Naomba ushauri wenu nataka kujenga nyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba ushauri wenu nataka kujenga nyumba

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by ladyfurahia, Jun 29, 2012.

 1. ladyfurahia

  ladyfurahia JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 13,648
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  WanaJF habari
  naomba ushauri wenu kwani nataka kujenga ya kawaida ambayo haitagharimu pesa nyingi kwani
  mimi ni mtoto wa mkulima naomba maoni, na vifaa mniandikie hapa namna gani naweza kujenga nyumba ya
  kawaida yenye vyumba sita na sitting room na choo kiwe cha ndani maana kutoka nje naogopa
  waungwana nisaidieni basi kwa mchangowenu wa ushauri na maoni
  kiwanja ninacho kina urefu wa futi 50 x60upana sasa nianzaje kuweka hiyo ramani na je nitafanyeje
  nisaidieni kwa ushauri wenu
   
 2. n

  naivasha Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ulichoita kiwanja kina urefu wa mita 20 na upana wa mita 16!!!!
   
 3. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Mtoto wa Mkulima (kama Pinda?). Nyumba ya vyumba sita, choo bafu na seating room!!! bila shaka na parking ya Vitz! Haya bana, ngoja wajenzi waje washauri.
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
 5. M

  MAPE2012 Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  no ni urefu wa mita 18 kwa upana wa mita15
   
 6. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Atakuwa amekosea huyu. Maana yake kiwanja kina ukubwa wa mita za mraba 270 tu? Hiyo inatakiwa labda iwe ndo saizi ya nyumba na si kiwanja maana hata vile vya high density viko kwenye mita za mraba zipatazo mia sita hivi na kidogo.
   
 7. Mracho Ngongoti

  Mracho Ngongoti Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 90
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Square feet 3000 ni square mita 278.7. Engineerz mtusaidie tafadhali.!
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/271912-laki-5-nitajenga-nyumba.html
   
 9. ladyfurahia

  ladyfurahia JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 13,648
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  Nimesubiri huo ushauri hamjanijibu waungwana nisaidieni mwenzenu hasa mainjiiniazi pls
   
 10. ladyfurahia

  ladyfurahia JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 13,648
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  hapana ni upana na urefu kwa mita za miguu yaani unapima kwa miguu kwenda urefu na kurudi upana sijui umenielewa au bado ujaelewa
  yaani futi za mraba 50x60 ndugu yangu nadhani mpaka hapo utanielewa vizuri na je vifaa ni vipi naomba nitumie mchanganuo wako
   
 11. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Naona requirements zako kama hazijaeleweka vizuri,vyumba sita vyote vya kulala?kama ndiyo nadhani space uliyonayo haitotosha.

  Lakini kama una maana nyingine i.e sitting room,dinning, kitchen,other bedroms na masterbedroom inawezekana ila kwa kujibana sana,pia tambua unahitaji pia upate nafasi uweke pits za vyoo, so jaribu kuweka bayana zaidi, ila bila kukukatisha tamaa waweza pata nyumba ndogo yenye kila kitu ndani na ukafurahia.

  Je wataka kujenga wapi?eneo limepimwa?una mchoro wa hicho unachotaka kujenga,kama hujanielewa uliza kadili unavyojua nitakuelekeza.karibu!
   
 12. Prince Gm

  Prince Gm Senior Member

  #12
  Feb 2, 2014
  Joined: Apr 10, 2013
  Messages: 102
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Nipigie 0765088771
   
 13. Zanzibar Spices

  Zanzibar Spices JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2014
  Joined: Jul 14, 2013
  Messages: 7,543
  Likes Received: 2,021
  Trophy Points: 280
  Hapa utakumbana na madalali fundi hapa.
  Maana inaonekana kilamtu anaweka ugum ili uende chamber of kibano.
  Huko atakuletea mambo ya upembuzi yakinifu, Fizibility studies,menobility studies akiingia kwenye chemibility study umeibiwa.

  Kuna link humu ilieleza kwa kirefu sana,kwepa sana mtu kujifanya ni mtaalam wa mambo hayo eti aje akusaide kutokea humu,ujue ana njaa huyo utaumia.

  Sie wengine tumejenga na mafundi wa mtaani mpaka leo nyumba zetu zipo.
   
 14. serio

  serio JF-Expert Member

  #14
  Feb 3, 2014
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,925
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  Hahahaaa, umenichekesha. Lakini kama ana mchoro naweza kumuandalia schedule of materials bure, bei za materials ataweka kulingana na eneo anakoishi.
   
 15. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2014
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Mimi professional-wise ni QS (Quantity Surveyor) ninachotaka kusema ni hiki:
  1. Vipimo vya kiwanja ulichosema vinakanganya. Mara unasema ukipima kwa miguu mara feet hueleweki
  2. Vyumba sita (nikiamini una maanisha bedrooms maana ndio nomenclature - mtu akisema nyumba ya vyumba vitatu self-contained anamaanisha vyumba vitatu vya kulala) vinakataana na suala lako la ukubwa wa kiwanja ukuchukulia mahitaji ya nyumba ya vyumba sita vya kulala - corridors, sitting room,kitchen, bathrooms, utility etc etc.
  3. Jambo la kwanza kabla ya kuamua utumie 'materials' gani unahitaji mchoro ili ujue nyumba yako ina ukubwa upi na mpangilio wa vyumba ukoje! After that kukokotoa mahitaji ya vifaa vya ujenzi inaweza kufuata hence kufikia kwenye makadirio ya gharama za ujenzi wa nyumba husika

  Hitimisho ni kua taarifa yako na mahitaji yako yanakinzana, inahitaji majadiliano ya kina kati yako wewe mteja na mimi mtaalamu ili kufanikisha lile linalowezekana

  Naomba kuwasilisha!
   
Loading...