Karibu Arusha... lakini wacha maneno mengi Dar uwe umejitayarisha kua mbabe hapa mjini kwetu...
1. Maisha Arusha ni ya garama sana kwa sababu ya mashirika yanje yaliyomo hapa... Lakini bado tunagangamala hivyo hivyo..
2. Maji yapo lakini inategema upo maeneo gani... Shida ni kama wakati wa kiangazi.
3. Umeme ni tatizo nahisi nchi nzima na sisi tunapokea share yetu
4. Wengi wana weza kusema barabara zetu ni mbaya na wakawa ni wakweli ila hatuna mafuriko wakati wa mvua kama Dar..
5. Magari kusema ukweli yanaongezeka lakini jam ya hapa ni kutegemea unaishi upandegani wa mjii na siyo ya kuamka saa 10 usiku kuwahi.
6. Kazi zipo lakini inategemea qualification yako... Hapa tunayo companies ya Tours nyingi tu ama organization's kibao wewe tu..
7. Bishara zetu hapa ni kwa dola... lol... Inategemea unakuja na idea gani opportunities zipo
Haya ndiyo mawazo yangu juu ya mji wa ARUSHA.