Ukweli ndo utakuweka huru. Ukisubiri itakuwa mbaya zaidi. Umenikumbusha mchezo wa Jangala ambapo mwanamke alificha ujauzito wa mwanae na baadae ikawa huwezi kuendelea kuuficha. Mambo inabidi yawe hadharani. Ni hapo mumewe akamuulizia mke kwanini ulinificha kwamba binti yetu ana mimba. Mke alijibu niliogopa ungekasirika. Mume (Jangala) alimuuliza mke " Kwani sasa nilivyojua nimefurahi?".
Ukisema ukweli inaweza mume asifurahie kilichotokea lakini utakuwa umejijengea taswira ya kuwa mkweli siku za usoni. Ukinyamaza halafu ajue mwenyewe hatakaa akuamini kamwe. Maamuzi ni yako.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.