Naomba ushauri: Niombe mkopo benki nikajiendeleze kimasomo au niombe mkopo kwa bodi?

sepema

JF-Expert Member
Jun 13, 2019
591
1,000
Salaam kwenu, kama kichwa cha mada kinavyosomeka.

Mimi ni mwajiriwa ambaye naweza kudhaminiwa namwajiri wangu kupata mkopo benki. Mwaka huu natamani nikajiendeleze kimasomo katika moja kati ya vyuo vikuu vilivyopo hapa nchini.

Kutokana na kwamba sitamudu gharama za masomo nataka kuomba mkopo.

Sasa nishaurini wakuu, nikakope benki au bodi ya mikopo?

Wasalaam!
 
Salaam kwenu, kama kichwa cha mada kinavyosomeka.

Mimi ni mwajiriwa ambaye naweza kudhaminiwa namwajiri wangu kupata mkopo benki. Mwaka huu natamani nikajiendeleze kimasomo katika moja kati ya vyuo vikuu vilivyopo hapa nchini.

Kutokana na kwamba sitamudu gharama za masomo nataka kuomba mkopo.

Sasa nishaurini wakuu, nikakope benki au bodi ya mikopo?

Wasalaam!
Mie nadhan bodi itapendeza zaidi...japo makato Yao yanachosha ila hawana limit ya katika ulipaji kama ilivyo kwa bank!
 
Bora uchukue benk mkuu,bodi ya mikopo hela yao kwa mwezi ni 15% kutoka kwenye mshahara
 
Benki na Bodi riba zao sawa sawa tu, sasa sijui benki watakupa kila mwaka au utalipa ada zote mara moja?
 
Chukua bank, kwani utaanza kulipa immediately, wakati unamaliza masomo na mkopo utakuwa umeisha kulingana na mda uliotaka nashauri kama mshahara unaruhusu unachukua wa mda mfupi, bodi utakutesa kwa mda mrefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chukua bank, kwani utaanza kulipa immediately, wakati unamaliza masomo na mkopo utakuwa umeisha kulingana na mda uliotaka nashauri kama mshahara unaruhusu unachukua wa mda mfupi, bodi utakutesa kwa mda mrefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shukrani mkuu. Hata mim naon bora wanikate nikiwa chuo ili nikirud uraiani nianze upya
 
Nataka nichukue ya miaka yote ibakie namna yakuilipa tu.
Vichekesho kama hivi huwa mnadanilodi wapi?

Nikuhakikishie tu hiyo pesa utaikula mwezi mmoja tu au utaibadilishia matumizi kabla ya semester mbili kuisha.
 
Wanufaika wapya wa Mkopo zaidi ya elfu 20 HESLB 2022/2023 | Majina ya Waliopata Mkopo
Habari njema kwa waombaji wote wa mkopo wa HESLB, Allocation ya mkopo bechi ya kwanza sasa inapatikana mtandaoni kuangalia allocation ya mkopo Tembelea Tovuti ya HESLB ya Maombi ya Mikopo na Mfumo wa Usimamizi https://olas.heslb.go.tz/index.php/olas/Olas

Nifanye nini nikikosa mkopo kwenye bechi ya kwanza HESLB?
Kuwa mvumilivu na subiri kwa sababu bodi ya mkopo inatoa majina ya waombaji wa mkopo waliopata mkopo kwa Bechi. Bechi za majina ya waliopata mkopo ni nyingi wakati mwingine hufikia tano au sita

Je nikisubiri hadi bechi zote za majina zikatoka na ikiwa sioni jina langu, nifanye nini?
Bodi ya mikopo hufungua dirisha kwa waombaji kukata rufaa kwa hivyo ikiwa unajiona kuwa una hoja, unaweza kukata rufaa
Je, nifanye nini ikiwa sipati mkopo baada ya kukata rufaa?
  • Lipa ada ya masomo na chakula cha kujifadhili na gharama za malazi.
Naweza kuomba mkopo huku nikiendelea na masomo?

  • Ndio mwaka ujao bodi itafungua dirisha jipya la maombi
Maswali baadhi ambayo naweza kukupa msaada angalau wa majibu kuendena na uelewa wangu
Je, iwapo nilikatisha(disco) masomo nifanye nini ili niweze kupata mkopo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) Soma hapa

Je, ni lazima nifuate taratibu gani ili nilipwe mkopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB)?

Ili bodi ifanye malipo, mnufaika lazima afuate taratibu hizi

1. Mfadhiliwa lazima ajiandikishe kikamilifu katika taasisi ya elimu ya Juu, vinginevyo itamfanya akose sifa ya kupokea fedha hizo.

2. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) lazima ipokee maelezo ya ziada ya wanufaika. Jukumu la kutuma taarifa hizo ni la taasisi ambayo wamekubali Wanufaika na kuwasajili kikamilifu.

Nyongeza:

iwapo mnufaika wa mkopo atajiandikisha katika taasisi ya elimu ya juu ambayo ni tofauti na ile ambayo TCU ilipeleka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB), mnufaika hatapokea fedha za mkopo hadi aombe kupangiwa upya au Kuhamishiwa mkopo.

Ikiwa mnufaika atabadilisha programu yake aliyoichagua awali, kiasi cha mkopo wake hakitabadilika hadi aombe kutengewa tena.

Mwisho, bodi ya mikopo Huendelea kufuatilia maendeleo ya mnufaika katika Vyuo vya Elimu ya Juu mara kwa mara ili kufanya uamuzi wa malipo.

Recomended Posts

 
Back
Top Bottom