Naomba ushauri

KALENDA

Member
Jan 21, 2011
72
28
Habari zenu wana JF,
Hivi karibuni nilimshitaki mtu kwa kosa la kuiba mali niliyomkabidhi kuiuza dukani kwangu.

Baada ya kesi kuisha mahakama / Hakimu alimuhukumu mtuhumiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja
nje ya gereza pamoja na kulipa pesa anazodaiwa kwa kulipia mahakamani kiasi alichopangiwa kila mwezi hadi
atakapomaliza deni lake.

Tangu hukumu imetolewa sasa ni miezi mitatu na huyo mfungwa amelipa pesa anazodaiwa katika mwezi mmoja
tu kati ya miezi 12 anayotakiwa kulipa. Kila ninapokwenda mahakamani kuchukuwa pesa anazotakiwa kulipa,
cashier ananiambia kuwa mfungwa wangu anasema hana pesa za kulipia deni langu.

Wataalamu wa sheria naomba mnifahamishe natakiwa kuchukuwa hatua gani ili niweze kupata haki yangu.
Natanguliza shukurani.
 
Back
Top Bottom