Naomba ushauri upweke umenichosha

Naomba ushauri upweke umenichosha

Mvuto unao? Wewe ni mrembo? Ukipita barabarani wanaume wanakupapatikia? Kama jibu "siyo" basi ameona alikosea kukuoa.
 
Rudia kuandika vizuri, hiyo yakukupa mgongo nimeona hiyo tu sasa hujasema alianza lini mpaka kufika Leo ,rudia kuandika ese yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba ushauri upweke umenichosha . Nipo kwenye ndoa kwa miaka 5 na miaka 31 haongei na Mimi, hataki mawasiliano, akija nyumbani haongei, ukimwambia BBY samahani naomba kuongea nawewe hataki. Akilala ananipa mgongo.nimejitahidi Kila mbinu lakini hataki kubadilika. Ila matumizi ananipa na Kila ninapo hitaji tukaechoni tuonge. Anajibu nashida gani nayeye wakati ananipa hela za kutosha. Ushauri wenu jamani nimechoka kuwa mpweke.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hamna wazazi, Mshenga, vipi kuhusu viongozi wa dini mlikofungia ndoa wanasemaje!?............Kama siyo chai kavu.....sijui!!!
 
Inawezeka amekosea. So!

Sent using Jamii Forums mobile app
.....................Hii hoja usiisikilize,siamini kama alikosea kukuowa na kama mlikuwa sawa hapo nyuma kisha ghafla akabadilika jua kuna sehemu alikuhisi vibaya may be kumsaliti etc.

Siyo kila mwanaume atakuambia kitu kwa uwazi labda ameona aendelee kuishi na wewe kwa manufaa ya watoto huku akiumia moyoni na anachokifanya anafanya akiamini yupo sahihi.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
.....................Hii hoja usiisikilize,siamini kama alikosea kukuowa na kama mlikuwa sawa hapo nyuma kisha ghafla akabadilika jua kuna sehemu alikuhisi vibaya may be kumsaliti etc.

Siyo kila mwanaume atakuambia kitu kwa uwazi labda ameona aendelee kuishi na wewe kwa manufaa ya watoto huku akiumia moyoni na anachokifanya anafanya akiamini yupo sahihi.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Asante. Kwaushauri, nifanyenini Sasa. Kama msamaha nimeomba Kama kunachochote nilimkosea. Lakini hakuna mafanikio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta kitu cha kukufanya uwe busy, tafuta kikundi cha vikoba ambacho mkivunja kikoba mnaenda Zanzibar kula bata bila waume zenu.

Tafuta bidhaa online uwe unaziuza kwenye status yako ya wasap mbayo nayo mumeo anaona halafu majibu ya wateja weka pia kama status...

Ukiona reaction zote hizo hana time na wewe hakuulizi hakugusi hapati wivu wowote na wewe, bibi tafuta mwanaume anayejielewa anza kuzungumza nae kihekima HALAHALA usidondoke kwenye penzi kimasihara.

Kama huna Kifua cha kuwa na ukaribu na mwanaume mwingine zaidi ya mmeo bila kukulala, endelea kukaa ndani mwako msubirie mmeo arudi mlale kimgongo mgongo.
 
Jalibu kuwa hot namaanisha jitaidi kupendeza na kutamanika akiwa kalibu na wewe then jitaidi kumpenda Mungu na kujali wazazi wake last thing alika ndugu zake kwa wingi nyumbani walishe,waveshe na yeye mpe zawadi lyk nguo nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jalibu kuwa hot namaanisha jitaidi kupendeza na kutamanika akiwa kalibu na wewe then jitaidi kumpenda Mungu na kujali wazazi wake last thing alika ndugu zake kwa wingi nyumbani walishe,waveshe na yeye mpe zawadi lyk nguo nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui Kama nipo sahihi: kamanilikosea nirekebishwe please. Nilijaribu kufanya haya yafuatayo pia.
Ikifika jion nilikuwa nikimuuliza nimpikie chakula gani anajibu chochote.
Akitoka kazini najitahidi kuvaa mavazi ya usiku nampokea kwa furaha namkumbatia namchumu haoneshi furaha anajibu Asante anapita na kuendelea na Mambo yake. Namfuata mmewangu nenda kaoge chakula kitamu nimekuandalia haoneshi ushirikiano, karibu chakula mmewangu anajibu Asante anakula kidogo akimaliza haongei analala. Nimejaribu kuwa mbunifu wa kubadi mazingira ya chumbani kwangu kwaajili ya kumshawishi. Lakini pia kuomba maongezi sehemu ambazo zingeweza kumshawishi kunisamehe huenda nilimkosea, lakini anajibu hakuna shida na yeye Yuko sawa na kusema Hana shida labda Mimi nashindwa kumuelewa . Na nilijaribu kumuacha kwa muda mrefu bila kumwambia chochote kwa kuhisi huenda anastress binafsi labda atabadilika laki Hali Ni ileile. Na ieleweke Mimi Ni mpambanaji na nakuwa biz kiasi na napata nafasi ya kufanya nyumba yangu safi na majukumu mengine ya nyumbani kwangu nayafanya inavo takiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom