Naomba ushauri nihakiki chuo gani kati ya hivi?

Said Mshana

Senior Member
Joined
Jul 10, 2016
Posts
105
Reaction score
152
Habari za wakati huu wana Jukwaa wenzangu, mm mdogo wenu nilifanikiwa kuomba vyuo vinne na namshukuru mungu majibu yametoka nimechaguliwa vyuo vyote hivyo nimekuja hapa kuwaombeni mnipe ushaur wenu ni chuo gani na koz gan nzur niconfirm itakayonisaidia hapo baadae.
Vyuo na kozi hizo ni;

1. NIT kozi ya Marketing and Public Relation
2. UDSM-Main Campus kozi ya Bachelor Of Arts with Education
3. TIA-Dar Campus kozi ya Marketing and Public Relation
4. MOCU-Kozi ya Procument and supply Chain Management

Kozi zote na vyuo vyote ni vizuri na ninavipenda ndo mana nimeviomba hivyo ningeomba kutokana na hali halisi ilivyo naomben ushauri wenu wa chuo kipi niconfirm kabla ya tare 17/10/2020 ambayo ndio mwisho wa confirmation

NATANGULIZA SHUKRAN
 
Nimetokea kuzipenda kozi zote na sina mtu wa karibu wa kunishauri ndo mana nimeamua kuja huku kwenye jukwaa ili niweze kupata japo ushauri ni kozi ipi niweze kuconfirm, ila kiukwel napenda zote japo hali halisi ya mtaani inanipa wakati mgumu nichague kipi niache kipi
Unataka kusoma chuo ili baadaye uwe nani ? Mwalimu? Marketing Officer? au Procurement officer
 
Kwa mimi ningekushauri ukasome TIA kwakuwa ni chuo nilichosoma ila coz changamoto ingawa UDSM pia ni kizuri ila iyo coz hapana kwaiyo TIA na UDSM ndio vyuo ingawa izo coz mimi hapana
 
Nimetokea kuzipenda kozi zote na sina mtu wa karibu wa kunishauri ndo mana nimeamua kuja huku kwenye jukwaa ili niweze kupata japo ushauri ni kozi ipi niweze kuconfirm, ila kiukwel napenda zote japo hali halisi ya mtaani inanipa wakati mgumu nichague kipi niache kipi
Nenda hiyo Bachelor of art with Education
 
Nimetokea kuzipenda kozi zote na sina mtu wa karibu wa kunishauri ndo mana nimeamua kuja huku kwenye jukwaa ili niweze kupata japo ushauri ni kozi ipi niweze kuconfirm, ila kiukwel napenda zote japo hali halisi ya mtaani inanipa wakati mgumu nichague kipi niache kipi

Achana kabisa na mpango wa Bachelor Of Arts with Education -unaweza ukapata mkopo chuo lakini baada ya hapo kwa zama hizi wengi hawajaajiriwa toka mwaka 2015, hata zikifunguliwa, competition itakuwa kubwa na mshahara ni mdogo.

Ningekushauri ufikirie zaidi Marketing & Public relations ya Hapo TIA, lakini uwe tayari kupambana sana, ukibahatika unaweza kuvuta mshahara mzuri makampuni binafsi zaidi.

Jitahidi uangalie unataka hasa kufanya kipi katika maisha na uwe na mpango wa kutoboa hata ukikosa ajira zaidi ya miaka 2 baada ya kuhitimu.
 
Haya mambo haya si mchezo nikicheki pale home bro kaua BCOM udsm tangu 2013 mpaka leo kaishia kuuza duka la mtu wa darasa la saba.
Kapige marketing na wakati unasoma hakikisha unaandaa plan ya ku survive mtaani maana ajira huku ni magumashi.
Mmmh mpaka naogopa
 
Ila mkuu jiandae kuja kuandika Uzi mwingine 2023 hapa, hizo program ni shallow sana mkuu.
 
Nimetokea kuzipenda kozi zote na sina mtu wa karibu wa kunishauri ndo mana nimeamua kuja huku kwenye jukwaa ili niweze kupata japo ushauri ni kozi ipi niweze kuconfirm, ila kiukwel napenda zote japo hali halisi ya mtaani inanipa wakati mgumu nichague kipi niache kipi
Hayo makozi uliyochagua ni ya hovyo.

Isipokuwa hiyo ya mwisho ya Procurement kidogo ni ya kijanja kwa sababu ukiisomea unaweza kufanya kazi kama procurement officer,store keeper,supply chain na ukikosa nafasi hizi kuna masomo mengi yanaingiliana na watu wa Finance and accounting una uwezo wa kujiongeza ukafanya kazi za kiuhasibu.

Ila hicho chuo sasa hata sikijui hicho sijui mocu
 
Yan procurement officer afanye kazi za finance na accounting?acheni kudanganya vijana jamani
 
Nimesema mambo yao mengi yanaingiliana.
Kwani wewe umeona kazi za finance ni ngumu sana ama?Hivi unafahamu kwamba miaka ya nyuma kabla kozi za procurement hazijaanza watu waliosomea finance ndio walikuwa wanafanya kazi za procurement?Hapo utofauti ni majina tu ya kozi lakini mambo ni yale yale tu.

Finance anaweza akawa procurement officer but vice versa is not possible..
 
Hakuna kazi ngumu kwenye finance kusema mtu wa procurement akashindwa sema wewe bado una ushindani wa kishule mimi ni mkongww nipo kwenye system miaka mingi wakati wewe bado umekariri.

Back
Top Bottom