Agri-processing and Value addition
1. Coconut Milk for Vegans/Vegetarians/Vegan Diet
Kuna mkuu hapo kakushauri utengeneze tui la nazi kwa ajili ya kupikia, iko pouwa. Ila kwa sasa kuna kundi la watu ambao wanafuata mfumo wa kula vyakula vitokanavyo na mboga za majani, hivyo basi waacha kula kitu chochote kile kitokanacho na mnyama, ikiwemo maziwa
Sasa mkuu, wewe unachotakiwa kufanya ni kuchukua ile tui ya nazi na kuifanyia mafekeche (homogenization na pasteurization etc.) halafu unaya-brand kama mbadala wa maziwa ya ng'ombe/mbuzi/ngamia etc kwa hao wasiokula mazao yote ya nyama.
2.Coconut Flakes
Hapa unachukua nyama ya nazi iliyokomaa, unaitenganisha kutoka kwenye gamba lake, halafu unaimenya kwa kutumia "potato/Vegetable peeler", utakacho kipata baada ya hapo ndo Coconut flakes.
Unaweza i-brand kama unsweetened au Sweetened au Flavoured Coconut flakes na hizi unaweza kutumika kama "snacks" kama ilivyo kwa irish potato crisps.
Unaweza kutumia
2a.food dehydrator = ili upate dehydrated coconut flakes
2b.Oven = ili upate toasted coconut flakes
Kama nilivyoeleza hapo, soko kubwa ni kama itaibrand kama snacks au urembo wa keki(cake topping)
3.Coconut oil
kama alivyosema mkuu huko juu, tengeneza mafuta ya nazi, halafu kwenye kuya-brand utumie maneno kama "Organic coconut oil", "Extra virgin coconut oil", "Cold pressed coconut oil". Hizo ni njia tu za kutanganza bidhaa ila utawavutia wale wanapenda kutumia vitu halisia.
Mafuta hayo yaweza yakawa ya
a.kupikia
b.kujipaka
Pia unaweza tumia mafuta hayo ya nazi katika kutengeza sabuni za nazi, zile sifa nzuri nzuri za mafuta ya nazi, ndio unapachika kwenye label ya sabuni yako.
4.Coconut water
Inasemekana maji ya dafu ni mazuri sana kawa afya ya miili yetu. Hivyo basi, ukiweza kuchuja, kuyafanyia mafekeche ili yakae muda mrefu bila kuharibika(atleast miezi 6) na kuyaweka katika vifungashio/chupa, utakuwa umepiga hatua kubwa.
Kama kawaida soko letu ni kwa wale wale wapenda afya tele aka healthy life stlye.
Nyama ya dafu utaifanya kama hapo juu , yaani "coconut flakes"
5. Coconut based jewellery, beauty objects
Hapa mkuu unatumia lile gamba(coconut shell) kutengeneza bidhaa za urembo. Wakati nakua nilishawahi ona machanuo ya nywele pamoja na vibanio vya vywele vilivyotengenezwa kwa gamba la nazi, siku hizi siyaoni sana.
Hapa mkuu soko lako utalenga ndani na nje ya nchi(Kupitia masoko mtandao kama Etsy).
6.Cocopeat au Coco coir
Mkuu, kwenye nazi au dafu kuna lile ligamba la nje kabisa linalotolewa lile linalokuwa na nyuzi nyuzi. Lile unaweza kuliozesha na kupata cocopeat/coco coir ule mchanga flani hivi wanaotumia kuoteshea miche vya miti na mboga kama nyanya.
Pia unaweza kuchukua na yale machicha yaliyobaki pale namba moja, ukayaozesha pamoja na haya magamba ukapata mchanga ambao wewe utau-brand kama soil conditioner, pia bado unaweza tumiwa na wale wakuoteshea miche.
katika yote hayo mkuu, End-product/By-product ya mchakato wa kwanza ndo inakuwa Raw material(Malighafi) ya mchakato wa pili.