Naomba ushauri

Habari zenu wana JF

Mm ni mwanamke , nimelelewa vizuri na wazazi wangu wote wawili, nimesoma nina advance diploma ya IT na kwa sasa naongeza ujuzi wangu ktk chuo cha IFM.

Nimeolewa na nina watoto wawili, mume wangu wa kwanza tuliishi miaka 8 , kutokana na mateso na vitimbwi kwa kweli nilishindwa kuendela kuishi naye nikaondoka.

nikaenda kupanga na nikawa ninaishi na watoto wangu . nilipata shida kwa muda lkn baadaye nikazoea. ninachoshukuru mungu nilikuwa na kibarua changu .

baada ya kiniacha tu, nikasikia kuwa ameoa na anaishi na huyo mwanamke kwenye nyumba tuliojenga wote. iliniuma sana , nikaamua kumshukuru mungu .
siku moja katika kuhangaika tulikutana mjini, akaniangalia kuanzia juu hadi chini na kuniambia maneno ya kejeli kiasi nilitamani ardhi ipasuke niingie. niliumia sana ,
siku nyingine akaambiwa kuwa huwa nakwenda kwenye maombi akasema na bado nitachanganyikiwa sana. kwa kweli namshukuru mungu alinifungulia mlango nikapandishwa cheo kazini na nikapata kwenda kusoma .

katika kukaa kwa muda nikapata tena mwanaume mwingine nikampena sana na nikaolewa naye na nikazaa mtoto mmoja na tunaishi vizuri sana , katika muda wote huo yule mume wangu wa kwanza alikuwa hanijali wala nn na wala hakuwahi kuleta matumizi yoyote yale kwa watoto. lkn cha kushangaza leo hii anadai watoto. na na kunitishia kuwa atanipeleka mahakamani kuninyanganya watoto.

kwa kweli inaniletea shida sana na kunitesa moyoni tena na kukumbuka mateso yote aliyokuwa ananipa tulipokuwa tunaishi wote.

wanajamii naombeni msaada nifanye nini ?

Csta Lisa Relax.
Kisheria hana uhalali wa kukun'yang'anya watoto ila tu endapo itaonekana kuwa watoto watapata malezi bora zaidi kama wakiwa na Baba na kama wao wataridhia kwenda kwa huyo baba yao mkorofi.
Tatizo lililopo ni ufinyu wa uelewa na utafsiri wa sheria ya custody ya watoto.Ila hana hoja za msingi kama wewe una uwezo na umeweza kuishi na hao watoto mpaka imefikia hapo ulipo.Watoto wakiamua pia watakuwa msaada mkubwa saana maana lazima wartaulizwa mahakamani kuwa wanaishije na wewe mama yao na wangependa kuishi na nani.So you have full support we kula shule relax wala hakufanyi kitu bangi zake tu!!
 
Pole lisa. Hizo ni changamoto tu za maisha.
Kuwa na amani na uzidi kumuomba mungu.
Natumai wadau watakushauri kisheria zaidi.
 
yaani umenipigilia msumari wa moto moyoni mwangu , ungejua nilivyonyanyasika nao usingesema, halafu pia watoto wenyewe wa kike , si baadaye watakuja kuwa machangu , maana sina hakika kama watalelewa vizuri .

Pole sana dada yangu. Mimi ni mwanamume, imenisikitisha sana hii story yako. Nachotaka kukushauri ni kuwa (1) una kila haki ya kuishi na wano sawa na yeye alivyo na haki. Lakini ukijipanga vyema nionavyo mimi kimazingira wewe ndiye ambaye unafaa zaidi kuishi na hao watoto. Kama walivyotangulia kukushauri wadau wengine. Nenda TAMWA waeleze kinaga ubaga hali ilivyokuwa baada ya ninyi kuachana, na hadi hapo ulipofika na jinsi ambavyo watoto umewatunza bila shida na hofu yako ikiwa hao watoto wataenda ishi naye. Ni mambo ambayo yapo wazi kila mtu anajua kuwa watoto wengi wanaoishi na mama za kambo huteseka kuliko wale waishio na baba za kambo.(2) Wewe ni mwanamke, naamini kwa kuwa umekuwa na hao wanao kwa muda mrefu ni wazi wanakupenda na ni rahisi kuwafanya wakakukubali wewe kwani hata mkienda mahakamani watoto wakisema hawataki kwenda ishi na baba yao bali na wewe hawawezilazimishwa!! SO STOP CRYING WOMAN, SHOW HIM THAT YOU ARE STRONG! I TRUST IN STRENGTH F YOU WOMEN. May God be with you.
 
nenda kwa mwanasheria. its that simple. Unaweza kufanya research yako mwenyewe kwanza kama kujua sheria ya ndoa, nk. Na kama analeta kesi unaweza kumuwajibisha yeye na kudai pia pesa za matunzi ya watoto. Nakushauri uanze ku-document vitu vyako tayari kwa mpambano.
Hao watoto wana umri gani?
 
Nashukuru kwa ushauri wako.
hata mm nafikiri ni hilo la kutaka kuniharibia ndoa yangu ndilo analo kichwani kwake.

maana nilipoachana naye nilikwenda kupanga mbali kidigo naye lkn eneo ni hilohilo tegeta, basi siku moja alikuw anapita na agri mm nimebeba mtoto mgongoni asubuhi nampeleka hospitali. akaniona lkn hata kuniuliza hakuniuliza wala kunipa lift ili niwahi walaaaaa, akapita kama hanijui ihali mtoto ni wakwake, nililia sana asikuambie mtu, na sitakagi kukumbuka maana nahisi simanzi. lkn nashukuru akapita msamalia akanipa lift na pesa za matibabu. yaani nilipata shida mm anayejua ni mungu.

nitapigana na nitasimama kwa miguu yangu I PROMISE THAT.

Go Girl! TAMWA ipo utapata msaada wa kisheria unaohitaji,na Mungu yupo kukutia nguvu.
 
wa kwanza yupo darasa la sita ana miaka 11

wa pili ana miaka 9 yupo darasa la nne

nyamayao nawapenda sana wanangu na nitapigana mpk damu ya mwisho kwa ajili yao. nilipokwa nakwenda kwenye maombi nilikuwa naomba mungu anibariki nilee watoto wangu wakue ili waje wanisaidie.

nakuelewa dear jinc unavyoumia, hata mie mzazi pia naelewa kabisa unavyo feel....mie bwana hata muda wa kwenda kuongea nae nicngekuwa nao nadahni ningeipeleka hii ishu kibabe babe kwanza kabla ya sheria, kazana mae watoto kulelewa na mwanamke mwingine na wewe upo ni big no...
 
Pole sana dada yangu. Mimi ni mwanamume, imenisikitisha sana hii story yako. Nachotaka kukushauri ni kuwa (1) una kila haki ya kuishi na wano sawa na yeye alivyo na haki. Lakini ukijipanga vyema nionavyo mimi kimazingira wewe ndiye ambaye unafaa zaidi kuishi na hao watoto. Kama walivyotangulia kukushauri wadau wengine. Nenda TAMWA waeleze kinaga ubaga hali ilivyokuwa baada ya ninyi kuachana, na hadi hapo ulipofika na jinsi ambavyo watoto umewatunza bila shida na hofu yako ikiwa hao watoto wataenda ishi naye. Ni mambo ambayo yapo wazi kila mtu anajua kuwa watoto wengi wanaoishi na mama za kambo huteseka kuliko wale waishio na baba za kambo.(2) Wewe ni mwanamke, naamini kwa kuwa umekuwa na hao wanao kwa muda mrefu ni wazi wanakupenda na ni rahisi kuwafanya wakakukubali wewe kwani hata mkienda mahakamani watoto wakisema hawataki kwenda ishi na baba yao bali na wewe hawawezilazimishwa!! SO STOP CRYING WOMAN, SHOW HIM THAT YOU ARE STRONG! I TRUST IN STRENGTH F YOU WOMEN. May God be with you.

Asante sana kwa kuguswa na tatizo langu , pia nashukuru sana kwa kunitia moyo. nitakaa kimya kwanza ili yeye aanze kwenda mahakamani , nimeshapata mwanasheria ameniambia nisubiri kwanza aanze , halafu hata nyumba tuliyojenga itabidi iuzwe na aanze kutoa matunzo ya watoto. nafikiri atajuta kunianza.

Nashururu sana wana JF wote mlioguswa na tatizo langu.
 
Lisa, mi nimedandia treni kwa nyuma....hebu nambie, huyu mmeo wa sasa na wanao wa mume wa kwanza wanaivana?
 
Habari zenu wana JF

Mm ni mwanamke , nimelelewa vizuri na wazazi wangu wote wawili, nimesoma nina advance diploma ya IT na kwa sasa naongeza ujuzi wangu ktk chuo cha IFM.

Nimeolewa na nina watoto wawili, mume wangu wa kwanza tuliishi miaka 8 , kutokana na mateso na vitimbwi kwa kweli nilishindwa kuendela kuishi naye nikaondoka.

nikaenda kupanga na nikawa ninaishi na watoto wangu . nilipata shida kwa muda lkn baadaye nikazoea. ninachoshukuru mungu nilikuwa na kibarua changu .

baada ya kiniacha tu, nikasikia kuwa ameoa na anaishi na huyo mwanamke kwenye nyumba tuliojenga wote. iliniuma sana , nikaamua kumshukuru mungu .
siku moja katika kuhangaika tulikutana mjini, akaniangalia kuanzia juu hadi chini na kuniambia maneno ya kejeli kiasi nilitamani ardhi ipasuke niingie. niliumia sana ,
siku nyingine akaambiwa kuwa huwa nakwenda kwenye maombi akasema na bado nitachanganyikiwa sana. kwa kweli namshukuru mungu alinifungulia mlango nikapandishwa cheo kazini na nikapata kwenda kusoma .

katika kukaa kwa muda nikapata tena mwanaume mwingine nikampena sana na nikaolewa naye na nikazaa mtoto mmoja na tunaishi vizuri sana , katika muda wote huo yule mume wangu wa kwanza alikuwa hanijali wala nn na wala hakuwahi kuleta matumizi yoyote yale kwa watoto. lkn cha kushangaza leo hii anadai watoto. na na kunitishia kuwa atanipeleka mahakamani kuninyanganya watoto.

kwa kweli inaniletea shida sana na kunitesa moyoni tena na kukumbuka mateso yote aliyokuwa ananipa tulipokuwa tunaishi wote.

wanajamii naombeni msaada nifanye nini ?

...Ohhh,
Mungu akupe nini! Mpe naye alee wanawe.

ilikuwa ni wajibu wake kuchangia malezi ya watoto,
kama ilivyo sasa anapotaka kuwachukua wanae awalee.
Usijitishe na doubts,...

Mpe kwa moyo mmoja, tena waambie watoto huyo ni baba yao,
nawe ni mama yao. Wana haki zote kwake na kwako pia.
Watoto hawana makosa.

La msingi, hakikisha mnakubaliana rights zote za kuwaona watoto,
iwe ni weekends, likizo, au kila baada ya muda fulani.
Incase watoto wanaathirika na mazingira, nyie wazazi wawili mkubaliane
watoto wapewe haki ya kuishi pale kwenye mazingira sahihi na makuzi yao.
 
Mbu huyu baba, mbona inaonekana hawezi hata kuwalea hawa watoto?
Kumbuka hapo, anaishi na mwanamke mwingine ambaye hana watoto/mtoto.
Mmmmh awe anayo hiyo neema ya kuwalea watoto wa mwenzie, vinginevyo,
watoto watakuwa watu wazima wenzie.

Ukiangalia historia ya huyu baba inatia mashaka kama ni kweli anawataka watoto kwa wema,
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

Kwa hiyo LD unataka kuniambia anawataka ili akawatie kwenye oven?

Otherwise uniambie we ni nabii, ila kiukweli baba naye ana haki ya kuwalea wanae.
 
Sina maana hiyo Babu,
Unajua kuna ile ukipima kabisa huyu baba baada ya kumuacha huyu dada,
Alikuwa anampita barabarani kama vile hamfahamu, hata wakati anamuona amebeba mtoto mgongoni tena mgonjwa
anampita. Halafu ukiangalia hata namna anavyowataka hao watoto, eti ataenda mahakamani, kweli jamani.

Bora angejirudi akaomba msamaha, na kuonesha ni kweli anatamani kuwalea watoto wake kwa moyo wa upendo.
Khaaaa mi Babu hii akili ya huyu baba binafsi sijaikubali hata kidogo.
 
Mbu huyu baba, mbona inaonekana hawezi hata kuwalea hawa watoto?
Kumbuka hapo, anaishi na mwanamke mwingine ambaye hana watoto/mtoto.
Mmmmh awe anayo hiyo neema ya kuwalea watoto wa mwenzie, vinginevyo,
watoto watakuwa watu wazima wenzie.

Ukiangalia historia ya huyu baba inatia mashaka kama ni kweli anawataka watoto kwa wema,

..naam LD, historia ya huyu baba kama tulivyohadithiwa na
mtaliki wake, dada yetu Lisa.

Kumbuka, mpaka sasa hatujapata upande wa pili wa shilingi,
maelezo ya Huyu baba, ili experiences zetu zi judge ukweli.

Character assassination ni jambo la kawaida baina ya wawili walioachana,
Sioni tofauti ya jambo hili hapa, ingawa kwa maelezo ya dada Lisa 'inaonekana'
kuna mapungufu ya hapa na pale kwenye judgements.

Kuna cases nyingi nazijua ambazo Mwanamke kwa kutumia kivuli cha haki za mtoto
ameweza kumnyima haki zake mwanaume kumuona/kuwaona watoto wake kiasi cha kupelekea
Uhasama mkubwa baina ya wazazi wawili na mtoto/watoto wao.

Ndio maana nasimamia hoja yangu, watoto ni haki ya wazazi wote wawili.
Huyo baba amekosa malezi ya watoto wake kwa miaka nane sasa,
Imagine, walipoachana (8yrs ago,) huyo mdogo alikuwa na 1yr na mkubwa 3yrs...
Kuna mushkeli mkubwa hapa.
 
Mheshimiwa Mosquito adui mkuu wa klorokwini lakini si Asprin, leo mi nna kazi moja tu kukugongea hii kitu:

The Following User Says Thank You to Mbu For This Useful Post:

Asprin (Today)

LD darling....Never rely on one sided story!....Hapa tungepata habari ya upande wa pili tungeweza kuhukumu. Kwa upande wangu, mme wa kwanza ataendelea kuwa innocent mpaka nitakapoisikia story ya upande wa pili.

Kumbuka wanaoachana, kila mmoja anamuona mwenziye ndo ana makosa!
 
...kabisa mkuu Aspirin, dawa ya kuponyesha kichwa maumivu yakizidi!
Pamoja na maelezo yakusikitisha ya dada Lisa, bado sikubaliani na maelezo yake haya;

Asante sana kwa kuguswa na tatizo langu , pia nashukuru sana kwa kunitia moyo. nitakaa kimya kwanza ili yeye aanze kwenda mahakamani , nimeshapata mwanasheria ameniambia nisubiri kwanza aanze , halafu hata nyumba tuliyojenga itabidi iuzwe na aanze kutoa matunzo ya watoto. nafikiri atajuta kunianza.

Nashururu sana wana JF wote mlioguswa na tatizo langu.

....kumkomoana na mzazi mwenzio sana sana ni kujenga uadui unaopelekea matatizo kwenye malezi ya watoto.
Si busara kuuza nyumba ambayo huenda itakuja kuwa urithi kwa hao wazawa wenu.

Kuna busara gani huyo baba auze nyumba, kisha ajipe gharama za kupangisha nyumba, huku nawe
ukimdai gharama za matunzo? ...humkomoi mtalaka wako tu, hata wanao utakuwa unawadhulumu.
Nadhani ni busara kutafakari kwamba, hakuna mshindi inapokuja suala la kugombania mtoto/watoto.

Maturity ni masikilizano, maelewano, na makubaliano.
Kila la kheri dada Lisa, wengi tumepitia huko.
 
Mheshimiwa Mosquito adui mkuu wa klorokwini lakini si Asprin, leo mi nna kazi moja tu kukugongea hii kitu:

The Following User Says Thank You to Mbu For This Useful Post:

Asprin (Today)

LD darling....Never rely on one sided story!....Hapa tungepata habari ya upande wa pili tungeweza kuhukumu. Kwa upande wangu, mme wa kwanza ataendelea kuwa innocent mpaka nitakapoisikia story ya upande wa pili.

Kumbuka wanaoachana, kila mmoja anamuona mwenziye ndo ana makosa!

Sawa babu,tuassume xmume yuko innocent. Makosa aliyoyatenda mkewe yanapaswa kumzuia yeye kuhudumia watoto wake? Kama siyo kwa nini hakufanya ivo huko nyuma?kwa nini anawataka sa izi kama sio kutaka kumharibia tu mwenzie amani?
 
Kwakuwa mimi ni Mwanasheria,naomba niwasilishe kwenu ushauri wangu mfupi sana wa kisheria.Lisa,waweza kutafsiri kifungu hiki? Hiki ndicho kifungu atakachokitumia Babawatoto.Ukishindwa kutafsiri wasiliana nami kwa thepresident2000@hotmail.com ukituma vocha kwenye no 0759230063 ili nikusaidie ushauri juu ya tatizo lako.Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971,kifungu chake cha 125 kinasomeka kwa kimombo:

125-(l) The court may, at any time, by order, place an infant in
the custody of his or her father or his or her mother or, where there
are exceptional circumstances making it undesirable that the infant be
entrusted to either parent, of any other relative of the infant or of any
association the objects of which include child welfare.​

(2) In deciding in whose custody an infant should, be placed the
paramount consideration shall be the welfare of the infant and, subject
to this, the court shall have regard-
(a) to the wishes of the parents of the infant; and
(b) to the wishes of the infant, where he or she is of an age to
express an independent opinion; and
(c) to the customs of the community to which the parties belong.
(3) There shall be a rebuttable presumption that it is for the good
of an infant below the age of seven years to be with his or her mother
but in deciding whether that presumption applies to the facts of any
particular case, the court shall have regard to the undesirability of
disturbing the life of an infant by changes of custody.(hapa panazungumzwa kuhusu miaka saba)
(4) Where there are two or more children of a marriage, the court
shall not be bound to place both or all in the custody of the same

person but shall consider the welfare of each independently
 
POLE SANA - KWANZA MSHUKURU MUNGU KWA KUMUWEKA WAZI HUYO MUME WAKO WA KWANZA NI WA NAMNA GANI - ULIDHANI NI MUME KUMBE NI SIMBA DUME. Pili Dada - watoto ni mali ya Mungu - Mungu ametupa tuwalee - sasa kama huyo mwanaume aliacha kuwalea ..... hana haki ya kuwa Baba wa hao watoto na ndio maana MUNGU AKAKUPA MUME MWINGINE - NA ISITOSHE AMEFANYIKA BABA(NOT BIOLOGICAL) MWEMA KWA HAO WATOTO

Watoto wote wanapenda UPENDO - na kama huyo Baba yao hakuwaonyesha upendo toka wadogo - sasa hivi ni ngumu sana wao KUMKUBALI - watoto wanajua BABA yao ni huyo mumeo wa sasa - PLEASE angalia sana watoto wasichanganyikiwe bado wadogo kwa kuambiwa - Baba ni huyu....wakati wanamjua Baba mwingine.............

Pili huyu mume wa kwanza hana mapenzi na watoto wake .............kama angewapenda mbona aliwaacha???? ANGALIZO - akiwachukua atawapeleka kijijini kwa bibi yao -.... kama ulivyoshauriwa:
a) Mwombe Mungu sana kuhusu hilo
b) Shirikisha TAMWA - kwani sidhani wanahongeka - wako serious na kazi zao - hao wanasheria wengine - kuwa mwangalifu pia kwani wengine wanahongeka na kuchakachukua kesi
c) Usikubali KUMPA WATOTO - He is very selfish, irresponsible, and stupid!!!!!
d) Waombee watoto wako wasijeingiwa na roho kama ya huyo Baba yao mzazi - ila wawe na roho kama yako ya UJASIRI na upendo

be blessed always
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom