Naombeni mkopo huu utumike ipasavyo

Naombeni mkopo huu utumike ipasavyo

Best home tutor

Senior Member
Joined
May 8, 2026
Posts
194
Reaction score
265
Mimi nishanunua chupi ya chuma wewe je

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limefikia makubaliano ya awali na serikali ya Tanzania kutoa ufadhili wa dola milioni 375.5 (takriban Shilingi bilioni 978.3).

Hatua hii inalenga kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na migogoro ya kimataifa, ikiwemo hali ya wasiwasi kati ya Marekani, Israel, na Iran.

Katika taarifa yake, IMF imebainisha kuwa Tanzania imefanikiwa kufikia malengo yake ya kiuchumi. Ukuaji wa uchumi unatajwa kubaki imara, huku mfumuko wa bei ukiwa mdogo na thabiti. Aidha, uwezo wa Benki Kuu ya Tanzania katika kusimamia sarafu za kigeni umeripotiwa kutosheleza mahitaji ya nchi.

Ripoti hiyo pia imepongeza ongezeko la matumizi ya serikali katika sekta muhimu za elimu na afya. Vilevile, Tanzania imepata sifa kwa kuimarisha ustahimilivu wake dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, hatua inayosaidia kulinda uchumi na jamii dhidi ya changamoto za kimazingira.

Hadi kufikia mwezi Mei 2026, jumla ya deni la Tanzania kwa IMF inakadiriwa kuwa takriban Dola za Kimarekani bilioni 1.43 (sawa na takriban Shilingi trilioni 3.73 za Kitanzania).
 
Deni la taifa Kwa ujumla ni shingap saiv?
 
Yamepata pesa za kuchezea. Wakati Nchi zingine zinapambana kumaliza madeni, Bibi hindu ni mwendo awa kukopa tu, na mzigo kumtwisha mwananchi.
 
Back
Top Bottom