Msema yote
JF-Expert Member
- Mar 19, 2013
- 448
- 301
Hodi kwa mara nyingine tena wana jamii,
Bila shaka mu wazima wa afya tele. Ndugu zangu nimekuja jukwaani hapa kwa mara nyingine nipate msaada wenu wa kimawazo ni kwa namna gani naweza kuvuka huu mtihani uliopo mbele yangu. Bila kupoteza muda nianze kama ifuaatavyo;
Mwaka 2103 nilipanga kuwa ifikapo 2104 nitaacha kazi na kujiajiri kwani nilipenda sana kufanya shuguli zangu binafsi tangu nikiwa mdogo(nilipenda kujiajiri), hivo basi ilipofika 2014 kweli nilifata taratibu zote za kuacha kazi na hatimaye nikaacha na kuamua kujiajiri Namshukuru Mungu mambo yanaenda vizuri japo changamoto zipo ila naamini ipo siku nitafika.
Kiukweli shughuli zangu bado siyo kubwa sana hivo napata mapato kidogo tofauti na kipindi nilipo kuwa mwajiliwa nilipokuwa nikilipwa pesa niyngi, Sasa tatizo liko hivi:
Kuna binti ambaye ninaye kwa muda wa miaka 4 sasa na mipango yetu ilikuwa mwakani tuoane lakini mpaka sasa nimekutana na vikwazo vingi sana ambazo kiukweli vinaniumiza na kufanya utendaji wangu wa kazi upungue.
Kiukweli binti aninipenda sana nami nampenda mno tatizo ni wazazi wake hawataki binti yao aolewe na mtu ambaye mwenye maisha kama yangu(maisha ya wastani tu), wanataka aolewe na mtu mwenye pesa na aliye mtumishi au muajiriwa katika kampuni yoyote kubwa.
Kwani binti yao kamaliza chuo mwaka jana sasa mzee wake alimtafutia mtu ambaye ni bosi katika shirika flani hapo Dar na anahitaji binti yake aolewe na huyo jamaa, kiukweli inaniuma sana mpaka inafika hatua najutia kujiajiri.
Binti anaonekana kutokukubaliana na wazazi wake na hataki kwenda Dar kwa huyo jamaa japo mzee wake kamwambia amemtafutia na kazi hivo anatakiwa aende kufanya kazi huko.
Sifa za wazazi wa binti ni kama ifuatavyo
1. Ni waajiriwa katika mashirika ya flani ya kigeni hapa Mkoani.
2. Ni kabila lingne tofauti na mimi
Naomba niishie hapa kwani naamini nimeeleweka, nachoomba nisaidiwe ushauri nini cha kufanya ili nifanikiwe kuwashawishi wazazi wa binti waniozeshe binti yao kwani nampenda sana