Kbd
JF-Expert Member
- Oct 9, 2009
- 1,260
- 447
Wanajukwaa nawasalimu wote kwa heshima na taadhima. Mimi Ninaishi kwenye nyumba ya kupanga mahali fulani na baba na mama mwenye nyumba wanaishi hapo hapo. Sasa huyu baba mwenye nyumba anatabia ya kumpiga mke wake sana esp anapolewa. Hiyo tabia imekuwa ikiniudhi sana sana na nilishawahi kuongea nae kuhusu hiyo tabia akaahidi kujirekebisha. Alijirekebisha kwa muda lakini naona sasa imeanza upya.................. Yaani ni mkorofi sana, anambonda mkewe na matusi na maneno ya kashfa mengi mno mpaka aibu. Huyu mdada kipindi fulani aliondaka kwao, na huyu mume akaomba samahani kwa wazee na kuwaahidi kuwa kitendo hicho hakitajirudia lakini naona mambo ni yale yale................................................................................................................................................................................................................... Sasa nilikuwa nauliza mimi kama raia mwema, naweza kwenda polisi kumshtaki huyu baba au nikaenda japo kwa tamwa kupata uongozi wa kisheria...........................mimi niko kinyume na talaka lakini ningetamani kumfundisha huyu mwanaume kitu ili asirudie kitendo kama hiki tena. Naomba kuwasilisha.