Naomba wanasheria na waendesha mashtaka mnisaidie hili

Voiced Voice

JF-Expert Member
Feb 1, 2018
248
249
Ukifuatilia kesi nyingi za serikali ambazo ama zinatupwa au serikali inashindwa utagundua kuwa sababu kuu ni ama kesi kufunguliwa kwa kifungu kisichohusika badala ya kifungu xy inafunguliwa kwa kifungu zf au kwa sheria isiyokuwepo au isiyotumika tena.

Zamani nilijua idara za serikali zinajaa wabobezi ma wajuzi tena wanakua wengi. Hivi inakuwaje mpaka waendesha mastaka na mawakili wa serikali kufungua kesi kwa vifungu vilivyokosewa?

Inatokea nini mpaka wanatumia kifungu kisichokuwepo kabisaa au kilihuishwa? Hivi kwenye sheria kuna siri ambazo huwezi kuzijua mpaka ufike mahakamani hata kama umebobea kwenye sheria?

Nilitegemea kushindwa kesi kuambatane na kushindwa kutoa ushahidi unaojitosheleza au kukosa ushahidi kabisa. Hii ya kufungua kesi kimakosa sijaielewa bado.

Je hawajui? wanakurupuka? hawajabobea? au kuna kitu sheria inacho wengine hatukijui?

Msaada tafadhari
 
Kuweka wrong provision ni kosa la kiubinadamu eidha kusahau, kutojua kama kuna mabadiliko ya sheria husika ,muda mwingine ni uvivu wa kuendekeza tabia ya copy and paste..na muda mwingine ni uchovu wa akili ,unakutana na mtu kwa kutojua ukomo wa kufile document mahakamani anampa mwanasheria au paralegal amwandalie documents ili awahi deadline dakika chache kabla ya shughuli za kimahakama hazijafika kikomo kwa siku hiyo, wadhani huyu mwandishi atapata muda wa kutosha kuproof read alichokiandika .... Kushindwa kesi kwa technicalities hakufanywi na mawakili wa serikali pekee ipo hata kwa mawakili wa kujitegemea....
 
Harafu kesi nyingi za serkal, serkal inashindwa kuna nn hapa mpaka kila kesi serkal ishindwe na mtu au watu binafs au kuna ka mchezo hapa nn watu wanatengeneza pesa.!?
 
Ungejaribu kuishitaki ili ushinde tungekuamini zaidi,hapa una generalize sana.
 
Utakua ni mgeni Tanzania au huwa hufatilii habari au umeamua kujibu lakini hukuwa na cha kujibu. Kwa nini nasema hivi? kwa kuwa ni wazi kesi nying serikali inashindwa na sio kushindwa kwa ushahidi hapana bali ni kwa makosa ya kufungua kesi kwa kifungu kisichokuwepo au kufungua kwa kifungu kilichofutwa, kutumia mifano isiyo sahihi na nk. kwa mtanzania halisi lazima ujiulize hawa wanaolipwa mishahara wanakuwaje na uzembe huu?
 
Mahakama kuu arusha wakati wa rulling ya kesi juu ya dhamana ya lema, ilioneshwa kusikitishwa sana na uwezo mdogo wa wanasheria wa serikali, na ikamshangaa sanaa AG kua na wanasheria mbumbumbu kama wale.

Shida inakuja ni pale ni je unaguswa vp na kesi yenyewe? Una interest gani pale? Sasa unashangaa unaambiwa na boss wako (toka ofisi ya AG) uende ukaendeshe kesi flani ukifika huko wewe unakua hauna cha kupoteza wala cha kupata, kwaio unajifanyia tu kutimiza wajibu, na kasumba hii mdio inawakuta karibu wanasheria wote wa serikali, ni vilaza huwezi kuamini, wanashindwa karibu kila kesi, wao silaha yao hua iko kwenye Nolle Proseque tu ambayo nayo mahakama kuu juzi imeagiza ifutiliwe mbali, DPP na ndugu zake hao wa serikali hawapaswi kua na mamlaka hayo.
 
Ukifuatilia kesi nyingi za serikali ambazo ama zinatupwa au serikali inashindwa utagundua kuwa sababu kuu ni ama kesi kufunguliwa kwa kifungu kisichohusika badala ya kifungu xy inafunguliwa kwa kifungu zf au kwa sheria isiyokuwepo au isiyotumika tena.

Zamani nilijua idara za serikali zinajaa wabobezi ma wajuzi tena wanakua wengi. Hivi inakuwaje mpaka waendesha mastaka na mawakili wa serikali kufungua kesi kwa vifungu vilivyokosewa?

Inatokea nini mpaka wanatumia kifungu kisichokuwepo kabisaa au kilihuishwa? Hivi kwenye sheria kuna siri ambazo huwezi kuzijua mpaka ufike mahakamani hata kama umebobea kwenye sheria?

Nilitegemea kushindwa kesi kuambatane na kushindwa kutoa ushahidi unaojitosheleza au kukosa ushahidi kabisa. Hii ya kufungua kesi kimakosa sijaielewa bado.

Je hawajui? wanakurupuka? hawajabobea? au kuna kitu sheria inacho wengine hatukijui?

Msaada tafadhari
ungeweka asilimia, labda kwa mwaka mmoja kesi kadhaa zilifunguliwa, kadhaa zilikuwa na defective charge sheet na zikapigwa chini na kadhaa zilishindwa kwa sababu fulani, na kadhaa walishinda. kwa kukusaidia ni kwamba, ukiona kesi hadi imesikilizwa na hakimu mwishoni anakuja kusema haikufunguliwa kwa hati ya mashitaka sahihi, mfano kama ni defective, ni kosa la wote, mahakama na waendesha mashitaka, usilaumu upande mmoja. kabla ya kusajili kesi, hakimu anatakiwa kujiridhisha na vifungu, akiona kifungu sicho au kimekosewa anatakiwa kukataa kusajili. kama amejisahau ikasajiliwa akagundua katikati, kifungu cha 234 CPA kuna option ya kubadilisha hati ya masahitaka hata kama kesi ilishaanda, au kurekebisha.

vilevile, ulishawahi kutembelea magereza? kuna wafungwa wamejaa, watu hadi wanalala ubavu ubavu, magereza nyingi tz zimezidiwa na wafungwa...kwanini? kwasababu kuna kesi nyingi hao hao mawakili walishinda watu wakafungwa (pamoja na kwamba kuna mahabusu pia)......kuna matatizo mengi mawakili wa serikali wanayafanya, lakini watu huona mabaya tu mazuri au ushindi huwa hawauoni. kila siku kesi zinaendelea mahakamani na kuna watu wanafungwa lakini asipofungwa mmoja tu utakuta kelele.....
 
Mahakama kuu arusha wakati wa rulling ya kesi juu ya dhamana ya lema, ilioneshwa kusikitishwa sana na uwezo mdogo wa wanasheria wa serikali, na ikamshangaa sanaa AG kua na wanasheria mbumbumbu kama wale.

Shida inakuja ni pale ni je unaguswa vp na kesi yenyewe? Una interest gani pale? Sasa unashangaa unaambiwa na boss wako (toka ofisi ya AG) uende ukaendeshe kesi flani ukifika huko wewe unakua hauna cha kupoteza wala cha kupata, kwaio unajifanyia tu kutimiza wajibu, na kasumba hii mdio inawakuta karibu wanasheria wote wa serikali, ni vilaza huwezi kuamini, wanashindwa karibu kila kesi, wao silaha yao hua iko kwenye Nolle Proseque tu ambayo nayo mahakama kuu juzi imeagiza ifutiliwe mbali, DPP na ndugu zake hao wa serikali hawapaswi kua na mamlaka hayo.
i beg to disagree with you kabisa. siwezi kuwatukana hao jamaa kuwa vilaza kwasababu nilishapita huko naelewa. kwa taarifa yako hata uwakili wa kujitegemea, mawakili wazuri huwa ni wale waliopitia AG, fanya tafiti utaelewa. wabobezi wa criminal wote huwa wameshapitia AG, na ukijua civil ni rahisi mno...hivyo mtaalamu wa civil hawezi kujisifu sana. hii ni ngumu kuelewa au kuamini hadi utakaposhitakiwa na kukutana nao.
 
ungeweka asilimia, labda kwa mwaka mmoja kesi kadhaa zilifunguliwa, kadhaa zilikuwa na defective charge sheet na zikapigwa chini na kadhaa zilishindwa kwa sababu fulani, na kadhaa walishinda. kwa kukusaidia ni kwamba, ukiona kesi hadi imesikilizwa na hakimu mwishoni anakuja kusema haikufunguliwa kwa hati ya mashitaka sahihi, mfano kama ni defective, ni kosa la wote, mahakama na waendesha mashitaka, usilaumu upande mmoja. kabla ya kusajili kesi, hakimu anatakiwa kujiridhisha na vifungu, akiona kifungu sicho au kimekosewa anatakiwa kukataa kusajili. kama amejisahau ikasajiliwa akagundua katikati, kifungu cha 234 CPA kuna option ya kubadilisha hati ya masahitaka hata kama kesi ilishaanda, au kurekebisha.

vilevile, ulishawahi kutembelea magereza? kuna wafungwa wamejaa, watu hadi wanalala ubavu ubavu, magereza nyingi tz zimezidiwa na wafungwa...kwanini? kwasababu kuna kesi nyingi hao hao mawakili walishinda watu wakafungwa (pamoja na kwamba kuna mahabusu pia)......kuna matatizo mengi mawakili wa serikali wanayafanya, lakini watu huona mabaya tu mazuri au ushindi huwa hawauoni. kila siku kesi zinaendelea mahakamani na kuna watu wanafungwa lakini asipofungwa mmoja tu utakuta kelele.....
Sasa kama ...kesi ikitolewa hukumu ...kwa kutotumia kifungu cha sheria kilicho sahii ...iyo hukumu itakuwa sahii kweli ...au mtu anaweza kukata rufaa ...kwa kutumia iyo hoja akaachiwa kwa kusema ...kuwa mahakama ilimuhukumu kwa kifungu cha sheria kisicho sahii.
 
kama imefika hadi hukumu wakati hawajabadilisha, hapo imekula kwao, manake ni kwamba hawajaprove charge, au kama charge ni defective, ni sawa na hamna charge yeyote ile, hewa tu.
 
Ndugu wanasheria naomba kuuliza ni ushahidi wa aina gani unaokubarika mahakaman?? Mimi nina photocopy ya hati ya makubaliano ya deni na mtuhumiwa lakini hakimu anaonyesha kuto ukubali ushahidi huo anahitaji original copy
 
ni mahakama gani umeenda? kasome kifungu cha 66 cha sheria ya ushahidi, utaona documentary evidence inatakiwa kuwa original, sio photocopy. pia endelea section 67 ya sheria ya ushahidi utaona kuna mazingira yanayoruhusiwa photocopy(secondary evidence) kupokelewa. kuna baadhi ya mazingira unatakiwa kuwa imekuwa certified, kuna baadhi ya mazingira hata isipokuwa certified inapokelewa mfano kama original imepotea au imekuwa destroyed etc.
 
ungeweka asilimia, labda kwa mwaka mmoja kesi kadhaa zilifunguliwa, kadhaa zilikuwa na defective charge sheet na zikapigwa chini na kadhaa zilishindwa kwa sababu fulani, na kadhaa walishinda. kwa kukusaidia ni kwamba, ukiona kesi hadi imesikilizwa na hakimu mwishoni anakuja kusema haikufunguliwa kwa hati ya mashitaka sahihi, mfano kama ni defective, ni kosa la wote, mahakama na waendesha mashitaka, usilaumu upande mmoja. kabla ya kusajili kesi, hakimu anatakiwa kujiridhisha na vifungu, akiona kifungu sicho au kimekosewa anatakiwa kukataa kusajili. kama amejisahau ikasajiliwa akagundua katikati, kifungu cha 234 CPA kuna option ya kubadilisha hati ya masahitaka hata kama kesi ilishaanda, au kurekebisha.

vilevile, ulishawahi kutembelea magereza? kuna wafungwa wamejaa, watu hadi wanalala ubavu ubavu, magereza nyingi tz zimezidiwa na wafungwa...kwanini? kwasababu kuna kesi nyingi hao hao mawakili walishinda watu wakafungwa (pamoja na kwamba kuna mahabusu pia)......kuna matatizo mengi mawakili wa serikali wanayafanya, lakini watu huona mabaya tu mazuri au ushindi huwa hawauoni. kila siku kesi zinaendelea mahakamani na kuna watu wanafungwa lakini asipofungwa mmoja tu utakuta kelele.....
Naweza kukujibu kitu kimoja tu kwa muda huu. Hao wafungwa walijazana jera ni wezi wa mifugo, vibaka, wakabaji, wagonvi, wavuta bangi na jamii hiyo. Wale wanaolitia/ waliolitia taifa hasara ya mabilioni tunaona wakiachiwa ama kwa kesi kufunguliwa kimakosa au kifungu hakipo.
 
Kuweka wrong provision ni kosa la kiubinadamu eidha kusahau, kutojua kama kuna mabadiliko ya sheria husika ,muda mwingine ni uvivu wa kuendekeza tabia ya copy and paste..na muda mwingine ni uchovu wa akili ,unakutana na mtu kwa kutojua ukomo wa kufile document mahakamani anampa mwanasheria au paralegal amwandalie documents ili awahi deadline dakika chache kabla ya shughuli za kimahakama hazijafika kikomo kwa siku hiyo, wadhani huyu mwandishi atapata muda wa kutosha kuproof read alichokiandika .... Kushindwa kesi kwa technicalities hakufanywi na mawakili wa serikali pekee ipo hata kwa mawakili wa kujitegemea....
Habari kiongozi.
Mimi ni mwl ktk shule moja ya private hapa Dar es salaam.

NINA MATATIZO MAKUBWA
1. Wameniundia zengwe kuwa nimewapa mtihani wanafunzi
2. Wakati nasahisha wakanizuia kumalizia, wakamalizia wao
3. Toka hapo wamenizuia nisaidie shuleni
4. Wameajir mwl mwingine

YOTE HAYA YANAFANYIKA
mimi sijaitwa na kuhojiwa kuhusu tuhuma hiyo.
Pia hawajanipa barua yoyote ya kunisimamisha au kunifukuza

SWALI
sheria zikoje ktk kumsimamisha na kumfukuza mwajiriwa kazini

Pia vp ni sawa kwa mkuu wa shule kutoa tu amri kwa walinzi pale getini wanizuie au maandishi yalihitajika

MSAADA WA KISHERIA PLZ

Natanguliza shukran
 
Back
Top Bottom