it depends unaangalia from which angle.
Mwana IT una flash ya 1Gb ukiulizwa ni sawa na Mb,Byte au bits ngapi,unatokwa na macho.Siyo lazima wote tusome IT,tunaweza kuwa hata waigizaji kuna fan nyingi tu.
Samani najua hesabu wengi ni tatizo la kitaifa,inawezekana nimetonyesha vidonda.Please I apologyze
NB:"I respect the fact that we differ and every one is unique in his or her own way".If two people agree in everything one of them is not thinking.