Naomba ushauri: Nimdhamini au niachane naye?

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,705
36,157
Ni mtu ambaye miaka 10 tulikutana katika harakati za utafutaji kazi. Tukapoteana tulionana mjini Dar mwaka jana.
Mwaka jana kibarua chake kiliota nyasi. Si unajua sekta binafsi mistake ndogo tu wanapita na wewe.

Familia ina hitaji kula, umri umeenda kahangahika kaamua aende kampuni ya Uzinzi Garda security. Huko kapata ila issue ni udhamini kawekewa vigezo vigumu.

Wanataka apeleke watumishi wa umma 2 wenye barua za mkono, picha, kopi ya NIDA, kopi ya kitambulisho cha kazi na barua zao za utambulisho kutoka serikali ya mtaa.

Kasema kupambana kutafuta wadhamini kachemka, anaomba msaada wangu hana namna. Sijui kama mdhamini mwingine kampata au ndo anataka aanze na Mimi.

Vipi wakuu nimdhamini, au nimwambie kuwa haiwezekani. Na kama namdhamini nimpe masharti yapi Ili kujihakikishia usalama wangu?

Thanks.
 
Kama umepoteana naye mda wa miaka 10 na hujui yaliyomtokea huko ni changamoto, cha muhimu:

- Angalia liability yako inaishia wapi, kama ni uzamini usio na masharti au liability msaidie.
 
Mbona issue ndogo sana hio, mdhamini kwa masharti ya mashahidi upande wako na wake dhidi ya dhamana yako.
Issue ni kwamba wanasema kama ataiba au ataibiwa lindoni na kukimbia wadhamini ndio tutapaswa kumpeleka au kulipa mali zilizoibiwa.
Hapo mashahidi wafanye nini?
Fafanua
 
Kwanza unatakiwa ujue maana ya kuwa mdhamini. Unamdhamini kwa lipi na ikatokea la kutokea utawajibika au utawajibishwa kwa namna gani. Pia uyo unayemdhamini unamjua kwa kiasi gani? Ndugu zake unawajua? Mahali anapoishi unapajua? Ikatokea ametoroka unajua pa kuanzia kumtafuta?
Kama utaamua kumdhamini basi jiridhishe mkuu jiridhishe.
 
Ni mtu ambaye miaka 10 tulikutana katika harakati za utafutaji kazi. Tukapoteana tulionana mjini Dar mwaka jana.
Mwaka jana kibarua chake kiliota nyasi. Si unajua sekta binafsi mistake ndogo tu wanapita na wewe.
Familia ina hitaji kula, umri umeenda kahangahika kaamua aende kampuni ya Uzinzi Garda security. Huko kapata ila issue ni udhamini kawekewa vigezo vigumu.
Wanataka apeleke watumishi wa umma 2 wenye barua za mkono, picha, kopi ya NIDA, kopi ya kitambulisho cha kazi na barua zao za utambulisho kutoka serikali ya mtaa.
Kasema kupambana kutafuta wadhamini kachemka, anaomba msaada wangu hana namna. Sijui kama mdhamini mwingine kampata au ndo anataka aanze na Mimi.
Vipi wakuu nimdhamini, au nimwambie kuwa haiwezekani. Na kama namdhamini nimpe masharti yapi Ili kujihakikishia usalama wangu?
Thanks.
tangu lini GARDA imekuwa Kampuni ya UZINZI??
 
Kupoteana miaka 10 si kipindi haba.. Mengi yatakuwa yalitokea hapo katikati.. Kumdhamini ni risk kubwa sana! Hata kama hana nia ovu lakini likitokea tatizo kazini na akaingia mitini mdhamini ndio utabebeshwa mzigo hasa kama unahusiana na fidia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom