Naombeni msaada kwa wafugaji wa Kuku wa kienyeji..

Esmile98

Member
Jun 27, 2016
7
0
Mimi ni mfugaji mdogo kitu kinacho niumiza ni aina gani ya chakula natakiwa niwapatie vifaranga.
*naitaji kufahamu magonjwa ya Kuku na dawa ambazo natakiwa niwapatie vifaranga
*vifaranga vinakuwa kama vimevaa koti den vinakufa he huu ni UGONJWA GANI.?
*napia napenda kujua kama vifaranga nikiviwekea bulb BULB inatakiwa ikae umbali gani.?
MSAADA WENU NI MUHIMU SANA KWANGU..
 
Wape vifaranga starter yaani chakula special kinachouzwa kwenye maduka ya mifugo,chakula hicho kina virutubisho vyote.
Magonjwa ya kuku yapo mengi,ila kwa vifaranga husumbuliwa na mafua,homa ya matumbo (typhoed),ukosefu wa vitamin.Pia kuna gumbolo,ndui na kideli.
Kuvaa koti kwa kifaranga ni dalili za ugonjwa mmoja wapi kati ya hayo niliyokuainishia.Kugundua kifaranga mwenye koti ni vizuri ukawa na daktari kwa ajili ya ushauri.
Umbali wa bulb na vifaranga,hutegemea umri wa kifaranga na uwezo wa mwanga wa bulb yenyewe.Inashauriwa kuweka bulb yenye mwanga mkali usiopungua watts 100 kwa vifaranga vya kuanzia siku moja hadi siku saba na umbali ni nusu meter yaani Cm 50,hii nikufanya joto liwafikie vizuri vifaranga.Nina mengi,ila naomba niishie hapa na wengine wajazie pia humu ndani kuna thread nyingi za ufugaji kuku wa kienyeji ukitafuta utazikuta.
 
Back
Top Bottom