Naomba uzoefu kwa mliowahi tumia hii mashine

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,802
Wakuu naomba kwa aliyewahi tumia hii mashine ya kupandia mazao anipe uzoefu kuhusu ubora(uimara) wake,urahisi wa kutumia na mazao yanayotumika kupandia kwa ujumla.
20230205_181757.jpg
 
Binafsi naona ili uwe na UCHUNGU na kazi yako ya kilimo, usitafute urahisi. Tumia nguvu, pambana kupanda bila mashine ili upate hasira
 
Binafsi naona ili uwe na UCHUNGU na kazi yako ya kilimo, usitafute urahisi. Tumia nguvu, pambana kupanda bila mashine ili upate hasira

Mashine zipo ili kuturahisishia kazi, sio kila anaetumia mashine hana uchungu na kazi yake.

Nikirudi mwenye maada, niliwahi kuiona hiyo mashine mwaka jana kwenye wiki ya maonyesho ya wana katavi huko mpanda. Sikufanikiwa kupata details zaidi maana mhudumu wa banda hilo hakuwepo na sikupata nafasi ya kurudi kwenye maonyesho hayo siku nyingine
 
Ni mashine nzuri kwenye suala Zima la upandaji. Kwa Mimi ninayo na nimeitumia kupanda mahindi na alizeti na mazao yanaendelea vizuri
 
Ok,vipi wakati wa kupanda wanahitajika watu wangapi?
Miaka kadhaa iliyopita Kuna rafiki yangu alinunua hii mashine, japo sio hii brand.

Mashine ni delicate.

Ni rahisi kutumia
Unaisukuma kwenda mbele hivyo vitu kama vibomba vinachimba na kupanda mbegu.

Ina vi disc mbalimbali vya kukadilia ukubwa wa mbegu... Kuna disc ya kupandia mahindi, maharage n.k. hivyo unaweza kupandia mazao aina tofauti

Vibomba vya kupandia vinakuwa vimewekwa kwa urefu Fulani kutoka kimoja mpaka kingine let say 30 cm ukitaka kupanda spacing ya 60cm unafunga kibomba kimoja Kati ya viwili n.k.

Unahitaji ardhi laini mfano iliyopigwa harrow ili kuweza kutumia hiyo mashine
.
.
.
mtu mmoja anaweza ku operate bila shida hii mashine
 
Safi wewe ni Mwl. mzuri sana. Sina swali.
 
Back
Top Bottom