Pole sana kwa changamoto,
Kua karibu na Mola wako kuliko ulivyowahi kua hapo mwanzo. Amini kabisa hakuna mtu au kitu chchote kinachoweza kukusaidia isipoku Allah
Jitahidi kukaa na udhu, dhikri zifanye nyakati zote ( subhanAllah, Allahu Akbar, la ilaha illa llah, la hawla wala quwata ila billah, nk, ayaat kursiyu baqara 255, suraht falaq, nas na ikhlas) ziwe zinapita moyoni mwako) swali rakaa mbili kisha mwombe Allah akuondolee hii mitihani, lia nae sema kama unamuona hakika atakusikia. Jifunze majina ya mwenyezi Mungu na maana yake yeye anajibu , anasikia , na anafanya jambo kua jepesi akitaka.
Ila hakikisha mfumo wako wa maisha unabadilika kbisa. Fanya aliyoamrisha mola wako na acha aliyokataza.
Pia usianze kuruka ruka mara kwa shekh mara kwa mganga mara kwa wachungaji, simama wewe pekee Allah atasikia
Ukisoma pia al fatha imaanishe utapata wepesi
(Mfno pale unaposema iyyak naabudu wa iyyaka nastaghiin hakikisha kwel ni yeye unamuuabudu pekee na kumtaka msaad yeye tu na si mwingin)
Kisha naapa kwa Allah kua kila kitu kitakaa sawa.
Ukiweza pia simama visimamo vya usiku