Naomba ushauri

Asante kwa ushauri,kiukweli nimechanganyikiwa.
Kuchanganyikiwa kupo, tena sana tu.............. ila hapa la maana ni kulia sana, ukinyamaza sali sana umwombe Mungu akuonyeshe njia.
Huwa nikiwa na jambo la kunitatanisha kulia kunanisaidia sana kuniweka sawa, kuniondolea hasira..... yaani nisipolia hata kusali siwezi. nikishanyamaza sasa ni busara tupu, ha haaaaaaaaaaaaa.
Pole mwaya
 
Jamani mama Bokhe, pamoja na kuwa nimekushauri mwanzo lakini naomba niongeze na haya na kama kweli utakubaliana na kuskiliza wanavyoosahuri wana jamvi basi, chukua hatua ukiyajua aya.

Iko hivi tatizo lililo ingia nyumbani mwako laweza kuwakuzaa matatzo mengi kuliko unavyofikiri au lilivyo, hii inatokana na ukweli kwamba jambo hili liko kihisia zaid, kiimani na uvunjaji wa heshima kitu ambacho mwisho wa siku huzaa fedheha na aibu na mafarakano makubwa katika familia. Anyway haijalisha ni muda gani ambao wewe umetumia kuiweka iyo familia yako pamoja kwa upendo na amani, ila kazi iyo yote yaweza kuharibiwa leo kama utahamalika na kutatua pasi hekima na utashi wa mambo.

Sisemi kwa ushabiki, wala kwa kutokujua but kama mama ambaye naweza kuwa nina experience ya mambo makubwa kuliko haya so what am saying ni kama vile am wearing your shoes.

Katika maisha kama unataka kurekebisha tabia ya mtu basi kuna jambo moja kubwa waweza lifanya nalo ni unafanya kitu kiitwacho reinforcement. Hii yaweza kuwa +ve ama -ve reinforcement. _ve reinforcement maana yake you induce something bitter in order to initiate +ve behaviour change na -ve reinforcement you remove something sweet/good inorder to initiate +behaviour change.

Hya nirudi kwenye point za msingi niliposema mwache huyo binti akae hapo ndani hadi ajifugue nilimaanisha unatumia both +ve &-ve reinforcement kwa wakati mmoja. Nafikiri ni ngumu kidogo kuelewa lakin kwanza kwa mumeo ni adhabu kwani yeye alitarajia utaact tofauti kabisa na hali halisi pia kwa binti ni adhabu ya milele amini usiamini. Na tena kama ukiweza kabla ya kauoangea na mumeo uwe umeshajipanga kabisa kuwa ni kwanini hutaki aondoke manake hata akitoka huyu ajaye anaweza pia kukutwa na jambo kama hili so uwe makini sana. Jipe moyo mkuu na weka nia na mungu akusimamie kaa na binti hadi ajifungue na uone kweli mtoto ni wa mumeo au la. wakati huu wote mumeo atajifunza mambo mengi sana.

Kuna hatari pia ya binti huyu kuwa amekuja kukupindua hili lisikutishe hata kidogo,kwani hawez hata kama ataloga, kwanza kabisa mweleze binti japo kapata ujauzito bado yeye ni binti wa kazi tu na siyo mke mwenzio. pia hakikisha kazi za ndani anafanya kama kaawaida wala usiwe na ukatili juu yake but uwe strict asikuzoee. Wakati yupo usimwambie mtu yyte yule jambo lolote zaid ya kusema na Mungu wako tu basi. amka saa nane kila siku sali kwa kumaanisha juu ya upepo huu mbaya ulio ingia ndani kwako na mungu atafanya njia.

Kuhusu watt wako kma ni wakubw yaani 18> just tell them kwa njia ya kirafiki sana pasi kuhamalika au kuonyesha kumchukia baba yao. unapowaambia tell them the truth ila watahadharishe wasiseme na baba yao wala kumchukia wala kumpiga huyo binti. kwanini nasema waambie hawa ndio watakao kupa faraja kipindi hiki.

Nina uhakika kabisa humu jamvini kuna wtu wengi ambao ni wahanga wa kumchukia baba kwasababu ya alivyo mtenda mama enzi tunakua but siyo sahihi manake ni laana kabisa. Waambie wanao kwa lugha nyepesi ili wakusaidie kuwa walinzi w amani yako ila usiwachochee kumchukia baba, kwa wamama wengi jambo hili linatushinda hasa tunapokuwa na wtoto wakubwa na siku zote hupendelea kuwa karibu na watoto kuliko wtoto kuwa karibu na baba jambo ambalo hubomoa misingi ya upendo na amani uliyoijenga wakti uko kijana.

Kumbuka kuwa ingawa muumeo kazini haibadilishi jina la yeye kuwa baba wa watt wako au kuwa mumeo miliyeapa kanisani, pia haipunguzi heshima yake ya kuwa binadamu manake kukosea ni kawaida ila tunafautiana extent tu.

ikiwa kweli utamtanguliza Mungu katika hili, kisha ukajua jinsi ya kuwaelekeza wanao kwa hekima na pia ukatumia busara katika kurekebisha hali hii ni dhahiri kuwa utashinda tu.

Najua dada yangu unapita pagumu sana, ila ukihamalika utapoteza kila kitu ullichojenga ni ngumu sana kuish na adui yako nyumba moja but ukiwweza nakuhakikishia utaona faida yake. najua nitatofautiana na wengi sana katika hili ilanimeona ushauri huu ukifanya kazi kwa watu walioukubali na mpaka sasa waume wameshika adabu.
kama kuna ushauri zaid niko kwa ajili yako tena bure kabisa just pm me.

Nimelichukulia kwa mtazamo tofauti kidogo so kama nitakuwa nmekosea mnisamehe sana ila kama mnataka kujua nini maana ya maisha hasa uliyoyajenga for years kwa upendo na ushirikiano na nini thamani ya mwanamke anayejua kuact prudently pale jambo gumu linapomtokea waulizeni wanaume wa humu jamvini MziziMkavu, ama Asprin, ama Bishanga ama mito ama boss nk.

amani na upendo na ushirikiano ulioujenga kwa miaka 10 siyo mchezo kuja kuibomoa kwa kosa la mara ya kwanza kama hivi, utajutia nguvu na wakati wako wote. Anyway mnisamehe kama nimekuwa niko tofauti sana na nyie.
 
Last edited by a moderator:
the boss we hujui tuu wengine huwa na ndoto za kuolewa na maboss zao,niliwah ku na housgal ambae alikua na ka tabia ka kutokuvaa chupi cku za weekend au ile mida ya kurud mr jion then atahakikisha kisket alichovaa n chepes au kinabana boss wake wa kike alipokuja kugundua akadai anackia joto jaman joto gan jion na w?end tu?so uckute huyo hg alifundishwa kwao amtege boss wake ucmtetee

hahahaaaaaaaa
umenikumbusha nilileta hg mpya kwangu.......
Bahati mbaya au nzuri mume wangu alikuwa kasafiri.....nikaka nae wiki nzima bila tatizo....

Baada ya mume wangu kurudi nikanote hg anavaa viguo vya ajabu ambavyo nilishapiga marufuku ndani mwangu(wanangu na hg wote hawaruhusiwi kuvaa), kumuuliza akasema anahisi joto...... Nikamwonya.....

Next day akaniuliza lini atampikia mume wangu chakula (kawaida napika mwenyewe chakuka cha jioni na chai)

kali kuliko kuna siku saa tano usiku (kulikuwa na mpira) nipo na husband sebuleni, dada katoka chumbani kwake kifua wazi, kwa maana ya matiti nje , chini kavaa kigagulo..... I see sikuwahi kukasirika kana siku hiyo...nilipomuuliza kaniambia dar joto........

Ilibidi nimpandishe basi arudi kwao kesho asubuhi...... Mie binafsi alinishinda.......
Inauma sana unapompokea mdada, na kumtreat kama ndugu yako, plus mshahara, off, nguo, hospitali, mapumziko na mazagazaga yote halafu atake kuishia kitandani kwako na mumeo......

Na inauma zaidi mumeo anapodiriki kula humo humo ndani.... Pole sasa mama bhoke
 
Pole sana dada kwa mkasa uliokukuta. Huna haja ya kuchukua maamuzi ya kumkomoa huyo hg wako wala mumeo, tulia chini na ikiwezekana umsaidie huyo hg hadi atakapojifungua salama baadae ikiwezekana aende kwao vizuri tu. Kilichotokea kwako ni kitu ambacho kwa binadamuu yeyote angeumia lakini uamuzi wa busara ndio njia pekee ya kufikia suluhu ya mustakabali mzima. Siku zote ndoa huongozwa katika uvumilivu, hekima, busara, kujali, upendo, kuaminiana na uaminifu. Ikiwa mmojawapo wa wanandoa akikosa sifa hizo, matokeo yake huwa kama yaliyokukuta Mama Bhoke. Kaa chini na mumeo au muwashirikishe watu wazima pia mjadili jinsi ya kusuluhisha tatizo kwa amani ili baadae muendelee na maisha yenu na mjaribu pia kuangalia nyufa zilizopelekea mumeo kukusaliti mzizibe yasije yakajirudia tena hapo baadae.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom