Naomba ushauri

Lisa

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
1,549
1,075
Habari zenu wana JF

Mm ni mwanamke , nimelelewa vizuri na wazazi wangu wote wawili, nimesoma nina advance diploma ya IT na kwa sasa naongeza ujuzi wangu ktk chuo cha IFM.

Nimeolewa na nina watoto wawili, mume wangu wa kwanza tuliishi miaka 8 , kutokana na mateso na vitimbwi kwa kweli nilishindwa kuendela kuishi naye nikaondoka.

nikaenda kupanga na nikawa ninaishi na watoto wangu . nilipata shida kwa muda lkn baadaye nikazoea. ninachoshukuru mungu nilikuwa na kibarua changu .

baada ya kiniacha tu, nikasikia kuwa ameoa na anaishi na huyo mwanamke kwenye nyumba tuliojenga wote. iliniuma sana , nikaamua kumshukuru mungu .
siku moja katika kuhangaika tulikutana mjini, akaniangalia kuanzia juu hadi chini na kuniambia maneno ya kejeli kiasi nilitamani ardhi ipasuke niingie. niliumia sana ,
siku nyingine akaambiwa kuwa huwa nakwenda kwenye maombi akasema na bado nitachanganyikiwa sana. kwa kweli namshukuru mungu alinifungulia mlango nikapandishwa cheo kazini na nikapata kwenda kusoma .

katika kukaa kwa muda nikapata tena mwanaume mwingine nikampena sana na nikaolewa naye na nikazaa mtoto mmoja na tunaishi vizuri sana , katika muda wote huo yule mume wangu wa kwanza alikuwa hanijali wala nn na wala hakuwahi kuleta matumizi yoyote yale kwa watoto. lkn cha kushangaza leo hii anadai watoto. na na kunitishia kuwa atanipeleka mahakamani kuninyanganya watoto.

kwa kweli inaniletea shida sana na kunitesa moyoni tena na kukumbuka mateso yote aliyokuwa ananipa tulipokuwa tunaishi wote.

wanajamii naombeni msaada nifanye nini ?
 
Jaribu kutafuta lawyer umweleze kila kitu watakusaidia, au vile vile unaweza kwenda kuwaona TAMWA hawa nafikiri ndio wanaweza kuwa msaada mkubwa kwako.
 
Pole sana dada yangu. Ukimpa watoto huyo baba hawataishi vizuri maana kuishi na mam wa kambo ni kazi ngumu sana. Nimefurahi kuwa una imani sana mshirikishe Mungu kwa hili utapata majibu. Mungu hamtupi mja wake mama
 
mimi ninavyojua watoto wakifikisha miaka 7 baba anaweza kuwachukua,shida inakuja je anawachukua watoto wanaenda kukaa na nani?? mama wa kambo!! usikubali dada, unaweza kutana na watoto wako wanauza maji baridi na sayona barabarani ukazimia kwa pressure!!

Ngoja tuone watu washeria hapa watasema nini!!!
 
Pole sana mwenzetu, ndo ya dunia haya, na hongera kwa kuyavuka yote haya. Suala la watoto kwa sheria na mila za kitanzania ni mali ya baba, nahisi utanyang"anywa tu. Lakini tafuta mwanasheria mzuri akusaidie.
 
thanks matisa
ila sina raha kabisa pindi niwaangaliapo wanangu na kuhisi siku moja sita kaa nao

nilimwita nikakaa naye chini nikamuomba awaache wakue wafike miaka 18 ndiyo awachukue maana hapo watakuwa wanatambua baya na zuri. lkn hataki
 
na watoto ukiongea nao wanasemaje?? simama mwanamke, mwanamke ni jeshi kubwa, mwanamke analeta ukombozi, mwanamke ni shujaa, usipende kuchukulia mambo kirahisi tu!! eti nimemwomba hataki, who is he by the way????? na siku zote alikuwa wapi??? mpeleke TAMWA.
 
pole sana.me nahisi huyo jamaa anataka kukukomoa tu na kufanya maisha yako yawe miserable.wala usibishane nae.we kaa kimya muangalie tuu.kwa jinsi ulivyosimulia alivyo hana ubavu wa kwenda mahakamani.anataka tu akupe heka heka akilini mwako maana kaona kila alilojaribu kukukomoa nalo umelihandle kwa umakini.ikitokea ameenda wala usipate hofu.vyama vya kutetea kesi za namna hii viko vingi.
 
karibu sana. Naelewa unavyojisikia ila usijali pia maana kila jaribu lina mlango wa kutokea. Mshirikishe Mungu tu utafanikiwa. Pia kama atakubali uwe unawaruhusu wanaenda kumsalimia baba yao mara moja moja ili nao wamfahamu. Kila la heri
 
Pole sana mwenzetu, ndo ya dunia haya, na hongera kwa kuyavuka yote haya. Suala la watoto kwa sheria na mila za kitanzania ni mali ya baba, nahisi utanyang"anywa tu. Lakini tafuta mwanasheria mzuri akusaidie.

yaani umenipigilia msumari wa moto moyoni mwangu , ungejua nilivyonyanyasika nao usingesema, halafu pia watoto wenyewe wa kike , si baadaye watakuja kuwa machangu , maana sina hakika kama watalelewa vizuri .
 
pole sana

as mama una nafasi nzuri ya kupanda/kuwaorient chochote utakacho kwa watoto.
Waandae kwa huo mzozo in your favour hata kama sheria itaondoa haki yako kuwa nao.(uongo mbaya ila hapa lazima ucheze na propaganda watoto wagomee kwenda kukaa na baba yao)
 
Pole sana mwenzetu, ndo ya dunia haya, na hongera kwa kuyavuka yote haya. Suala la watoto kwa sheria na mila za kitanzania ni mali ya baba, nahisi utanyang"anywa tu. Lakini tafuta mwanasheria mzuri akusaidie.
Ningependa kujua ni sheria ipi inasema hivyo na imeandikwa wapi
 
yaani umenipigilia msumari wa moto moyoni mwangu , ungejua nilivyonyanyasika nao usingesema, halafu pia watoto wenyewe wa kike , si baadaye watakuja kuwa machangu , maana sina hakika kama watalelewa vizuri .
Lisa inaonekana una uoga fulani na hicho ndio kitachokuponza
 
Pole sana dada yangu. Ukimpa watoto huyo baba hawataishi vizuri maana kuishi na mam wa kambo ni kazi ngumu sana. Nimefurahi kuwa una imani sana mshirikishe Mungu kwa hili utapata majibu. Mungu hamtupi mja wake mama

Kwa kweli huwa nafunga na kusali , namshukuru mungu huwa ananifunualia maombi yangu.

watoto wangu kwa kweli hawajui linaloendela na huyu baba yao mpya anawapenda sna na hawabagui kabisa. na mm napenda wa kwake pia siwabagui maana tulikutana kila mmoja ana watoto wawili ingawa wote walikuwa wakike. ndiyo mungu akajalia tukapata wakiume mmoja.

nashukuru sana kwa kunitia moyo. najua nitapata ufunuo wa matatizo yangu nawe katika kusali naomba uliweke na hili la kwangu.

mungu akubariki na wewe pia
 
Lisa inaonekana una uoga fulani na hicho ndio kitachokuponza

hapana si uoga ila niliongea na wazazi wangu nikawaeleza kila kitu wakanishauri nikae naye chini kwanza nimsikilize anachosema halafu tujue nn cha kufanya. na yote haya yasingetokea kama mungu angempa watoto maana huko kwa mkewe mpya hana watoto.
 
mimi ninavyojua watoto wakifikisha miaka 7 baba anaweza kuwachukua,shida inakuja je anawachukua watoto wanaenda kukaa na nani?? mama wa kambo!! usikubali dada, unaweza kutana na watoto wako wanauza maji baridi na sayona barabarani ukazimia kwa pressure!!

Ngoja tuone watu washeria hapa watasema nini!!!

Susy huo ni utaratibu ambao upo kisheria...lakini sio kwamba wakifikisha miaka 7 tu basi baba ndio ana haki ya kuchukua watoto na mama hana haki...HAPANA! Mahakama huwa inaangalia mchango wa malezi ya mtoto/watoto katika miaka hiyo 7, kama baba halikuwa hajali wala hatoi hela za malezi, basi mama bado yuko kwenye nafasi kubwa sana ya kupewa full 'custody' ya watoto hao. Pia, baba ana haki ya kuwa na wanawe kisheria...lakini sio kuwachukua na kuishi nao bila mahakama kujiridhisha kuwa baba atawajali hao watoto.

From the story you gave my sister, I dont see that man taking your children away from you...labda kinguvu, kimila, lakini sio kisheria! Ila uwe makini, ugomvi wako na ex-mwenza wako kuhusu watoto unaweza ukakuharibia uhusiano wako na mumeo mpya. Endelea kumomba mungu wako, mshirikishe mumeo mpya kila atua aone ni jambo linalomhusu pia...and relax, huwezi pokonywa wanao kisheria!
 
Jamani leo JF full masikitiko!Pole sana mpendwa!Kwanza kabisa ongea na wanao wajue kinachoendelea na utake sana kujua wao wangependa kwenda kukaa kwa baba yao?Kama ni ndio inabidi ubadilishe maoni yao!Japo sio sahihi ila ni kwa faida yao!Kama ni hapana unatilia mkazo kiasi gani mama wa kambo anaweza kufanya maisha yao magumu.Then tafuta mwanasheria na usiogope kwenda mahakamani maana watoto wakubwa hua wanaulizwa kama watapenda kwenda kwa baba yao au lah!Sasa kama watoto hawamtaki ataaibika yeye
 
hapana si uoga ila niliongea na wazazi wangu nikawaeleza kila kitu wakanishauri nikae naye chini kwanza nimsikilize anachosema halafu tujue nn cha kufanya. na yote haya yasingetokea kama mungu angempa watoto maana huko kwa mkewe mpya hana watoto.
Then if that's the case na baada ya kukaa na chini mkaongea kama wazazi na still akafikia hatua ya kuku threaten kukupelekea mahakamani then the best way to deal with it tafuta mwanasheria
 
Back
Top Bottom