Naomba ushauri wa Kisheria katika hili, nataka nivunje uchumba na huyu mwanamke

suala la kurasimisha ni gumu kidogo,kutokana na kuwepo kwa historia ya uhasama baina yangu na wazazi wake,na pia hata ningemuoa bado nisingekuwa na ushirikiano na familia yake,hivyo solution ni kuvunja uchumba
Poleh sana
Jipe muda kutafakari

Au upande wao pia wanakukwamisha kwa vigezo vya hela lakini wana malengo yao?..

Walishakutamkia wao kuwa uvunje uchumba?.
 
Kiongozi unaoa familia nzima? Kama unampenda ishi nae issue za kwao mwachie mwenyewe.
 
Poleh sana
Jipe muda kutafakari

Au upande wao pia wanakukwamisha kwa vigezo vya hela lakini wana malengo yao?..

Walishakutamkia wao kuwa uvunje uchumba?.
pesa sio tatizo,hawanidai kitu,na walipanga mahari kwa kunikomoa kutokana na uhasama baina yangu na wao,nikawalipa yote cash,ila nilichomwambia binti,asitegemee ushirikiano baina yangu na familia yake.

Sijui kuna mchango wa harusi kwao,au fulani anaumwa,au msiba asitegemee kuwa nitaongozana naye,ila yeye nilimpa ruhusa ya kwenda muda wowote akihitaji,
 
Poleh sana
Jipe muda kutafakari

Au upande wao pia wanakukwamisha kwa vigezo vya hela lakini wana malengo yao?..

Walishakutamkia wao kuwa uvunje uchumba?.
la kuvunja uchumba nahitaji nilifanye mimi,baada ya kumuona binti analeta mashinikizo kutoka kwao,kuwa lazima nishirikiane na familia yake.
 
mwanzoni nilikuwa na mtazamo kama wako,lkn baadae binti akabadilika na kusema hawezi kukubali kuolewa ikiwa sitakuwa na ushirikiano na familia yake,nikaona solution achape lapa akaungane na familia yake
Kama hataki kuolewa si aende zake tu. Mwenyewe nimekata mawasiliano na ukweni zaid ya miaka 2 na ndoa inasonga. Issue ya kwao ni yake though namuwezesha na na nilimuambia akitaka kata radar na kwetu anaruhusiwa.
 
Unajisumbua saana.

Cha kufanya kaa kimya....usionyeshe kucare lolote. Si yupo kwako hapo?

Wewe amka nenda kazini mwachie chakula cha kutosha. Ukitoka kazini kama hajapika ingia jikoni pika kisha lala.

Kesho amka uende kazini uendelee na hayo maisha. Akikuletea habari mama kasema hivi wewe jibu haya kisha kaa kimya.

Hii ndiyo namna ya kuishi na mwanamke asiyejua anaposimamia.
 
Kama hataki kuolewa si aende zake tu. Mwenyewe nimekata mawasiliano na ukweni zaid ya miaka 2 na ndoa inasonga. Issue ya kwao ni yake though namuwezesha na na nilimuambia akitaka kata radar na kwetu anaruhusiwa.
uzuri ni kuwa mkeo anaelewa hali halisi ilivyo ndo maana hakupi mashinikizo ya kushirikiana na familia yake,hapo mutadumu sana
 
Unajisumbua saana.

Cha kufanya kaa kimya....usionyeshe kucare lolote. Si yupo kwako hapo?

Wewe amka nenda kazini mwachie chakula cha kutosha. Ukitoka kazini kama hajapika ingia jikoni pika kisha lala...
hivyo ndo nilikuwa nafanya na hata ruhusa ya kwenda kwao nilikuwa nampa, lakini kila alipokuwa anakwenda kwao na kurudi,ndipo akawa analeta mashinikizo kuwa lazima nishirikiane na familia yake,hali ya kuwa anajua fika walipanga mahari kwa kunikomoa.
 
hivyo ndo nilikuwa nafanya,na hata ruhusa ya kwenda kwao nilikuwa nampa,lakini kila alipokuwa anakwenda kwao na kurudi,ndipo akawa analeta mashinikizo kuwa lazima nishirikiane na familia yake,hali ya kuwa anajua fika walipanga mahari kwa kunikomoa.
Ulikua hufanyi hivyo. Jikalie kimya. Akiyaleta usinsikilize wala kuonyesha unataka kujua aliyoyaleta kutoka nyumbani.

Kukaa kimya kutakusaidia akishajifungua. Ishi maisha yako. Muonyeshe yeye si kitu kwenye maisha yako unaweza kusonga bila yeye na unafanya kumsaidia tu kuwa hapo.
 
Wengine wameshaelezea hapo juu, sina sababu ya kurudia. Kwa ufupi ni kwamba;

1. Uchumba ni hatua kuelekea ndoa, na hatua hiyo haikufungi kama unavyoweza kufungwa katika ndoa, hivyo unaweza kukatisha hatua ya uchumba kwa taratibu au bila taratibu.

2. Upande wa pili walikupa orodha ya vitu na gharama ya kutimiza ili uoe, hawapaswi kubadilika, na ikiwa ndivyo basi una haki ya kudai pesa na gharama zako, kwa sababu huna hakika ikiwa baadaye hawatabadilika tena.

3. Kuhusiana na ujauzito: kuwa makini bro, kuna nyuzi nyingi sana zimo humu JF, pitia na zisome, zina ukweli ndani yake. Angalizo, usiwe mwepesi kujubali mimba, wapo wengi hulea mimba hadi watoto ambao sio wao-hii si sawa, labda kama umeridhia kutoa sadaka.
 
je sheria inatutambua kama wanandoa,ikiwa hatuna cheti cha ndoa,na hatujaishi pamoja zaidi ya miaka miwili?
Huyo ni Mkeo halali, kwani mmeshaishi zaidi ya miezi 6 (Tafuta Sheria za Ndoa 1971) halafu mtoto wa watu umeshambebesha Mimba, sasa haumtaki hilo ni kosa siwezi kusema ni ubakaji lakini ni uzinifu.

hapo huna sababu maalum ya kumuacha Bint maana sababu unayotoa ni hiyo 2m uliyotoa na gharama kuongezeka kila siku, au kukushinikiza uende kwao.

Tafuta mshenga wako wapige stop, leo mkeo na kijacho
 
Habari za asubuhi wana jukwaa la sheria,

Kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu. Nipo kwenye mahusiano na binti mmoja wa miaka 23, nilifanikiwa kwenda kwao kujitambulisha na nikawa kwenye mpango wa kupeleka posa mwezi January mwaka huu, lakini ukatokea mvutano baina ya mama yake binti na mimi kuhusu suala la imani, mama yake binti akitaka nifuate imani ya mwanawe ili nimuoe binti yake, nilimwambia binti tubaki marafiki na uhusiano uvunjike kwa kuwa sitaweza kabadili imani yangu...

Hakuna sheria yeyote hapo serious ya kukufunga, ukiishi na mwanamke kwa miaka 2 (I think) bila ndoa ana Kuwa conaidered mke kisheria!

Huyo ni muasherati mwenzako mmepeana mimba, ila issue hapo ni hiyo mimba, ambayo it will drain you kifedha!

Cha kufanya, muache huyo Mtoto hapo wewe kaa kwingine ila mhudumie kila kitu maana ni majukumu yako!

Usiendelee kula utamu wa watu, hapa ndo huwa utalogeka na hautatoboa nakuhakikishia!

Akijifungua mnunulie makorokoro kibao aone raha, ataenda kwao kuhudumiwa na mama yake, toa Support nzuri kabisa!

Akishaenda kwa Mama yake kuhudumia, wewe hamisha Nyumba kusikojulikana, ila usimwambie mtu!

Endelea kumpa some amount monthly akiwa kwao, fanya kwa mpesa na wema record kabisa itakusaidia baadae!

Usije ongelea au kukubali tena kuishi naye, wataenda ustawi wa jamii, wewe nenda waambie huna mpango naye, onyesha Support yahela na receipt zote za kuhudumie Mtoto!

Sasa kama wewe ni muhuni na utakuja kukwepa gharama za Mtoto usije fuata Huu ushauri, Mtoto ni jukumu lako na ni lazima umlee’
 
Ujauzito ni wako. Ueleweki. Weee sio wa kwanza Tza kuoa dini tofauti na hapa ndipo wengi ndio anguko letu. Sheria ya ndoa Mwanamme akiishi na mwanamke zaidi ya miezi 6 mna hesabika nyinyi ni mke na mume.

Achana na hayo mahadith hatujui kitakacho zaliwa kina neema gani.

Ushauri
Maji umryavulia nguo yaoge.. Ishe nae usimfukuze kwani umrshaingia kwenye ukurasa wa kuwa Baba..
 
Nimeshamrudisha kwao tayari kwa kuwa mzazi wake aligoma kutoa ruhusa kwa viongozi wa dini,wasitufungushe ndoa,kwani aliona kama anamuuza mtoto wake kwa sababu mahari yote ilipelekwa kwa wakati mmoja na yote,na wao walitaja mahari kwa minajili ya kunikomoa,
 
nimeshamrudisha kwao tayari kwa kuwa mzazi wake aligoma kutoa ruhusa kwa viongozi wa dini,wasitufungushe ndoa,kwani aliona kama anamuuza mtoto wake kwa sababu mahari yote ilipelekwa kwa wakati mmoja na yote,na wao walitaja mahari kwa minajili ya kunikomoa,
Huyo mama yake ana matatizo sanaaa...!! Kuoa mtu wa dini tofauti yataka moyoo sanaa yani muda wowote anaikana imani na kurudi alikokuwaaa.

Huyo ni mkeo kama walipokea mahari kabisa bhasi ni mkeo so either ukomae na mkeo maana wakwe zako chenga sanaa itakuwa wanataka kukupiga helaa tu wapuuzi hao au uwasikilize upoteze hela..mtoto na mke.
 
Hakuna sheria yeyote hapo serious ya kukufunga, ukiishi na mwanamke kwa miaka 2 (I think) bila ndoa ana Kuwa conaidered mke kisheria!

Huyo ni muasherati mwenzako mmepeana mimba, ila issue hapo ni hiyo mimba, ambayo it will drain you kifedha!

Cha kufanya, muache huyo Mtoto hapo wewe kaa kwingine ila mhudumie kila kitu maana ni majukumu yako!..
walinikomoa kwenye mahari 2.5M ,nikawalipa yote cash,baada ya kuwalipa mahari,wakagoma kutoa ruhusa kwa viongozi wa dini ili watufungishe ndoa kwa madai ya kuwa watakuwa wanamuuza binti yao.hivyo nikawarudishia binti yao
 
Mmmh...!! Hii kalii Wewe unawasikiliza wazazi wa demu na kufanya mambo kwa hasira ndio maana. Kama demu anakupa support ebu fanya yako na mkeoo hao wakwe njaa achana naoo. Me naona mkeo hana kosaa hapo kosa ni wewe kukosa msimamo. Mara ulipe maharii...mara utake kumfukuza mkeo..
 
Huyo mama yake ana matatizo sanaaa...!! Kuoa mtu wa dini tofauti yataka moyoo sanaa yani muda wowote anaikana imani na kurudi alikokuwaaa... Huyo ni mkeo kama walipokea mahari kabisa bhasi ni mkeo so either ukomae na mkeo maana wakwe zako chenga sanaa itakuwa wanataka kukupiga helaa tu wapuuzi hao au uwasikilize upoteze hela..mtoto na mke.
Siwezi kukomaa naye kwa kuwa yeye anasikiliza maelekezo ya mama yake na sio yangu,yeye alitakiwa asimame na mimi ukizangatia wazazi wake walishachukua mahari,
 
Back
Top Bottom