Mungu hakukosea kusema ukweli humuweka mtu huru, na uhuru huo ndio unaoleta amani na faraja ndani ya mioyo ya wanadamu. Palipo na ukweli hamna mafarakano na mashaka. Nimefurahishwa sana na kitendo cha kumkwepa huyo X wako ili tu utunze heshima ya ndoa yako na wewe mwenyewe kwa ujumla.
Kama usiposema ukweli sasa hivi, Je ikitokea wao kwa wao wakaambiana unadhani mmeo atajihisi yupo salama kwako!? Na atafikiria kwanini muda huo hukumwambia. Unatmueka ktk hali kubwa sana ya mawazo.
Siku zote katika mapigano au katika mashindano ukimuona mtu amekushambulia na wewe ndo unajipanga ujue utamshambulia wapi. Hii ni indicator na umeoneshwa kuwa huu ni wakati muafaka wa wewe kufanya marekesho kwa Mme na X wako.
Ushauri wangu, mwambie mmeo ukweli wote kama ulivyoeleza hapa, na kama kuna mengine usisite kumueleza. Hata mume awe mkali vipi, kwa kesi ilivyo lazima atakusifu na kukuona wewe ni shujaa. Mueleze mmeo ukweli naye atakuelewa.
Nakutakia kila la heri!