Thesnooperman
Member
- Jul 3, 2013
- 57
- 6
Mimi ni kijana wa kiume nina miaka 22,ninaishi dar es salaam.Ukweli nimemaliza form 6 mwaka jana na kufaulu vizuri tu na kuwa na vigezo vya kujiunga na chuo kikuu,lakini nimeshindwa kwasababu sikuwa na pesa za kutosha kuweza kulipia ada iliyokuwa imebakia hapo shuleni na ikapelekea mpaka sasa sijachukua vyeti vyangu vya form6.Hii imekuja baada ya mama ya mama yangu kufariki mwaka 2011 na ndo pekee niliyekuwa namtegemea kwa kila kitu.Sasa tokea amefariki nimekuwa ktk hali ngumu sana.Sasa wanajf naombeni msaada wa kunisaidia kupata kazi ambayo itakuwa ina masilahi na kuweza kutatua matatizo yangu.Pia kama mtu anaweza akanifadhili,natumaini mtanisaidia asanteni.