Internet itaingia kwenye "Wifi Router", server zote mbili zitaingia kwenye switch, server zinaweza pia kuingia kwenye hiyo Wifi Router kama hiyo wifi-router ni hizi za kawaida ambayo ina switch built in switch ina ports kadhaa za kuchomeka vifaa.
Natumaini hiyo access point ni hiyo hiyo Wifi Router au ni kifaa tofauti?
Kama ni hiyo hiyo weka hiyo alama ya AP juu ya Wifi router ili iwe clear kuwa sio kifaa tofauti.
Pia kuwa makini kuwa hizi Wifi-Router zinafanya kazi ya DHCP na DNS so angalia zisigongane na hiyo DHCP/DNS server yako, probably unaweza kuzizima hizo function kwenye hiyo router.