Ili upate ushauri mzuri inabidi useme matumizi yako muhimu ya hiyo projector, maana kuna projector zenye matumizi tofauti, tofauti. Kwa mfano:-
Multimedia projector:
Hizi ni nzuri kwaajili ya kuangalia movie, kucheza game na huenda zisifae kwaajili ya presentation. Bei yake ni kuanzia laki 4 (ebay price), mwanga wake mara nyingi huwa haufiki lumen 2500, na zinazo fika, bei hua juu kidogo.
Mobile projector:
Hizi huwa na bei nafuu sana kama elfu 60,000 (ukiagizia toka ebay), mwanga wake ni mdogo kiasi cha lumen 1000-15000, hivyo zitahitaji chumba kiwe na mwanga hafifu sana au giza kabisa kuweza kuona vizuri, zinatumia betri na zilizo nyingi hazitafaa kwa matumizi ya ofisini au shuleni ingawaje kuna baadhi (kama picopro) zinaweza tumika ofisini kwa presentation ya watu wachache, nazo huuzwa bei juu kulinganisha na nyingine za kundi la mobile projectors.
Professional projector:
Hizi zinauzwa bei juu kidogo kuanzia laki 6 (ebay price), zina mwanga wa kutosha kuweza kutumika hata ofisini au shuleni ie. Lumen huanzia 2500-3500 au zaidi. hufaa kwa matumizi yote.
Kitu kingine cha kuzingatia kwa aina yoyote ya projector ni lamp technology and lamp life. Maana tatizo kubwa la projector ni kufa kwa zile taa zake, na kuna taa ambazo zinadumu kwa muda mrefu bila kuharibika (long lamp life) na taa za muda mfupi (short lamp life). Lamp life hupimwa kwa masaa mfano 3500hrs (short life) au 30000hrs (long life). Upatikanaji wa spare ya taa na gharama yake pia ni vema kuzingatia, kwa kawaida kubadili lamp huweza kughalimu hadi laki 2 kwa professional projector, na wakati mwingine unaweza kukosa kabisa standard replacement kama projector imetengenezwa na kampuni uchwala, hivyo kukulazimu kuweka universal lamp ambazo mara nyingi hulipuka baada ya matumizi kidogo. Kwa Tanzania, wauzaji wa projector za epson ni wengi pia lamp spare hupatikana kwa urahisi, hivyo ni vema uanze kuchunguza brand za epson kama mdau mmoja alivyo shauri hapo juu.
NB: Kwa matumizi ya darasani (shuleni) usinunue projector yenye lumen chini ya 2500
Nawasilisha tafadhali.