Fourier
JF-Expert Member
- Dec 24, 2014
- 218
- 76
Juzi wakati natoka nyumbani kwenda katikati ya jiji nilikutana na msichana mmoja ndani ya daladala. Huyu Msichana Alikuwa mzuri kiasi kwamba alivyokuja kukaa kwa Seat yangu moyo ulianza kunienda mbio nisijue nianze na lipi, Maana kwanza alinikuta na earphone masikioni na bus lilikua empty kiasi kwamba raia wengine walikua wanatukodolea macho kama vile walikua wanataka nione nitafanya nini.
Tulipita Foleni Za Mataa Mbili Tatu Bado Nikifikiria Nimuanzaje, Mara Fasta Wazo Likaja Nikajfanya Nashuka Kituo Fulani Cha Mbele Ambacho Sikufahamu na nilikua namuomba anikumbushe tukikaribia.
Dada mwenyewe alikua mcheshi kwani nilivomsifia kuwa kapendeza alicheka sana na kisha akaniambia na mimi nimependeza, hamadi tukakaribia kile kituo na akaniambia, hapo Nilikuwa sina jinsi ni kushuka tuu japo safari yangu ilikuwa inaendelea mbele mpaka mwisho wa daladala. Lakini sikushuka hivihivi kwani nilifanikiwa kupata namba ya yule mrembo.
Sasa suala linakuja tangia nimpigie simu usiku wa ile siku, zimepita siku mbili hatujawasiliana na leo nimetoka kumtumia message tangia jioni mpaka sasa usiku huu wa saa tatu hajajibu.
Naombeni ushauri wakuu kama ni sahihi kuanza kumpigia pigia kwa simu au nisubiri kwanza.
Asanteni.