Naomba ushauri wenu walimu, wazazi na walezi

Southern Highland

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
16,050
Reaction score
27,455
Huwa mnatumia mbinu gani kwa watoto ambao viwango vyao kielimu (darasani) wanashuka. Yani hapandi au ana mantain hapo hapo.

Napata shida nina mdogo wangu (ke) yani hapandi. Na wastani wake ni mbovu. Mwakani hapo ana NECTA. Naombeni ushauri na maoni yenu tafadhali.

Nina imani muda bado upo na uwezo ninao anaweza kubadilika.
 
1.Mpe uhuru akuchagulie masomo anayopenda yeye bila kutumia nguvu
2 uhuru akuandikie masomo asiyoyapenda yeye bila kutumia nguvu
3. Fuatilia masomo aliyochagua kuwa anayapenda na tafuta alama zake katika mitihani
4.Mchanganye katika makundi mbalimbali ya usomaji na asiwe na kundi moja na kwa marafiki fanya hivyo
5.Mtafutie mwalimu wa kumfundisha masomo ya ziada hasa kwa yale aliyotaja kuwa hayapendi kama ni binti mtafutie mwalimu wa kiume na kama ni wa kiume mtafutie mwalimu wa kike
6.Mpe muda mrefu wa kupumzika hasa katika kipindi cha mitihani
 
Yupo level gani
 
Kiongozi namba moja na mbili tayari nimeshafanya. Namba 3 ndio ninachofanya na sijaona ikisaidia. Namba 4 hapo sijafuatilia. Lakini ni kitu ambacho naona kinaweza kusaidia. Kuhusu mwalimu itabidi nilifanyie kazi.
 
Kwanza lazima ujue ana ndoto zipi?
anapenda shule?
anapenda walimu?
hajihusishi na mapenzi?

Mzoeshe tu kujisimamia mwenyewe ajue ndoto zake na masomo yake
vinahusiana
 
Takiwmu zinaonesha viwango vya ufaulu wa wanafunzi wanaokunywa wine vilikuwa vya juu kuliko wanafunzi ambao hawatumii. Embu jaribu kumpa nusu glass ya wine kila jioni kwa mda wa miezi sita uone kama ufaulu wake haujaongezeka!
 
Ana tatizo la kisaikologia. Labda kuna jambo lililotokea zamani likamfanya achukie kusoma. Au labda kuna hisia za mapenzi zinamsumbua. Au hapo shuleni kuna mwalimu au mazingira yanayomfanya achukie kusoma. Ukimuuliza ana tatizo gani hata yeye mwenyewe hawezi kukueleza. Zungumza naye tu 'kiujumla' kuhusu shule, marafiki zake, vitu anavyopenda, marafiki zake n. k. lakini usizungumzie masomo. Msililize kwa makini. Utagundua kuna kitu kiko kwenye 'sub-conscious' brain yake ambacho kinachukua ule muda wake wa ku-concentrate
 
Hmm.. Kiongozi kwenye ndoto zake ni ngumu sana kujua. Kuhusu mapenzi ni binti wa miaka 17 si rahisi kwangu kujidanganya hajihusishi na masuala hayo. So ipo 50/50 kwenye usawa huo.

Shule na walimu ye mwenyewe anaonyesha bado anahitaji na walimu anawapenda pia
 
Mchunguze anakipaji kipi, maana kusoma akili zetu zote hazifanani
Hmm. Hata kama kiongozi. Lakini hata awe na kipaji cheti cha form four ndio msingi ndugu. Yani walau hapo huko mbele tutaangalia tunafanyaje.
 
Ana tatizo la kisaikologia. Labda kuna jambo lililotokea zamani likamfanya achukie kusoma. Au labda kuna hisia za mapenzi zinamsumbua. Au hapo shuleni kuna mwalimu au mazingira yanayomfanya achukie kusoma. Ukimuuliza ana tatizo gani hata yeye mwenyewe hawezi kukueleza. Zungumza naye tu 'kiujumla' kuhusu shule, marafiki zake, vitu anavyopenda, marafiki zake n. k. lakini usizungumzie masomo. Msililize kwa makini. Utagundua kuna kitu kiko kwenye 'sub-conscious' brain yake ambacho kinachukua ule muda wake wa ku-concentrate
Mimi siyo mwepesi kumtambua mtu kisaokologia lakini ulichoeleza nahisi inaweza kuwa moja ya sababu. Nitajitahidi kulifanyia kazi
 
Takiwmu zinaonesha viwango vya ufaulu wa wanafunzi wanaokunywa wine vilikuwa vya juu kuliko wanafunzi ambao hawatumii. Embu jaribu kumpa nusu glass ya wine kila jioni kwa mda wa miezi sita uone kama ufaulu wake haujaongezeka!
Mh hii kitu..!!
 
Usisahau kufanya naye maombi huku na yeye akijikabidhi kwa Mungu siku kwa siku.
 
Back
Top Bottom