Naomba Ushauri.

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,719
107,770
Wana JF wenzangu naomba ushauri kuhusu miji hii MWANZA,DODOMA,ARUSHA

Ushauri huu uzingatie maisha kiujumla i.e gharama za maisha,huduma(maji/umeme/barabara) msongamano na upatikanaji wa kazi na biashara katika miji hii.

Nilizaliwa na kukulia DSM lakini DSM niliyoiacha sio niliyoikuta na kwa kweli maisha yake kwa jumla naona yamebadilika sana.

Naomba wanaJF wanaoishi au walio na uzoefu wowote na miji niliyoitaja wanisaidie
ASANTENI.
 
Karibu Arusha... lakini wacha maneno mengi Dar uwe umejitayarisha kua mbabe hapa mjini kwetu...

1. Maisha Arusha ni ya garama sana kwa sababu ya mashirika yanje yaliyomo hapa... Lakini bado tunagangamala hivyo hivyo..
2. Maji yapo lakini inategema upo maeneo gani... Shida ni kama wakati wa kiangazi.
3. Umeme ni tatizo nahisi nchi nzima na sisi tunapokea share yetu
4. Wengi wana weza kusema barabara zetu ni mbaya na wakawa ni wakweli ila hatuna mafuriko wakati wa mvua kama Dar..
5. Magari kusema ukweli yanaongezeka lakini jam ya hapa ni kutegemea unaishi upandegani wa mjii na siyo ya kuamka saa 10 usiku kuwahi.
6. Kazi zipo lakini inategemea qualification yako... Hapa tunayo companies ya Tours nyingi tu ama organization's kibao wewe tu..
7. Bishara zetu hapa ni kwa dola... lol... Inategemea unakuja na idea gani opportunities zipo

Haya ndiyo mawazo yangu juu ya mji wa ARUSHA.
 
aaah kumbe loner wewe ni wa kumunyumba eeh....anyway mbebabox karibu jiji la utalii...hapo kwenye blue usiogope sana, sio sehemu zote, ila jua tu maisha ya Arusha yapo ghali kidogo lakini utazoea, biashara kubwa hapa ni mambo ya utalii japo pia zingine zinalipa lakini sio sawa na Dar, hali ya usalama sio nzuri saaaaana jiandae kukutana na mashine zikindirima popote utakapokuwa unatembea japo kwa sasa hali hiyo imepungua kidogo. bar ni nyingi sana na guest houses (gesti) ndio usiseme na week end zote zinakuwa zimejaa (habari ndio hiyo)....kwa sasa ni hayo
 
Hali ya hewa nayo ni murua...hutogombani na joto la Dar!:target:

ARUSHA hio i guess,pia watu wa huko mnaonyesha ni wakarimu.........watu wa DAR hata ukiwauliza njia kujibu mpaka uwape kitu kidogo
 
Jaribu Dodoma
Kwanza gharama ya maisha ni ndogo ukilinganisha na dar au arusha.
Mji mdogo(mjini), hamna msongamano wa magari. Barabara ili mradi zinapitika mkuu.
Vumbi na upepo ni tatizo pia sehemu zingine maji ya chumvi sana, ila huduma kama umeme na maji unaweza kupata.
Upatikanaji wa kazi, hapo sina uhakika sana ila kuna mashirika binafsi na hata ofisi za serikali jaribu bahati yako.

Karibu sana Dom..
 
ARUSHA hio i guess,pia watu wa huko mnaonyesha ni wakarimu.........watu wa DAR hata ukiwauliza njia kujibu mpaka uwape kitu kidogo
Dar hata mtu akikukanyaga samahani ukiipata una bahati.Kila mtu anakimbia kimbia na mishemishe zake hata hamwoni mwenzake....ila A taun hata asiekujua anakupa tabasamu!!:welcome:
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom