Naomba ushauri: Nataka kuachana na Mwanamke ninayeishi naye

Kwanza Pole lakini binafsi naona hata wewe una makosa from the beginning kwanini umruhusu yeye ndo akupangie ilihali wewe ndo baba mwenye nyumba? Kitendo cha wewe kila unapokuwa na uhitaji uanze kujieleza kwake tayari kimepunguza kitu flani kwako


Uamuzi upo mikononi mwako ukitaka anza sasa kuya badilisha toka kwwnye huo utumwa mkalishe chini mpe mipango mipya namna unataka mambo yaende alafu kuwa serious kama hayupo tayari piga chini usiishi kuwafurahisha watu au kwakudhani watu wtakuchukuliaje


Maisha yenyewe ndo haya utaishi nq stress mpaka lini? Ma single matha wana asili ya upole huyo umempatia wapi mpaka akupelekeshe kiasi hicho? Punguza upole na wewe chukua hatua sasa onyesha utofauti .......
Asante
 
Mwanamke akizaa anakuw na confidence za ajabu na roho mbaya wachache sana hawana izo mambo ila anajiamini kupitiliza inaboa anajifanya yeye ndo yeye ndo maana hawaolewi wengi
Kweli maana mpaka akawa single mother maana yake ana tatizo ndio maana hakuolewa

Sasa sisi kujitia ujuaji tunawavagaa tu hata bila kufuatilia historia
 
Hakuna kitu kibaya na kinacho waangamiza watu wengi sana kama kufanya maamuzi yanayohusu maisha yako kwa kutazamia maoni na mitazamo ya watu wanaokuzunguka.....

Wewe ndio nahodha wa jahadhi la maisha yako....wewe ndio unatakiwa ukabiliane na kupambana na dhoruba kwenye jahadhi la maisha yako....mustakabali wa jahadhi la maisha yako liko mikononi mwako.......ushupavu, umakini na ujasiri ndio vitaamua kulifikisha salama jahadhi la maisha yako nchi kavu au kulizamisha........

Shahidi wa kwanza wa maisha yako ni wewe....muda mwingi unatakiwa kusema na nafsi yako na kuliko mtu mwingine yoyote....jambo lolote linalo hatarisha afya yako, ustawi wa uchumi wako, amani ya moyo wako na nafsi yako unapaswa kulifanyia maamuzi magumu bila kuangalia pembeni.........

Kumbuka kuwa....
Wanaohudhulia mazishini ndio wanaohudhulia msibani........

Akili KUMKICHWA......
Asante sana
 
Pole sana, halafu wanaume wasikuhizi sijui mpoje! Wazazi wenu hawakuwalea vizuri, kupishana mwaka sio sababu ya dharau au kwasababu alishapata mtoto, wanawake tuhangaike na kina Baba chanja na nyie tena? Unashindwa vipi kumdhibiti mwanamke!
 
Najmkushaur, dawa ya mwanamke Ni mwanamke mwenzie.

Tafuta mchepuko mpuuze ukapoze stress zako uko, atajirekebisha mwnyw

Mwenzio Mimi nna mchepuko, na Sina tatizo na Hilo

Vinginevyo unataka ufe siku so zako shehe
Ili uwe na mchepuko uwe na hela, Mwenzio si nakabidhigi hela kumbe najipiga pin

Mwanaume usipokuwa na hela hufurukuti
 
Hivi ndivyo navyojua lakini kuna namna alinizugaje sijui nikajikuta huwa tunabwaga tu mzigo mezani wote

Mpaka nakosa hela kuwasaidia wazee wangu

Halafu ana maneno fulani ya uropofu yanania hasira sana

Huyu nikiendelea kukaa naye nitafanya maajabu
Badili formation hiyo 4 4 2 tushapigwa....weka striker mmoja mbele...anzia kukabia nyuma 5 4 1....acha kulialia....!! Tengeneza kipato cha pembeni....kwamisha mshahara hata niazi 2...nyie watu vp lkn mbona mankosa ujasiri....!! Upendo sio dhambi wala utumwa...embu badilika mkuu kuwa strong wkt mwingine huna haja hata ya kuumia...nguvu!!
 
Kwahiyo mkuu unaona nibora uendelee kupata strees kwajili mmesha anza kufanya maendeleo, ivi unaji sacrifice kwajili tu mmesha nunua labda kiwanja au mmesha weka msingi ....nahisi tatizo lipo kichwani kwako bado ndomana huyo mwanamke anatumia advantage
Hakuna mkamilifu mkuu sikatai huenda nina tatizo

Slow learners huwa mpaka tusanuliwe ndio tunasanuka
 
hawa watu ni shida japo sio wote, wenye uzoefu wanaweza kulitolea ushuhuda, yalinikuta, mwanzoni unaweza kujilaumu kwa nini ulichelewa kumfahamu kumbe anakuingiza kingi anyway siamini kama wote wako hivyo
Wewe unaelewa kumbe

Mwanzo huwezi kujua kama unaingizwa mkenge
 
Hakuna kitu kibaya na kinacho waangamiza watu wengi sana kama kufanya maamuzi yanayohusu maisha yako kwa kutazamia maoni na mitazamo ya watu wanaokuzunguka.....

Wewe ndio nahodha wa jahadhi la maisha yako....wewe ndio unatakiwa ukabiliane na kupambana na dhoruba kwenye jahadhi la maisha yako....mustakabali wa jahadhi la maisha yako liko mikononi mwako.......ushupavu, umakini na ujasiri ndio vitaamua kulifikisha salama jahadhi la maisha yako nchi kavu au kulizamisha........

Shahidi wa kwanza wa maisha yako ni wewe....muda mwingi unatakiwa kusema na nafsi yako na kuliko mtu mwingine yoyote....jambo lolote linalo hatarisha afya yako, ustawi wa uchumi wako, amani ya moyo wako na nafsi yako unapaswa kulifanyia maamuzi magumu bila kuangalia pembeni.........

Kumbuka kuwa....
Wanaohudhulia mazishini ndio wanaohudhulia msibani........

Akili KUMKICHWA......
Umenena vema
 
Napitia majuto makubwa sana, Nikionaga nyuzi za kupondea masingle mother humu inaniuma natamani nisimame jukwaani niwaambie wale ambao hawajaoa wasikilize vizuri maonyo kuhusu single mother

Niliamini mwanamke ni mwanamke tu, Upumbavu

Acha kuwalaumu masingle mother mkuu changa karata zako vzr...!! You r a man, nyumbani panatakiwa pawe mahali pa kukimbilia, pa amani, pa furaha sio pa majuto.

Alafu sio kesi inaamuliwa nyimbani toka kidogo, nenda hata baagmoyo mkapimzike huko, mle mfanye yenu hata week.

Ngumi azisaiidii ndio maana mnaishia jela au kuchomana, ukishindwa basi bwaga manyanga, hasara roho pesa makaratasi.
 
Watu tunahangaika kupata waume bora wengine wanawasumbua dunia hii haina usawa kabisa jamani!

Nakushauri pima hayo maendeleo ambayo mlishaanza taabu utakayopata maisha yako yote, angalia tu usije toa roho ya mtu kwa stress, anza kama bongo movie ukipata mshahara toa pesa ya chakula nyingine baki nayo, halafu hapo simama kama mwanaume sio kulia lia hapa wee dogo!
 
Sawa lakini approaching yake kwangu ndio tatizo, Wanawake mnakosea namna ya kuzungumza na wanaume angeniuliza nilimaanisha nini kistaarabu ningemweleza maana binti hajaenda kwao kitambo halafu sikuwa serious ilikuwa stori ya kuzugia nilikuwa napita zangu nikamkuta anaosha vyombo tukazungumza nikasepa

Sasa nilivyowaka kwanini ananitaka nijieleze kwa kuongea na binti ndo akashuka eti ooh nilitaka kujua kama kwao wamemuulizia. Wangemuulizia si ningemwambia maana tunalala kitanda kimoja
Sasa hilo la dada wa kazi ndio la kukialia mkuu? Inshort ukiona mkeo anakupigia simu na unahisi atakuboa uko kazini... mwambie niko busy lets talk at home, akikomaa kata simu, ikiwezekana zima.

kuwa nunda, kijana embu gangamala basi mkuu kesi zingine hadi wadada wanatushangaa humu....!!
 
Back
Top Bottom