Naombeni kujua ukweli

Nachaone

Member
Sep 24, 2018
67
73
Huwa nasikia sikia kuwa endapo wazazi ambao kundi zao za damu zinafanana na wakapata Mtoto basi huyo Mtoto atakuwa na matatizo mengi ya kiafya na hii huweza kupelekea umauti kwa Mtoto huyo.

KUNA UKWELI KUHUSU HILI?? Na kama sio kweli ni kipi ambacho kinaweza kusababisha matatizo ya kiafya kwa mtoto atakayezaliwa kutokana na vinasaba vya wazazi kutoendana???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachojua Mimi kitaalamu mtoto hupata complication endapo mama/mjamzito Rhesus Factor iwe NEGATIVE, afu Mtoto awe POSITIVE kwa ujauzito wa Kwanza mtoto atakuwa salama tu ila kwa ujauzito wa pili ikitokea iwe Kama hali niliyotaja hapo juu tatizo litatokea maana tayari Mama atakuwa ameshatengeneza Antibodies dhid ya rhesus Positive za mtoto maana siku zote Positive hutawala negative na inakuwa Kama kitu kipya Kwa mama.. lakini hali Kama hiyo huweza kutokea pia hasa mama awe Blood group O afu Mtoto awe blood group A au B japo hii huwa haina hataree sana. Kwa tatizo la Kwanza hapo juu Kuna sindano huitwa Anti-D ambayo mama huchomwa mapema ndani ya masaa 72 baada ya kujifungua na hapo kwa mimba itakayofuata hata iweje mtoto atabaki salama kitaalamu complications zote nilizotaja hapo juu huitwa HAEMOLYTIC DISEASE OF NEW BORN..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom